NgomaNzito
JF-Expert Member
- Jan 10, 2008
- 559
- 26
Kwa masikio yangu alituhumu wazushi wachonganishi lakini si suala ambalo ni la ukweli.unaelewa watanzania wengi wavivu kufanya uchunguzi.hupenda kuzusha na kusubiri alyezushiwa ajibu ndipo aanze kuhoji.huu si uandishi.Naamini uandshi mzuri ni kufanya uchunguzi ndipo aundike habari za mtu.uandishi wa namna hii ndio wenye maana na hata mtu ukisoma unapenda mwandishi aendelee kuandika.Tatizo la uzushi lipo hata kwetu kwa baadhi ya wana JF.
Unamaanisha Kubenea alituhumu watu kwa habari asizokuwa nazo? mbona tumeona mengi ameanika yakiwa na vielelezo? mbona waliotuhumiwa basi hawakwenda mahakamani kama walivyodai wamumalize aache kutoa habari za uongo? Kwanini wanamwandama kwa kummwagia tindikali, prezidaa kuchimba mkwara na mengine kama kufunga tovuti yake?
Akilimtindi,Nimekupata sawia ngoma nzinto, hili aliliruhusu mwenyewe na bahati nzuri limeikaba serikali yake mwenyewe. Hakujua kwanini Mkapa alikuwa mkali kipindi cha serikali yake? Sasa yeye amekuwa mpole utadhani yeye ndio msafi, kumbe naye fisadi. Sasa uhuru huu uliopo haufai kutunyima tena maana tumeshapata akili kutokana na uhuru huu huu, la msingi yeye na wenzake wajisafishe hapo uhuru huu huu utatumika kuwasifia na kuwapongeza kwa kujitoa muhanga kwa ajili ya watanzania.
Mimi nina uhakika waandishi wetu wengi wa habari hawafanyi utafiti wa kina kwenye habari zao nyingi ndio maana mwezetu hapa juu kaeleza kuwa inafikia mtu kuwa na hamu ya kuendelea kusoma habari yenyewe.
Pia habari nyingi haziandikwi kwa upana unakuta news iko very shalow sasa kama inamhusu mtu ndio kabisa data zinakuwa fuupi ndio maana wanaambiwa ni makanjanja.
Tuwape changamoto waandishi wetu wapiganie uhuru huu tulionao
Akilimtindi,
Nadhani uhuru haukutolewa na "yeye mwenyewe" kama ulivyosema. Uhuru tunaotumia unatolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Toleo la 2005.Turejee Ibara ya 18 ya Katiba, na nina nukuu " kila mtu a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake,
b) anayo hki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka
ya nchi
c) Anayo uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika
mawasiliano yake,
d) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio
mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia masuala
muhimu kwa jamii.
Hakuna atakayetueleza kuwa ufisadi huu mkubwa si jambo au tukio muhimu kwa maisha ya Watanzania. Serikali kama haitaki kuchokonolewa ilikuwa na wajibu wa kutoa "taarifa sahihi" kwa mujibu wa Katiba, na kwa kuwa haikutoa "tukitafuta" tusilaumiwe. Ni haki yetu.
Isitoshe Ibara ya 20 inaenda mbele zaidi,
20(1) kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na ....kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo". Kama kwa kutoa mawazo yetu, na "kuwasema mafisadi..." anayedhani tumevunja Sheria ya nchi ajitokeze hadharani na aeleze ni sheria ipi ya Taifa hili tumevunja. Tatizo letu ni kukosa ushujaa na ujasiri katika kutetea haki, maslahi na rasilimali za Taifa letu, ambazo ninarudia tena, si za Rais, wala Serikali bali ni zetu, na Rais na Serikali tumewakabidhi kuzitunza tu kwa dhamana. Hivyo Akilimtindi, naungana nawe, lakini nadhani haki hiyo tusipewe na mtu, awe Rais, au nani bali tupewe na Katiba na sheria za nchi. anayesema kuwa tunachonganisha, tunachochoea naye awekwe kwenye mizani kupimwa anamtetea nani na kwa maslahi ya nani. Nikisema hivi, ni dhahiri ninapinga kabisa kuwasema tu watu, kuwaseng'enya, kuendekeza umbeya. Lakini tunapokuwa na tetesi, japo Dogo, Serikali inawajibika kutoa majibu sahihi kwa kuwa inavyombo vya uchunguzi, nyaraka zote ziko mikononi mwake. Isipotoa isitulaumu kuwa kuna uchochezi bali ijilaumu kwa kutotekeleza vizuri majukumu yake, tena ya Kikatiba. Wenye kujua haki zao, Katiba, na Sheria za nchi hawatatishwa hata kidogo, na Mhe. wa Awamu ya Tatu aling'anka na watu kufyata kwa vile tu vyombo vya Habari na Watanzania walivumilia wakiamini "usafi wake.." kumbe mambo tofauti. Tumeumwa na nyoka, hata jani tu latutisha sasa na hatutaachia kamwe. Tuungane, Tushikamane, Uhuru utarejea unakostahili, haki zitalindwa na Rasilimali zitalindwa. Kama tulipoibua tukaambiwa ni kelele za mlango na hazimzuii mwenye nyumba kulala, na leo yeye mwenyewe aliyetoa kauli hizo katamka hadharani, tena kupitia Bunge Tukufu kuwa ni kweli, na kuwa asilimia 75 zitarejeshwa na kuelekezwa kwa mkulima Tunataka nini zaidi, akiri au aombe msamaha vipi? Hii siyo kusema ninakubaliana na aliyosema, La hasha, amezua maswali mengi zaidi kuliko majibu. Tutaendelea hadi majibu yote yapatikane. Tuendelee na mshikano huo huo, hakuna mtu mmoja peke yake anaweza kushinda vita hivi! Kwa Pamoja ushindi uko dhahiri.

mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia masuala muhimu kwa jamii. Hakuna atakayetueleza kuwa ufisadi huu mkubwa si jambo au tukio muhimu kwa maisha ya Watanzania. Serikali kama haitaki kuchokonolewa ilikuwa na wajibu wa kutoa "taarifa sahihi" kwa mujibu wa Katiba, na kwa kuwa haikutoa "tukitafuta" tusilaumiwe. Ni haki yetu. Isitoshe Ibara ya 20 inaenda mbele zaidi, 20(1) kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na ....kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo". Kama kwa kutoa mawazo yetu, na "kuwasema mafisadi..." anayedhani tumevunja Sheria ya nchi ajitokeze hadharani na aeleze ni sheria ipi ya Taifa hili tumevunja.
Akilimtindi,
Kama kwa kutoa mawazo yetu, na "kuwasema mafisadi..." anayedhani tumevunja Sheria ya nchi ajitokeze hadharani na aeleze ni sheria ipi ya Taifa hili tumevunja. Tatizo letu ni kukosa ushujaa na ujasiri katika kutetea haki, maslahi na rasilimali za Taifa letu, ambazo ninarudia tena, si za Rais, wala Serikali bali ni zetu, na Rais na Serikali tumewakabidhi kuzitunza tu kwa dhamana. Hivyo Akilimtindi, naungana nawe, lakini nadhani haki hiyo tusipewe na mtu, awe Rais, au nani bali tupewe na Katiba na sheria za nchi. anayesema kuwa tunachonganisha, tunachochoea naye awekwe kwenye mizani kupimwa anamtetea nani na kwa maslahi ya nani. Nikisema hivi, ni dhahiri ninapinga kabisa kuwasema tu watu, kuwaseng'enya, kuendekeza umbeya. Lakini tunapokuwa na tetesi, japo Dogo, Serikali inawajibika kutoa majibu sahihi kwa kuwa inavyombo vya uchunguzi, nyaraka zote ziko mikononi mwake. Isipotoa isitulaumu kuwa kuna uchochezi bali ijilaumu kwa kutotekeleza vizuri majukumu yake, tena ya Kikatiba. Wenye kujua haki zao, Katiba, na Sheria za nchi hawatatishwa hata kidogo, na Mhe. wa Awamu ya Tatu aling'anka na watu kufyata kwa vile tu vyombo vya Habari na Watanzania walivumilia wakiamini "usafi wake.." kumbe mambo tofauti. Tumeumwa na nyoka, hata jani tu latutisha sasa na hatutaachia kamwe. Tuungane, Tushikamane, Uhuru utarejea unakostahili, haki zitalindwa na Rasilimali zitalindwa. Kama tulipoibua tukaambiwa ni kelele za mlango na hazimzuii mwenye nyumba kulala, na leo yeye mwenyewe aliyetoa kauli hizo katamka hadharani, tena kupitia Bunge Tukufu kuwa ni kweli, na kuwa asilimia 75 zitarejeshwa na kuelekezwa kwa mkulima Tunataka nini zaidi, akiri au aombe msamaha vipi? Hii siyo kusema ninakubaliana na aliyosema, La hasha, amezua maswali mengi zaidi kuliko majibu. Tutaendelea hadi majibu yote yapatikane. Tuendelee na mshikano huo huo, hakuna mtu mmoja peke yake anaweza kushinda vita hivi! Kwa Pamoja ushindi uko dhahiri.
Ngomanzito,Dr Slaa
Hapo nakubaliana na wewe aslimia mia,uhuru wa kikatiba tunao lakini haya mambo ya kutishana eti wewe naitakuweka ndani haswa ndio noupigia kelele hapa na kuwaomba waandishi wa habari na vyama vya kijamii kumweleza Mh. kwamba sio hiyari yake kuwepo kwa uhuru huo