barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Wanachama na mashabiki wa Yanga leo wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na kampuni ya IPP MEDIA ambayo ipo chini ya Reginald Mengi.
Wanachama na mashabiki wamefikia hatua hiyo baada ya kukasirishwa na kitendo cha Reginald Mengi kutumia vyombo vyake vya habari kuandika habari za uongo na uchochezi kuhusu Yusuph Manji ili kuivuruga Yanga. Madai ya mashabiki hao wa Yanga ni kuwa Mengi ambaye pia ni mwanachama wa Yanga anaonyesha kutofurahishwa kwake na uwepo wa Manji katika klabu ya Yanga.
Mashabiki hao wanasema wanachoma magazeti hayo kama ishara ya kutokubaliana na "hujuma" za Mengi dhidi ya Manji Mwenyekiti wa Yanga ambaye wanasema ameifikisha team katika hatua ya mafanikio ya 16 bora ya kombe la CAF kitu ambacho hakijawahi kufikiwa kwa miaka zaidi ya 15
Mashabiki hao pia wamemuonya Mchambuzi wa Michezo wa Clouds Media,Shafih Dauda kutumia ukurasa wake wa Fb na Blog yake kudhoofisha Yanga na uongozi wake kwa kuandika habari za uchochezi na ufitini.
Hii ndio Yanga,Wao wanaiita ya Kimataifa