Ni mtazamo tu...
Hapo ndio ninapompendea kiumbe wa kike....
Anapokuwa bado kigori 16-19 utamsikia mimi bwana
mume wangu lazima awe mrefu,handsome mwenye pesa
na kila aina ya sifa(akibahatika kumpata alhamdullilah)
Akivuka hapo kuanzia25-30 utamsikia aah mume
ninayemtaka asiwe mrefu sana,sura haijalishi kwa sana
ila tu aweze kunipenda na kunijali(akitokea alhamdullilah
Kuanzia 30-35 kiumbe huyohuyo utamsikia ninayemtaka
sitajali sura mradi tu awe na shughuli yake inayomwingizia kipato
Kutoka 35 na kuendelea kama hakubahatika kupata, kiumbe
huyohuyo utamsikia akisema aah mimi yeyote atakayejitokeza
niko tayari kuolewa naye,sasa jamani tuwaeleweje hawa binadamu..??
NAWAZA TU HAPA KWENYE PC YANGU.....