Uhuru wa habari unatumika vibaya - JK

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
Kwenye Hotuba ndeefuu ya Jk kadai tunatumia vibaya uhuru wa habari tulionao vibaya kuwachimbachimba watu. Lakini hapa amesahau kuwa hivi sasa ni karne ya 21 ya sayansi na teknologia pia hali ya sasa huwezi kufananisha na enzi ya cold war watu kufungwa midomo wasiseme kwa ujumla kashangaza sana watu.

Je Rais anataka viongozi wakitumia madaraka waliyonayo watu wakae kimya. kwa maoni yangu naona anataka kuleta mambo ya kizamani ya kuwatisha vyombo vya habari,wapinzani na jumuia mbalimbali wasichokonoe uozo wa serikali yake na kuusema haya mambo ya kutishana yalishapitwa na wakati na namwomba abatilishe usemi wake watu tupo huru kuongea chochote asitutishe kuwasema rafiki zake lazima tuweseme wametuibia fedha zetu.
 
Hii inamaanisha hata sisi hapa JF tunatumia uhuru huo vibaya kweli wanabodi ka sio kututaka tusiseme mabaya na mazuri ya nchi yetu
 
Nimekupata sawia ngoma nzinto, hili aliliruhusu mwenyewe na bahati nzuri limeikaba serikali yake mwenyewe. Hakujua kwanini Mkapa alikuwa mkali kipindi cha serikali yake? Sasa yeye amekuwa mpole utadhani yeye ndio msafi, kumbe naye fisadi. Sasa uhuru huu uliopo haufai kutunyima tena maana tumeshapata akili kutokana na uhuru huu huu, la msingi yeye na wenzake wajisafishe hapo uhuru huu huu utatumika kuwasifia na kuwapongeza kwa kujitoa muhanga kwa ajili ya watanzania.
 
Kwa masikio yangu alituhumu wazushi wachonganishi lakini si suala ambalo ni la ukweli.unaelewa watanzania wengi wavivu kufanya uchunguzi.hupenda kuzusha na kusubiri alyezushiwa ajibu ndipo aanze kuhoji.huu si uandishi.Naamini uandshi mzuri ni kufanya uchunguzi ndipo aundike habari za mtu.uandishi wa namna hii ndio wenye maana na hata mtu ukisoma unapenda mwandishi aendelee kuandika.Tatizo la uzushi lipo hata kwetu kwa baadhi ya wana JF.
 
Unamaanisha Kubenea alituhumu watu kwa habari asizokuwa nazo? mbona tumeona mengi ameanika yakiwa na vielelezo? mbona waliotuhumiwa basi hawakwenda mahakamani kama walivyodai wamumalize aache kutoa habari za uongo? Kwanini wanamwandama kwa kummwagia tindikali, prezidaa kuchimba mkwara na mengine kama kufunga tovuti yake?
 
Mimi nina uhakika waandishi wetu wengi wa habari hawafanyi utafiti wa kina kwenye habari zao nyingi ndio maana mwezetu hapa juu kaeleza kuwa inafikia mtu kuwa na hamu ya kuendelea kusoma habari yenyewe.
Pia habari nyingi haziandikwi kwa upana unakuta news iko very shalow sasa kama inamhusu mtu ndio kabisa data zinakuwa fuupi ndio maana wanaambiwa ni makanjanja.

