Uhamiaji waelezea sababu za kutimua watumishi

Uhamiaji waelezea sababu za kutimua watumishi

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Hatua hiyo imetokana na idara hiyo hivi karibuni kupokea malalamiko mengi kupitia kampuni na taasisi mbalimbali kuwa kuna watu wanapita kwenye ofisi wakijitambulisha kuwa maofisa kutoka uhamiaji.

MSEMAJI UHAMIAJI 2.JPG


Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam kwa njia ya simu, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda, alisema kutokana na hali hiyo, wameamua kuwatangaza watu hao ambao baadhi walisimamishwa kwa makosa ya rushwa na utovu wa nidhamu.

Mtanda alisema idara ya Uhamiaji iliwasimamisha kazi watu hao mwaka 2016/17 na kwamba wengine waliacha kazi wenyewe.

Alisema wameamua kufanya hivyo ili chochote kitakachojitokeza dhidi yao, idara haitahusika.

“Tumeamua kuwatangaza kwa sababu hivi karibuni tumepokea malalamiko mengi kupitia kampuni na taasisi mbalimbali kuwa kuna watu wanapita kwenye ofisi hizo wakijitambulisha kuwa maofisa kutoka uhamiaji.

“Hawa tuliowatangaza leo (jana) kuwa sio wafanyakazi tena wa Idara ya Uhamiaji lengo ni ili jambo lolote likitokea huko nje dhidi yao itambulike si watumishi wetu tena,” alisema.

Mtanda alisema orodha hiyo ambayo imeambatanishwa na picha za watu hao ni kwa lengo la umma kuwatambua kuwa si wafanyakazi wa idara hiyo tena.

Katika tangazo lililotolewa juzi na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, idara hiyo haitahusika au kutambua huduma yoyote itakayotolewa na watajwa kwenye picha.

Watu hao ni Thobias Lyewe, Julieth Mrema, Nina Muga, Loveness Wilson, Wilbard Ompapson, Salama Dilunga, Philbert Chaula, Mkombozi Chodri na Alfred Mrema.

Wengine ni Imaculata Mwakatika, Ramadhani Ally, Ritha Maganga, Jovin Mkuchu, Veronika Max, Angela Mwambwiga, Peter Bally, Elizabeth Kibinga na Lucy Munyanga.

Chanzo: Niapashe
 
Kwa hiyo kosa ni kujitangaza wao Uhamiaji au??Maana ndio point kubwa kulingana na huyo msemaji
 
Kama walikuwa hawajafukuzwa kazi rasmi basi walikuwa bado ni wafanyakazi halali wa Uhamiaji na walikuwa na haki zote za kujitambulisha hivyo!. Unless kama walikuwa wanafanya utapeli

Labda uhamiaji kama walivyoutangazia umma kuhusu kuwafukuza hao watu si vibaya pia kwa mtindo huohuo wakauelezea umma.
1. Je watu hao kujitangaza kuwa ni watumishi wa idara ya uhamiaji walivunja sheria gani za nchi?

2. Je ni makosa gani ya utumishi waliyotenda, yenye ushahidi, na due process gani imefuatwa ili kuwatimua?

Hili jambo ni muhimu kwa sababu linahusu haki za raia wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wanaolindwa na sheria za utumishi wa umma
 
Kwa hiyo kosa ni kujitangaza wao Uhamiaji au??Maana ndio point kubwa kulingana na huyo msemaji
Tatizo hapo ni wao wanaopita huko anakosema? Je, walifukuzwa kwa makosa yanayofanana na malalamiko hayo? Je kuna wafanyakazi wangapi wa uhamiaji ambao wameshaacha kazi au kugukuzwa? Hao hawawezi kisumbua hayo makampuni?

Mambo mengine ni ubashite tu.

Je, polisi fake na ambao wengine tumeona wamekamatwa, jeshi la polisi litoe picha za askari polosi walioacha kazi, waliofukuzwa au kustaafu kwasababu kuna watu wanajitambulisha kama polisi?

Ndio maana kukawa nashiria. Hapo huyu bwana amechemka big time.
 
Back
Top Bottom