Kuna jamaa yangu alienda ofisi za uhamiaji leo kutafuta pasi ya karatasi ili aende Uganda cha ajabu akaambiwa karatasi za pasi zimeisha Dar es Salaam yote akitaka aende Kibaha Mkoa wa Pwani. Akaamua kufunga safari hadi Kibaha kweli bwana akaambiwa zipo ila atoe elfu 20 apatiwe kitu... akalia hali akapata kwa shilingi 15 alipotoka nje akasikia wenzie waliotoka Dar wakilalamika kwani kila mtu alipigwa bei yake kuna waliolipa elfu 30, elfu 20 kwa ajili ya pasi hiyo ambayo bei yake halali na ya kwenye risiti ni sh elfu 10 tu. Najiuliza hii nchi sasa inaelekea wapi ? Watanzania tuunganishe nguvu zetu Oktoba kieleweke jamani tuachane na hekaya za maisha bora hewa kwa kila Mtanzania.