Tuwape changamoto waandishi wetu wapiganie uhuru huu tulionao
 
Nimekupata sawia ngoma nzinto, hili aliliruhusu mwenyewe na bahati nzuri limeikaba serikali yake mwenyewe. Hakujua kwanini Mkapa alikuwa mkali kipindi cha serikali yake? Sasa yeye amekuwa mpole utadhani yeye ndio msafi, kumbe naye fisadi. Sasa uhuru huu uliopo haufai kutunyima tena maana tumeshapata akili kutokana na uhuru huu huu, la msingi yeye na wenzake wajisafishe hapo uhuru huu huu utatumika kuwasifia na kuwapongeza kwa kujitoa muhanga kwa ajili ya watanzania.
Akilimtindi,
Nadhani uhuru haukutolewa na "yeye mwenyewe" kama ulivyosema. Uhuru tunaotumia unatolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Toleo la 2005.Turejee Ibara ya 18 ya Katiba, na nina nukuu " kila mtu a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake,
b) anayo hki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka
ya nchi
c) Anayo uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika
mawasiliano yake,
d) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio
mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia masuala
muhimu kwa jamii.
Hakuna atakayetueleza kuwa ufisadi huu mkubwa si jambo au tukio muhimu kwa maisha ya Watanzania. Serikali kama haitaki kuchokonolewa ilikuwa na wajibu wa kutoa "taarifa sahihi" kwa mujibu wa Katiba, na kwa kuwa haikutoa "tukitafuta" tusilaumiwe. Ni haki yetu.
Isitoshe Ibara ya 20 inaenda mbele zaidi,
20(1) kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na ....kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo". Kama kwa kutoa mawazo yetu, na "kuwasema mafisadi..." anayedhani tumevunja Sheria ya nchi ajitokeze hadharani na aeleze ni sheria ipi ya Taifa hili tumevunja. Tatizo letu ni kukosa ushujaa na ujasiri katika kutetea haki, maslahi na rasilimali za Taifa letu, ambazo ninarudia tena, si za Rais, wala Serikali bali ni zetu, na Rais na Serikali tumewakabidhi kuzitunza tu kwa dhamana. Hivyo Akilimtindi, naungana nawe, lakini nadhani haki hiyo tusipewe na mtu, awe Rais, au nani bali tupewe na Katiba na sheria za nchi. anayesema kuwa tunachonganisha, tunachochoea naye awekwe kwenye mizani kupimwa anamtetea nani na kwa maslahi ya nani. Nikisema hivi, ni dhahiri ninapinga kabisa kuwasema tu watu, kuwaseng'enya, kuendekeza umbeya. Lakini tunapokuwa na tetesi, japo Dogo, Serikali inawajibika kutoa majibu sahihi kwa kuwa inavyombo vya uchunguzi, nyaraka zote ziko mikononi mwake. Isipotoa isitulaumu kuwa kuna uchochezi bali ijilaumu kwa kutotekeleza vizuri majukumu yake, tena ya Kikatiba. Wenye kujua haki zao, Katiba, na Sheria za nchi hawatatishwa hata kidogo, na Mhe. wa Awamu ya Tatu aling'anka na watu kufyata kwa vile tu vyombo vya Habari na Watanzania walivumilia wakiamini "usafi wake.." kumbe mambo tofauti. Tumeumwa na nyoka, hata jani tu latutisha sasa na hatutaachia kamwe. Tuungane, Tushikamane, Uhuru utarejea unakostahili, haki zitalindwa na Rasilimali zitalindwa. Kama tulipoibua tukaambiwa ni kelele za mlango na hazimzuii mwenye nyumba kulala, na leo yeye mwenyewe aliyetoa kauli hizo katamka hadharani, tena kupitia Bunge Tukufu kuwa ni kweli, na kuwa asilimia 75 zitarejeshwa na kuelekezwa kwa mkulima Tunataka nini zaidi, akiri au aombe msamaha vipi? Hii siyo kusema ninakubaliana na aliyosema, La hasha, amezua maswali mengi zaidi kuliko majibu. Tutaendelea hadi majibu yote yapatikane. Tuendelee na mshikano huo huo, hakuna mtu mmoja peke yake anaweza kushinda vita hivi! Kwa Pamoja ushindi uko dhahiri.
 
Mimi nina uhakika waandishi wetu wengi wa habari hawafanyi utafiti wa kina kwenye habari zao nyingi ndio maana mwezetu hapa juu kaeleza kuwa inafikia mtu kuwa na hamu ya kuendelea kusoma habari yenyewe.
Pia habari nyingi haziandikwi kwa upana unakuta news iko very shalow sasa kama inamhusu mtu ndio kabisa data zinakuwa fuupi ndio maana wanaambiwa ni makanjanja.

