Uhasama wa Saudia na Qatar

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
Uhasama wa Saudia na Qatar
wazidi kuongezeka Baada ya kufichuka njama za
Qatar za kuupindua utawala
wa kifalme Saudi Arabia,
uhasama baina ya nchi hizo
mbili umechukua mkondo
mpya mara hii kuhusu umiliki wa Uwahhabi.
Mrithi wa kiti cha ufalme Saudi
Arabia Nayef bin Abdul Aziz
amenukuliwa na tovuti ya Al
Awamiya akisema kuwa nchi
yake haitoirushusu Qatar kuchukua nafasi ya Saudia
kama kitovu cha Uwahhabi.
Matamshi hayo yanakuja
baada ya serikali ya Qatar
kutangaza kuwa msikiti
mkubwa zaidi nchini humo utajulikana kama Msikiti wa
Muhammad ibn Abdul
Wahhab, mwanzilishi wa
kundi la Wahhabi.
Weledi wa mambo wanasema
hatua hiyo ya Doha ina lengo la kuipokonya Saudi Arabia
nafasi yake kama kitovu cha
Uwahhabi katika ulimwengu
wa Kiarabu. Aidha weledi wa
mambo wanasema Marekani
inaichochea Qatar kuendeleza vita vyake vya maneno dhidi
ya Saudi Arabia. Wiki iliyopita
kulivuja mazungumzo ya siri
ambapo Waziri Mkuu wa Qatar
Hamad bin Jassem Al Thani
alinukuliwa akisema ufalme wa Saudi Arabia utapinduliwa
na Qatar hivi karibuni. Mkanda
huo wa sauti pia ulimnukulu
Jassem Al Thani akisema kuwa
wanajeshi wa nchi hiyo hiyo
wataukalia kwa mabavu mji wa Qatif wa mkoa wa
Mashariki mwa Saudi Arabia.

Source:radio iran swahili
 
Source:radio iran swahili
duuu nilikuwa sijui hapo bold; mkuu hii post mahala pake ni international forum
qatar labda wapate msaada kutoka west, kuimaliza qatar ni rahisi sana kupitia foreigners wanaoishi qatar wewe uliona wapi mpaka security officers wa airport ni raia wakigeni, ukiwa pale airport wafanyakazi 80% ni raia wakigeni, wahudumu ndani ya ndege + pilots wote wageni sasa hapo unaulinzi kweli?
 
Back
Top Bottom