Uhuru "Uliobinafsishwa" ndio tunaojiandaa kuusherehekea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhuru "Uliobinafsishwa" ndio tunaojiandaa kuusherehekea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 29, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu Mwanakijiji hata uhuru wa mawazo umebinafsishwa! Na huko bungeni mbunge akiongea tofauti na 'maelekezo ya ubinafsishaji' huo basi anaambiwa kakiuka kanuni na kutolewa nje. Wengine wanasema 'unatoka kauli za uchochezi'

  Kwa maneno mengine watanzania wengi hawana uwezo (according to wabinafsisha) hata kufikiri let alone kuhoji! oh... nimesahu kauli mbiu ya 50 yrs of independence: "Tumethubutu, tumeweza, tunasonga mbele".

  Incredible!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Gotdayuuum!! That lady at the beginning gave me goose bumps. Very articulate and very passionate. That's what's upper. Who is she, by the way? Anybody know?

  Nije kwenye hii miaka 50 ya uhuru. Unajua mimi hakuna kitu kinachonichefua kama mavumbi ambayo hugeuka kuwa tope pindi mvua zinyeshapo. Kuna siku moja bana mi nimetoka zangu Samaki Samaki, pale Mlimani city. Siku hiyo sikuwa na usafiri wangu mwenyewe kwa hiyo nikaomba lifti ya rafiki mmoja.

  Naye bila ya choyo akanipa lifti hadi karibu na kwetu. Nikashuka nikaanza kuelekea nyumbani. Sasa usiku huo umeme ulikuwa umekatika. Si mnajua mambo ya mgao tena. Na mvua ilikuwa imenyesha jana au sijui juzi yake ile. Sikumbuki vizuri lakini njiani madimbwi yalikuwa bado na maji kibao yaliyotuama.

  Sasa mtu mzima nimetinga Nike AIRMAX 2011 zangu nyeupe pyee (halafu za bei mbaya sasa). Njiani kwa sababu ya giza sikuweza kuona vizuri nilipokuwa nakanyaga. Si nikajistukia mguu mmoja unazama kwenye dimbwi....daaaah. Aisee nilimaindi....yaani AIRMAX zangu hizi bado mpya, yaani ndo zimetoka tu halafu zinachafuka na mitope? Haikubaliki hii. Hapana kabisa.

  Njia nzima kurudi nyumbani nilimtukana kila kiongozi wa CCM niliyeweza kumkumbuka jina. Niliilaani sana hii mijitu. Yaani miaka yote hii 50 hata barabara nzuri tumeshindwa kujenga. Hivi kwani kujenga barabara nzuri zisizo na mavumbi wala matope zinyeshapo mvua zina ugumu gani kutengeneza?

  Haya majitu yameniharibia NIKE AIRMAX 2011 zangu. Nimemaindi hivyo mjue.....
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Jibu utaambiwa hakuna hela, lakini I have seen streets zenye barabara za matofali au concrete!!!! Hivi hataa hii inatushinda?
   
 5. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Ni ukweli usiopingika kwamba watanzania hatujawahi kuwa huru katika nchi yetu miaka yote ya uhuru. Uhuru kamili ni pale tunapoweza kumtoa raisi madarakani kwa njia ya kura. Sasa wapi tuliwahi kuwa huru na kuja bibafishisha uhuru. Lazima ikumbukwe kuwa Tanzania katika miaka 30 baada ya uhuru ilitilia maanai sana kujenga Taifa lenye nguvu za kisiasa kuliko yote africa. Matawi ya chama mpaka vijijini! Matawi ya chama mahala pa kazi!! Huwezi kwenda chuo chochote mpaka uwe na kadi ya chama! Mimi kinachoniuma sana ni kule kupuuza kujenga maktaba za taifa ngazi za wilaya! Wabunge wapo lakini hawajui umuhimu wa maktaba. Si dhani hata wenyewe kama wana utamaduni wa kuweka book shelves sebuleni. Sasa hivi ilitupasa kuweka maktaba ngazi za vijiji.
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Machungu haya aidha tuyamalizie kwenye maandamano au kwenye box la kura 2015 na tuzilinde kura zetu na zitangazwe ndani ya muda!! Pia kuachana na sherehe hizo za uhuru bandia au wa kifamilia na ushikaji!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  The lady can serve better as a speaker of the national assembly, anaongea kama mtanzania halisi mwenye uchungu wa nchi sio kama wauza sura wengine.