Tuwape changamoto waandishi wetu wapiganie uhuru huu tulionao

Hapo naweza kukuelewa mkuu, nadhani hawajafikia viwango kamili vya uhandishi bora lakini nina imani kwamba wana nia njema na nchi yetu kasoro tu wale waandishi vibaraka wa mafisadi. Tuwasaidie waweze kuelewa zaidi namna ya kutoa habari zilizojitosheleza, huenda pia hii ni jinsi ya kufanya wachape magazeti mengi zaidi kwa kuchapa habari nusu nusu kila gazeti. Ni biashara yao lakini naona kuna umuhimu wa kuendelea kuwashauri. Sawa mkuu.
 
Akilimtindi,
Nadhani uhuru haukutolewa na "yeye mwenyewe" kama ulivyosema. Uhuru tunaotumia unatolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Toleo la 2005.Turejee Ibara ya 18 ya Katiba, na nina nukuu " kila mtu a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake,
b) anayo hki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka
ya nchi
c) Anayo uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika
mawasiliano yake,
d) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio
mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia masuala
muhimu kwa jamii.
Hakuna atakayetueleza kuwa ufisadi huu mkubwa si jambo au tukio muhimu kwa maisha ya Watanzania. Serikali kama haitaki kuchokonolewa ilikuwa na wajibu wa kutoa "taarifa sahihi" kwa mujibu wa Katiba, na kwa kuwa haikutoa "tukitafuta" tusilaumiwe. Ni haki yetu.
Isitoshe Ibara ya 20 inaenda mbele zaidi,
20(1) kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na ....kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo". Kama kwa kutoa mawazo yetu, na "kuwasema mafisadi..." anayedhani tumevunja Sheria ya nchi ajitokeze hadharani na aeleze ni sheria ipi ya Taifa hili tumevunja. Tatizo letu ni kukosa ushujaa na ujasiri katika kutetea haki, maslahi na rasilimali za Taifa letu, ambazo ninarudia tena, si za Rais, wala Serikali bali ni zetu, na Rais na Serikali tumewakabidhi kuzitunza tu kwa dhamana. Hivyo Akilimtindi, naungana nawe, lakini nadhani haki hiyo tusipewe na mtu, awe Rais, au nani bali tupewe na Katiba na sheria za nchi. anayesema kuwa tunachonganisha, tunachochoea naye awekwe kwenye mizani kupimwa anamtetea nani na kwa maslahi ya nani. Nikisema hivi, ni dhahiri ninapinga kabisa kuwasema tu watu, kuwaseng'enya, kuendekeza umbeya. Lakini tunapokuwa na tetesi, japo Dogo, Serikali inawajibika kutoa majibu sahihi kwa kuwa inavyombo vya uchunguzi, nyaraka zote ziko mikononi mwake. Isipotoa isitulaumu kuwa kuna uchochezi bali ijilaumu kwa kutotekeleza vizuri majukumu yake, tena ya Kikatiba. Wenye kujua haki zao, Katiba, na Sheria za nchi hawatatishwa hata kidogo, na Mhe. wa Awamu ya Tatu aling'anka na watu kufyata kwa vile tu vyombo vya Habari na Watanzania walivumilia wakiamini "usafi wake.." kumbe mambo tofauti. Tumeumwa na nyoka, hata jani tu latutisha sasa na hatutaachia kamwe. Tuungane, Tushikamane, Uhuru utarejea unakostahili, haki zitalindwa na Rasilimali zitalindwa. Kama tulipoibua tukaambiwa ni kelele za mlango na hazimzuii mwenye nyumba kulala, na leo yeye mwenyewe aliyetoa kauli hizo katamka hadharani, tena kupitia Bunge Tukufu kuwa ni kweli, na kuwa asilimia 75 zitarejeshwa na kuelekezwa kwa mkulima Tunataka nini zaidi, akiri au aombe msamaha vipi? Hii siyo kusema ninakubaliana na aliyosema, La hasha, amezua maswali mengi zaidi kuliko majibu. Tutaendelea hadi majibu yote yapatikane. Tuendelee na mshikano huo huo, hakuna mtu mmoja peke yake anaweza kushinda vita hivi! Kwa Pamoja ushindi uko dhahiri.

Dr. slaa,

Hesima zako Mkuu, hakika hata wewe mkuu kumbe wamekupata? ni kweli una huhakika kuwa kuna kitu kimerudishwa? kweli iko kazi, mzee kale kamchezo ka sungura kaingia ndani ya sikio la tembo uliwahi kukasikia kakihadithiwa?

