Uhuni huu Manispaa ya Ilala hadi lini?

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Ufisadi mkubwa unafanywa na manispaa ya Ilala katika ujenzi wa barabara ya kutoka Pugu kwenda majohe. Barabara hii ilianza kujengwa tangu mwaka 2012 na haijawahi kumalizika.

Daima barabara hii hujengwa nusunusu na kwa pole pole sana, kiasi cha kwamba mvua inapokuja huharibu kabisa na kuifanya isipitike. Baada ya mvua kuharibu ujenzi huanza upya na kwa gharama kubwa zikiwemo za kusoma na kujaza vifusi kwenye barabara ili kuifanya ipitike.

Kinachoshangaza zoezi hilo la kuleta kifusi hufanywa kwa siku kadhaa, halafu ule ujenzi wa pole pole unaendelea tena, kusubiri mvua nyingine ije ili barabara iharibike watu wapate dili.

Jana mvua za rasharasha tu zimenyesha magari yamekwama. Yaani hii nchi sijui ina laana. Maana kwa ujenzi wa hovyo hovyo wa barabara kama huu unaofanywa na manispaa ya Ilala huko Majohe, ni hasara kubwa kwa serikali. Maana wanajenga barabara mwaka mzima haiishi, halafu ikija mvua inaharibu wanaanza upya, na mwakani hivyo hivyo.

Yaani nchi ni kama haina kiongozi, meya wa huko anafanya kazi ya kuuza tu sura kwenye vyombo vya habari huku mbunge wao akiwa ICU anapumulia mashine. Hana habari na matatizo ya wanaukonga. Kwanza hutamuona hata bungeni akiuliza wala kuchangia hoja. Yeye anapokea mshahara tu, anasubiri ubunge wa fadhila kutoka kwa CCM umuangukie tena na Mwakani.

Sijui na meya naye anapata cha juu? Maana sielewi anawezaje kuuvumilia wizi mrahisi kama huu.

Huyu mkandarasi ameajiriwa na manispaa au anajitolea? Nashangaa sana kwamba hii nchi ina viongozi wanaoweza kuona ushenzi kama unaofanywa huko majohe, na wakauvumila tu, wala hawasikii kuumia moyoni kwamba ni kodi za walalahoi zinateketea kwa njia ya kihuni.

Mvua ndiyo hii inakuja, ole wenu ile barabara isipitike, nafikiri mtajua chungu na tamu ya wanamajohe. Maana wamewapania ile mbaya.
 
Hii barabara haifai na hata kinachotengenezwa hakionekani.

Kuna nyumba nzuri pembeni mwa hii barabara lakini zimekuwa mavumbi tu wenye nyumbani ni wakuwahurumia.

Manisapaa wawekeeni japo rami yavkuondoa hilo vumbi linaloharibu nyumba za watu.
 
Tunaposema ccm ni janga tunaimanisha ukishaona mpaka wanyama wanawakata jua ccm ni boom linalosubiri kulipuka
 
Hii barabara haifai na hata kinachotengenezwa hakionekani.

Kuna nyumba nzuri pembeni mwa hii barabara lakini zimekuwa mavumbi tu wenye nyumbani ni wakuwahurumia.

Manisapaa wawekeeni japo rami yavkuondoa hilo vumbi linaloharibu nyumba za watu.
My friend hii barabara iliadiwa kujengwa kwa kiwango cha lami tangu huo mwaka 2012. Wakati barabara ya Mombasa mazizini ikijengwa, na hii ya Majohe ilikuwa kwenye program hiyo. Lakini watawekaje lami ilihali wanakuja wanagusagusa udongo kwa miezi kama mitano au sita hivi kusubiria mvua ije, halafu ikishakuja na kuvuruga kabisa barabara wanaanza upya? Ina maana hela iliyokuwa itoshe kuwekea lami inaishia kurekebishia upya barabara badala ya kuendelea mbele. Kama yule mkandarasi wa kutengeneza ile barabara hajitolei, basi kwa hakika mkurugenzi wa manispaa hii anapiga dili kubwa sana. Na nitashangaa kama katika mabadiliko ya wakurugenzi, Pinda hatamfuta kazi huyu mkurugenzi mhuni.
 
Back
Top Bottom