Uhamiaji wahusishwa na dawa za kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhamiaji wahusishwa na dawa za kulevya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Jul 29, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,901
  Trophy Points: 280
  NZANIA


  Add Comment

  Uhamiaji wahusishwa na dawa za kulevya 29/07/2011

  0 Comments


  Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania, imeingia kwenye kashifa ya kuhusishwa na kushamiri kwa dawa za kulevya baada ya mtuhumiwa wa Rashid Mtopea (30), kukamatwa na hati nne za kusafiria.

  Hati hizo zilitolewa na Idara ya Uhamiaji kwa nyakati tofauti, zote zikiwa zinatumiwa na mtuhumiwa huyo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

  Mtopea, mkazi wa Magomeni Mikumi, Dar es Salaam, alikamatwa juzi na Polisi wa Kikosi cha Dawa za Kulevya katika kizuizi cha Kabuku wilayani Handeni, Tanga.

  Uchunguzi uliofanywa na
  gazeti UHURU umebaini kuwa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya nchini wamekuwa wakitumia hati za kusafiria zaidi ya moja kama mbinu ya kuwawezesha wasikamatwe. Uhuru imefanikiwa kupata namba za baadhi ya hati za kusafiria zilizokuwa zikitumiwa na Mtopea katika safari zake mbalimbali nje ya nchi, huku zikiwa na miaka tofauti ya kuzaliwa wakati zina picha ya aina moja. Hati ya kwanza ya kusafiria ya Mtopea ina namba AB 361969, iliyotolewa Desemba 8, 2009, mjini Dar es Salaam na inaonyesha kwamba alizaliwa Aprili 25, 1983. Hati nyingine ni yenye namba AB 438110, ikiwa na jina la Pritesh Bhati, ambayo ilitolewa Oktoba 28, 2010 mkoani Tanga, ikionyesha kuwa amezaliwa 1979.

  Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi nchini zimesema kuwa, idara hiyo imekuwa kikwazo katika kupambana na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya kutokana na kushiriki kuwapatia hati za kusafiria kinyume cha sheria. Zimesema kuwa tukio la kukamatwa kwa Mtopea kunatokana na juhudi binafsi zilizofanywa na askari wa kitengo hicho, ambao waliweka mtego na kufanikiwa kumnasa mtuhumiwa huyo.

  "Kama tungezubaa tu, tungewakosa, kwani wana mbinu kubwa ambazo sasa zimeshajulikana, hasa hii ya kuwa na hati mbili za kusafiria... "Hawa jamaa wa Uhamiaji wabadilike, ni jambo la kushangaza kuona mtu mmoja anapewa hati mbili kwenye nchi mmoja... ifikie wakati waache tamaa na waweke uzalendo mbele," kilisema chanzo hicho.

  Chanzo hicho kilisema kuwa mtuhumiwa huyo ana hati zaidi ya moja za kusafiria zilizotolewa na idara hiyo mjini Dar es Salaam na Tanga kwa muda na miaka tofauti.

  Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa, alikiri mfanyabiashara huyo kuwa na hati zaidi ya moja za kusafiria, "Huyu ni mtu mkubwa, tajiri na wapo wengi wa namna hii, hivyo kuwakamata kunahitaji ushirikiano mkubwa kutoka mamlaka husika,'' alisema.

  Nzowa alisema ushirikiano mzuri ukiwepo utasaidia kupunguza biashara hii au kuitokomeza kabisa nchini.

  Kabla ya kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo, alionekana kituo cha mabasi mjini Tanga akimkabidhi begi kubwa, Idd Mwaduga (34), mkazi wa Pongwe, ambaye aliingia katika basi la Kampuni ya Raha Leo.

  Baada ya Mtopea kumkabidhi begi hilo, aliingia katika gari ndogo akiwa na mwanamke Ronin Hussein (25) na kuanza safari ya kuja Dar es Salaam, akiwa amelitangulia basi la Raha Leo na alipofika katika kizuizi hicho alikamatwa na baadaye basi hilo nalo lilikamatwa.

  - via
  UHURU
   
Loading...