Mkuu nadhani ungenifurahisha kama tungeanza kujiandaa 2010, achana na hizi propaganda za hawa jamaa, Mkuu unajifanya umesahau wausika ni kina nani hapo?
 
Akilimtindi,
Nadhani uhuru haukutolewa na "yeye mwenyewe" kama ulivyosema. Uhuru tunaotumia unatolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Toleo la 2005.Turejee Ibara ya 18 ya Katiba, na nina nukuu " kila mtu a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake,
b) anayo hki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka
ya nchi
c) Anayo uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika
mawasiliano yake,
d) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio
mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia masuala muhimu kwa jamii. Hakuna atakayetueleza kuwa ufisadi huu mkubwa si jambo au tukio muhimu kwa maisha ya Watanzania. Serikali kama haitaki kuchokonolewa ilikuwa na wajibu wa kutoa "taarifa sahihi" kwa mujibu wa Katiba, na kwa kuwa haikutoa "tukitafuta" tusilaumiwe. Ni haki yetu. Isitoshe Ibara ya 20 inaenda mbele zaidi, 20(1) kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na ....kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo"
. Kama kwa kutoa mawazo yetu, na "kuwasema mafisadi..." anayedhani tumevunja Sheria ya nchi ajitokeze hadharani na aeleze ni sheria ipi ya Taifa hili tumevunja.

Nimekupata vizuri sana Dr., lakini mimi nilimaanisha kwamba Mkapa yeye alitukaba kutumia hiyo sheria Kikwete akalegeza uzi sasa imemzidi nguvu. Hata hivyo lenye nguvu zaidi ni hiyo (d) kuhusu uhuru wa kupata taarifa, inapigilia msumari suala la magazeti na internet kuwa na uhuru wa kuwapa habari wengine kuhusu nini kinafanyika wakati gani. Pia naona ni jambo la msingi kuelezea waziwazi hisia zetu kuhusu uchafu fulani unaoonekana mahala haswa pale serikali inapokuwa kimya na kushindwa kutoa maelezo kuhusu hisia hizo za wananchi. Mimi natilia mkazo nikisema tunahitaji sana kwa mawazo yangu kuwa na mikakati sahihi kwa uchaguzi ujao mapema tukiwa tayari walau tunajua mbinu azitumiazo huyu mpinzani wetu. Nina hakika pesa ndio itatumika zaidi 2010 kufanya lolote liwezekanalo ili CCM ishinde tena, tufanye kila tuwezalo kufunga illegal sources za hela kwa hawa jamaa. Kwa kufanya hivyo naamini watahaha sana na tutaona vilivyoko mifukoni mwao maana vitaanguka wakati wakihaha kurudi madarakani.
 
Akilimtindi,
Kama kwa kutoa mawazo yetu, na "kuwasema mafisadi..." anayedhani tumevunja Sheria ya nchi ajitokeze hadharani na aeleze ni sheria ipi ya Taifa hili tumevunja. Tatizo letu ni kukosa ushujaa na ujasiri katika kutetea haki, maslahi na rasilimali za Taifa letu, ambazo ninarudia tena, si za Rais, wala Serikali bali ni zetu, na Rais na Serikali tumewakabidhi kuzitunza tu kwa dhamana. Hivyo Akilimtindi, naungana nawe, lakini nadhani haki hiyo tusipewe na mtu, awe Rais, au nani bali tupewe na Katiba na sheria za nchi. anayesema kuwa tunachonganisha, tunachochoea naye awekwe kwenye mizani kupimwa anamtetea nani na kwa maslahi ya nani. Nikisema hivi, ni dhahiri ninapinga kabisa kuwasema tu watu, kuwaseng'enya, kuendekeza umbeya. Lakini tunapokuwa na tetesi, japo Dogo, Serikali inawajibika kutoa majibu sahihi kwa kuwa inavyombo vya uchunguzi, nyaraka zote ziko mikononi mwake. Isipotoa isitulaumu kuwa kuna uchochezi bali ijilaumu kwa kutotekeleza vizuri majukumu yake, tena ya Kikatiba. Wenye kujua haki zao, Katiba, na Sheria za nchi hawatatishwa hata kidogo, na Mhe. wa Awamu ya Tatu aling'anka na watu kufyata kwa vile tu vyombo vya Habari na Watanzania walivumilia wakiamini "usafi wake.." kumbe mambo tofauti. Tumeumwa na nyoka, hata jani tu latutisha sasa na hatutaachia kamwe. Tuungane, Tushikamane, Uhuru utarejea unakostahili, haki zitalindwa na Rasilimali zitalindwa. Kama tulipoibua tukaambiwa ni kelele za mlango na hazimzuii mwenye nyumba kulala, na leo yeye mwenyewe aliyetoa kauli hizo katamka hadharani, tena kupitia Bunge Tukufu kuwa ni kweli, na kuwa asilimia 75 zitarejeshwa na kuelekezwa kwa mkulima Tunataka nini zaidi, akiri au aombe msamaha vipi? Hii siyo kusema ninakubaliana na aliyosema, La hasha, amezua maswali mengi zaidi kuliko majibu. Tutaendelea hadi majibu yote yapatikane. Tuendelee na mshikano huo huo, hakuna mtu mmoja peke yake anaweza kushinda vita hivi! Kwa Pamoja ushindi uko dhahiri.

