Uhamiaji kutoa vibali maalum kwa Warundi waje kulima Tanzania

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
makaka_0.jpg

Idara ya Uhamiaji nchini imeweka utaratibu wa kutoa kibali maalum kwa raia wa Burundi ambao wanataka kuja nchini kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo ikiwa ni moja ya nia za kupunguza raia wa nchi hiyo ambao huingia nchini kinyemela hususani katika mikoa ya Kigoma na Tabora kwa ajili ya kufanya kazi za kilimo kama vibarua.

Mpango huo umetangazwa na Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini Dk.Anna Makakala mwishoni mwa ziara yake iliyomfikisha katika wilaya zote na katika maeneo ya mpaka na nchi jirani mkoani Kigoma ambapo amesema vibali hivyo vya miezi mitatu vitawezesha raia hao kutambuliwa na serikali kupata fedha na kutambua wako wapi na idadi yao.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema uamuzi huo wa idara ya uhamiaji utasadia kupunguza uhalifu na kuongeza tija katika kilimo pamoja na kujenga mahusiano mazuri na nchi jirani ya burundi ambayo raia wake wanaongoza kwa kuja nchini kufanya vibarua bila ya kibali na hivyo kuongeza idadi ya wahamiaji haramu.

Chanzo: ITV
 
Very good move. Hii tabia ya kukamata hawa wananchi masikini wanaojitafutia riziki kwa jasho lao ifike mwisho. Most ya Hawa Watu kutoka Burundi wanakuja kutafuta maisha thru vibarua nk. Wakipewa vibali itapunguza rushwa na uonevu wa polisi wetu dhidi ya hawa wananchi masikini!

Africa is one!
 
My take:

Sikubaliani na uhamiaji kwa sababu wanaleta janga nchini.

Vita na vifo vya wafugaji na wakulima Tanzania vimepingua kutokana na maelewano ikiwemo uvumilivu na desturi. Sasa kuruhusu watu waje kulima, kutachochea rushwa na Ugomvi.

Nashauri watoa vibari kwa watu wanaotaka kuja kuwekeza kwenye Viwanda kwa sababu Serikali ya Magufuli ni Serikali ya Viwanda.
 
MKUU kama kuna maeneo Kwa nini wasiwapeleke wafugaji au wakulima watamaliza huo mgogo wa kupigana kila kukicha?

Halafu watangaze kwanza hayo maeneo Kwa watanzania kwanza kama kuna wanaohitaji watakwenda kuyatumia kabla ya kuwapa waburundi. Waangalie kwanza nyumbani kwao kabla ya kutoka nje.
 
Hapo wanataka kupewa Wanyarwanda. Ili sasa kuzuga wanaanza kuwatangazia kuwapa warundi. Wamejishtukia kila siku ni Rwanda.
 
Kwa hiyo vibali vitakuwa vinatolewa kipindi cha msimu wa mvua?!!
 
Hiki ni kichekesho cha karne...!!
Yaani raia wa nchi nyingine apewe kibali kuja kulima Tanzania kwani huko Burundi hakuna Ardhi..?
Je, wanakuja kama vibarua wa kwenye mashamba ya Watanzania au wanaanzisha mashamba yao? Je, hicho chakula au mazao wakivuna wanapeleka Burundi au yanabaki Tanzania? Je, wakiuza hiyo fedha wanapeleka kwao au wanatumia wakiwa Tanzania tu?

Hii siyo bure...!!Ukizama deep kwenye hii policy inaelekea kutaka kuhalalisha WARUNDI NA WANYARWANDA KUHAMIA TANZANIA.....Hii maneno tunasikia juujuu kuwa Mkulu wa nchi ana ka-asili ka kutokea pande za Banyamlenge, Intarahamwe na M-23 inawezekana kuna ukweli Fulani.!!! Tusibiri maana yajayo yanafurahisha.
 
Hureee ! Manamba wanarejea ! Yaani sisi kama wakoloni sasa, na tutawahesabu kwa konzi
 
Wahamie mara ngapi sasa, wakati milioni tano ya watanzania ni wao ifikapo 2030 watajitwalia nchi ya bure bye bye Tanzania.

Imhotep,
Unachosema ni correct by 100 pc. Inawezekana kabisa huu ni mkakati maalumu kwa ajili ya Uchaguzi wa 2020 ili nanino mwenzao apate kura na ushindi wa kishindo toka kwa jamaa zake.....!!!
 
Hiki ni kichekesho cha karne...!!
Yaani raia wa nchi nyingine apewe kibali kuja kulima Tanzania kwani huko Burundi hakuna Ardhi..?
Je, wanakuja kama vibarua wa kwenye mashamba ya Watanzania au wanaanzisha mashamba yao? Je, hicho chakula au mazao wakivuna wanapeleka Burundi au yanabaki Tanzania? Je, wakiuza hiyo fedha wanapeleka kwao au wanatumia wakiwa Tanzania tu?

Hii siyo bure...!!Ukizama deep kwenye hii policy inaelekea kutaka kuhalalisha WARUNDI NA WANYARWANDA KUHAMIA TANZANIA.....Hii maneno tunasikia juujuu kuwa Mkulu wa nchi ana ka-asili ka kutokea pande za Banyamlenge, Intarahamwe na M-23 inawezekana kuna ukweli Fulani.!!! Tusibiri maana yajayo yanafurahisha.
kwasababu ya mfalme
 
Hii kali miezi mitatu keshalima, keshavuna, kauza/kabeba maana kibali muda utakuwa umeshaisha. Wawe wa bunifu zaidi kwa chochote walicho dhamiria katika huu utaratibu mpya.
 
Very good move. Hii tabia ya kukamata hawa wananchi masikini wanaojitafutia riziki kwa jasho lao ifike mwisho. Most ya Hawa Watu kutoka Burundi wanakuja kutafuta maisha thru vibarua nk. Wakipewa vibali itapunguza rushwa na uonevu wa polisi wetu dhidi ya hawa wananchi masikini!

Africa is one!
Yale yale ya Nyerere kule maeneo ya manyovu. MAumivu ya kichwa huanza taratibu. Baadae utaja sikia, ....hawa wote nawapa vibali vya uraia wa watanzania...
 
Back
Top Bottom