LUCKYHUSTLER
Member
- Jul 9, 2012
- 14
- 11
*UHURU WA KUFUNGA MLANGO.*
Ndugu Paul ( siyo jina halisi) baada ya kutumikia kifungo cha miaka kumi na saba jela kwa kosa la kumuua mchumba wake bila kutarajia siku alipomfumania, alipotoka jela alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Erick kuzungumza naye kwani aliamini ndiye mtu pekee wa kumsaidia ( the only friend) hasa baada ya kuwa amemsikia Erick kupitia motivational talks alizozifanya kipindi akiwa gerezani.Ndugu huyu alipotoka jela aliomba apelekwe kwa mchungaji yeyote akaombewe *kwahiyo aliaamua kuanza na Mungu.*
To cut short a long story bwana huyu baada ya kutoka jela mara nyingi alitembea mikono nyuma hii ilitokana na athari ya kufungwa pingu muda mrefu hivyo amezoea kutembea hivyo. Usiku wa kwanza baada ya yeye kutoka jela wakati anakwenda kulala alimwambia rafiki yake kwamba *LEO KWA MARA YA KWANZA NITAFUNGA MLANGO MIMI MWENYEWE BAADA YA MIAKA 17 YA KUWA NAFUNGIWA MLANGO.* Nilipoisikia stori hii nilitafakari sana mambo mawili la kwanza uhuru wa kufunga mlango na la pili ni uhuru wa kuwa huru hata baada ya kuwa na uhuru wa kufunga na kufungua mlango.
Uhuru wa kufunga mlango unatupa picha ya kuona thamani ya vitu tulivyopewa bure na Mungu ; - kutembea, kushirikiana na kufanya mambo kwa hiari yetu wenyewe.Uhuru huu wa kufunga mlango hujenga mazoea ambayo huathiri uhuru wa kuwa huru hata baada ya kuwa huru kufunga mlango. Kwenye hiyo stori huyu bwana hata baada ya kutoka jela alitembea mikono nyuma si kwa kupenda bali ni mazoea yaliyojengwa na kitendo cha kufungwa pingu muda mrefu. Hata alipokuwa huru kimwili bado alikuwa na ufungwa wa kiakili ( slave mentality).
Uhuru wa kufunga mlango unapatikana pale tu yule aliyekuwa ameupoteza huo uhuru anaporejeshewa uhuru wake. Ila uhuru wa kiakili unamtaka mhusika afikiri nje ya boksi (*Think out of the box*). Kila mtu bila kujali kama amepoteza uhuru wake wa kufunga mlango ama la analo boksi! Na ili ufikiri nje ya boksi lazima ujue boksi lako linalokushikiria. Boksi ni mfumo wa kufikiri tuliouzoea, mfumo wa kufanya mambo kwa mazoea. Boksi ni mipaka tuliyojiwekea katika akili zetu ikihusisha kile tunachokijua sasa.Ukitaka kuwa na fikra tunduizi (critical thinking) ni lazima ujizoeze kufikiri mwenyewe usifuate mkumbo/mazoea pia usijiwekee mipaka yaani ufikiri nje ya boksi.
Fikiri furaha aliyokuwa nayo huyu ndugu kwa kuwa huru kufunga mlango wake mwenyewe baada ya miaka 17, pia fikiri changamoto alizokumbana nazo kwenye maisha ya kawaida mpaka alipokuwa huru kifkra ni lazima ilimpa changamoto sana. Kwani alikuwa huru kimwili ila akili yake imekuwa programmed kufikiri kama mfungwa japo yuko huru.Kila alipotembea aligeuka geuka nyuma kutizama kama kuna askari magereza anam take care! kumbe yuko huru kimwili.
Chunguza pia maisha yako hata kama una uhuru wa kufunga mlango wako, angalia maboksi uliyonayo yafanyie kazi kwani yanakuzuia kufikia kiwango cha ubora unachostahili katika lile ulifanyalo.
_Think out of the box._
*Goodluck Edington Moshi.*