Dr Slaa
Hapo nakubaliana na wewe aslimia mia,uhuru wa kikatiba tunao lakini haya mambo ya kutishana eti wewe naitakuweka ndani haswa ndio noupigia kelele hapa na kuwaomba waandishi wa habari na vyama vya kijamii kumweleza Mh. kwamba sio hiyari yake kuwepo kwa uhuru huo
 
Ngomanzito,
Nashukuru. Napenda kuwapongeza sana vyombo vya Habari. Vyombo vya Habari ni vyombo muhimu. Hivyo, ni vyema i) Vyombo vyote vikatambua umuhimu wao kwa maslahi ya Taifa.Mara kadhaa imetamkwa kuwa 'Vyombo vya Habari ni mhimili wa Nne". Hili likukibalika, na wote tukaheshimu maadili ya hilo zile dosari za kusemwa vyombo vya Habari zitaondoka. ii) Vyombo vya Habari vikishajiweka Sawa, tutapiga kelele kama kuna mtu anataka kuvinyanyasa kwa maslahi yake binafsi, kwa kutaka tu kuvionea, kutaka kuficha uovu na au kuwabeba wachafu na waharibifu katika Jamii. iii) Wimbi la vyombo vya Habari kumilikiwa na Watu wanaotuhumiwa ni lazima likemewe kwa sababu hutegemei chombo cha Habari linalomilikiwa na mtu anayetuhumiwa kuwa sehemu ya Mhimili wa Nnne. Kwa upande mmoja tuna kazi ya kuviweka vizuri vyombo vya Habari, lakini kwa upande mwingine tunatakiwa kupiga kelele. iv) Wabunge, ni Sauti ya Wapiga kura na siyo Sauti ya Serikali kwa mujibu wa Katiba ndiyo maana vina jukumu la kuisimamia Serikali. Ushabiki unaozidi kiwango ni lazima ukemewe na wote wenye kuipenda nchi, kwani Bunge likigeuka kuwa la Mashabiki, litapoteza siyo tu mwelekeo lakini atakosekana katika nchi mtetezi wa Wananchi na vyombo vyao, vikiwemo vyombo vya Habari. Nashukuru hatua tuliyopiga sana sasa hivi, ambao wamejitokeza Wabunge makini, jasiri, ambao wanatetea ukweli badala ushabiki wa vyama. Truth is one and is indivisible, hivyo hakuna cha mtazamo wa fulani katika ukweli isipokuwa kwa Taifa lisilo na 'objective" values. Objective values daima ziko juu ya matakwa ya mtu mmoja mmoja na au chombo kimoja kimoja kiwe cha siasa, kiwe cha Habari.
 