  Mtangazaji wa kiume Deo Rweyunga ni bure kabisa anauchungu sana na serikali kuambiwa ukweli kuhusu yanayosemwa kuliko ukweli kuwa uhuru wa nchi umebinafsishwa.

  Rweyunga anawasihi watu waache Jazba, he is not informed at all, ukweli ni kuwai jazba inakuja shauri ya njaa na matatizo, mtu asiye na shida hana jazba kabisa. Jazba inaisha pale matatizo yanapokwisha
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Rweyunga ni kibaraka tu, kwani JK alipopata tu Urais si aliambatana naye USA!
   
 9. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,691
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  DAR ES SALAAM, Tanzania, March 11- Tanzania and the International Monetary Fund failed to reach agreement on a standby credit from the I.M.F. to help Tanzania pay its debts, Edwin Mtei, a director of the fund, said today-New York Times,March 12,1985.
   
 10. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jamani naomba mnisaidie huyo dada aliyeongea mwanzo ni nani angalau nimtumie text msg ya kumpongeza maana kaongea kwa uchungu hadi unaona kabisa maneno yanatoka moyoni.
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Huyo daad ni mpambanaji halisi, mara zote akiongea anaongea ukweli halisi. Mimi nadhani watuwa kuanza nao ni hawa wabunge maamuma wa CCM hawa ndio wanaotuangusha kwa kiasi kikubwa sana. wanalala tu bungeni, wanapitisha hoja zisizo na tija kwa taifa hili! ukisema ukweli wewe ni mchochezi yaani mpaka inatia kinyaa. Katiba mpya nayo itamaliza huu upuuzi kama aliokuwa anausema jana LUKUVI, eti uchochezi, over my a...., mxiiiii kwa vile anakula na kuiba kodi zetu basi wasisemwe!!! Big Up sana DADA yetu
   
 12. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Leo Je tatizo sio Ngeleja tena?
   
 13. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ingawa Mwenyekiti na na zome zomea toka upande wa CCM walijitahidi kumvuruga lakini alitoa message clear kwenda kwao, mie niliipenda zaidi kwani kila alipokatishwa na kuruhusiwa kuendelea daima hakuonyesha kutetereka....anaitwa Mheshimiwa Chiku Abwao (Mbunge wa viti maalum CDM)

  Ila naye Mheshimiwa Lusinde (Kibajaji) naona akapimwe akili kwani aliomba mwongozo eti wabunge wawe wanapimwa akili kwanza kabla ya kuanza bunge kwani maneno ya huyo mama yalimwingia baarabaaraa
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Jul 29, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Tatizo miaka yote imekuwa ni Ngeleja. Jamaa ni mtu mbaya sana. Anasababishaga mvua ziache kunyesha halafu anaenda kufyonza maji kwenye hayo mabwawa ya kuzalisha umeme ili wengine tupate shida. Karaha zetu kwake raha. Wajanja wa mjini siku hizi wanasema raha jipe mwenyewe bana. Naye kweli anajipa raha.

  Halafu kaanza huu mchezo wake mchafu tokea wakati wa Mwinyi. Sijui atakoma lini huyu mtu. Mbaya sana huyu. Niunge mkono katika kumlaani.
   
 15. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,717
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  hapa umeniacha hoi kwa kicheko, kwa hiyo jamaa anatapisha mabwawa kama vile vyoo vya uswahilini loh!!!!!!!!,
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Huyu ni MZEE MWANAKIJIJI ukisema MWANAKIJIJI unamaanisha MAGGID
   
Loading...