Uhamiaji Kufuatilia Ajira za Utapeli Mtandaoni

Uhamiaji Kufuatilia Ajira za Utapeli Mtandaoni

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
976
Reaction score
1,952
Hivi karibuni Idara ya Uhamiaji ilitoa tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya Uhamiaji vijana wa Kitanzania kupitia tovuti na mitandao yake ya kijamii (Instagram, Twitter, Facebook).

Kufuatia tangazo hilo, kumekuwepo na Matapeli wanao walaghai Wananchi kupitia mitandao ya kijamii na baadhi yao kuwapigia simu au kuwatumia ujumbe kwa njia ya sms kwamba kuna nafasi za ajira na kuwataka kutuma fedha ili wawasaidie kupata nafasi hizo za ajira.

Idara inapenda kuufahamisha Umma kuwa mchakato huo wa ajira ulishakamilika na uliendeshwa na kusimamiwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za ajira kama ilivyoainishwa kwenye tangazo la ajira. Hivyo, Wananchi wanaombwa kupuuza na kutoa taarifa kwa vyombo vya
usalama pindi wanapopigiwa simu au kutumiwa ujumbe huo.

Taarifa rasmi za Idara kuhusu ajira na nyinginezo, hutolewa kupitia mifumo rasmi ya mawasiliano ikiwemo Vyombo vya Habari, tovuti ya Idara ambayo ni www.immigration.go.tz na mitandao yake ya kijamii (@UhamiajiTz).

Aidha, Idara ya Uhamiaji inaendelea na uchunguzi kwa lengo la kuwabaini wanaohusika na uhalifu huo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Imetolewa na;

SSI. Paul J. Mselle

MSEMAJI MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI
IMG_3776.jpeg
IMG_3777.jpeg
 
Sasa idara ya uhamiaji imejipachika majukumu ya Polisi, kupeleleza.
 
Back
Top Bottom