Akilimtindi,
Nadhani uhuru haukutolewa na "yeye mwenyewe" kama ulivyosema. Uhuru tunaotumia unatolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Toleo la 2005.Turejee Ibara ya 18 ya Katiba, na nina nukuu " kila mtu a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake,
b) anayo hki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka
ya nchi
c) Anayo uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika
mawasiliano yake,
d) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio
mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia masuala
muhimu kwa jamii.
Hakuna atakayetueleza kuwa ufisadi huu mkubwa si jambo au tukio muhimu kwa maisha ya Watanzania. Serikali kama haitaki kuchokonolewa ilikuwa na wajibu wa kutoa "taarifa sahihi" kwa mujibu wa Katiba, na kwa kuwa haikutoa "tukitafuta" tusilaumiwe. Ni haki yetu.
Isitoshe Ibara ya 20 inaenda mbele zaidi,
20(1) kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na ....kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo". Kama kwa kutoa mawazo yetu, na "kuwasema mafisadi..." anayedhani tumevunja Sheria ya nchi ajitokeze hadharani na aeleze ni sheria ipi ya Taifa hili tumevunja. Tatizo letu ni kukosa ushujaa na ujasiri katika kutetea haki, maslahi na rasilimali za Taifa letu, ambazo ninarudia tena, si za Rais, wala Serikali bali ni zetu, na Rais na Serikali tumewakabidhi kuzitunza tu kwa dhamana. Hivyo Akilimtindi, naungana nawe, lakini nadhani haki hiyo tusipewe na mtu, awe Rais, au nani bali tupewe na Katiba na sheria za nchi. anayesema kuwa tunachonganisha, tunachochoea naye awekwe kwenye mizani kupimwa anamtetea nani na kwa maslahi ya nani. Nikisema hivi, ni dhahiri ninapinga kabisa kuwasema tu watu, kuwaseng'enya, kuendekeza umbeya. Lakini tunapokuwa na tetesi, japo Dogo, Serikali inawajibika kutoa majibu sahihi kwa kuwa inavyombo vya uchunguzi, nyaraka zote ziko mikononi mwake. Isipotoa isitulaumu kuwa kuna uchochezi bali ijilaumu kwa kutotekeleza vizuri majukumu yake, tena ya Kikatiba. Wenye kujua haki zao, Katiba, na Sheria za nchi hawatatishwa hata kidogo, na Mhe. wa Awamu ya Tatu aling'anka na watu kufyata kwa vile tu vyombo vya Habari na Watanzania walivumilia wakiamini "usafi wake.." kumbe mambo tofauti. Tumeumwa na nyoka, hata jani tu latutisha sasa na hatutaachia kamwe. Tuungane, Tushikamane, Uhuru utarejea unakostahili, haki zitalindwa na Rasilimali zitalindwa. Kama tulipoibua tukaambiwa ni kelele za mlango na hazimzuii mwenye nyumba kulala, na leo yeye mwenyewe aliyetoa kauli hizo katamka hadharani, tena kupitia Bunge Tukufu kuwa ni kweli, na kuwa asilimia 75 zitarejeshwa na kuelekezwa kwa mkulima Tunataka nini zaidi, akiri au aombe msamaha vipi? Hii siyo kusema ninakubaliana na aliyosema, La hasha, amezua maswali mengi zaidi kuliko majibu. Tutaendelea hadi majibu yote yapatikane. Tuendelee na mshikano huo huo, hakuna mtu mmoja peke yake anaweza kushinda vita hivi! Kwa Pamoja ushindi uko dhahiri.

Dr. Slaa.

Mheshimiwa hata mimi nakubaliana na wewe kuwa uhuru hautoki kwa mtu bali inabidi uwe kwenye katiba kama ilivyo na iwe kwa uwazi zaidi.

Pia nawapongeza wote wanao endeleza mapambana bila kujali vigingi wanavyokutana navyo mpaka ushindi upatikane.

Huyu bwana mkubwa wetu yeye mambo yamemuelemea thats why hataki watu waulize anataka watu wachulie mambo kiraisi na kucheka tu wakati wananchi wa kawaida wanakufa maana maisha kwakweli yamekuwa magumu sana kwa sasa na especially kwenye awamu hii isiyo na vision.

Tuendeleze mapambano mpaka kieleweka kwa kupeleka elimu ya uraia vijijini hata kwa kufanya fund raising kwa ajili ya mambo hayo. Kama tunachangia harusi sidhani tushindwe kuchangia elimu ambayo inatuhusu wote na vizazi vijavyo kujitambua.

Aksanteni
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom