JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
Kikosi cha Uhamiaji Kiteto Mkoani Manyara, leo kitakutana na viongozi wa dini (Wakristo) kuwapa maelekezo ya namna ya kupokea wageni.
Kamanda wa Uhamiaji Kiteto Ikomba Eliud Mathew amezungumzia malengo ya kukutana nao kuwa ni kutoa maelekekezo wajue madhara na faida ya kupokea wageni.
"Natambua taasisi za kidini zimekuwa zikipokea wageni kwaajili ya kufanya shughuli za kidini, hili sio tatizo bali wanapaswa kufuata taratibu za kisheria"
Utaratibu wa wageni kuingia nchini uko wazi, hili lazima lifahamike kwa viongozi hao ili Serikali iweze kufahamu shughuli zinazofanywa na wageni, alisema Kamanda Ikomba
Katika hatua hiyo Kamanda Ikomba alisema Wilaya ya Kiteto ina Wahamiaji Walowezi zaidi ya 6000 ambao waliingia nchini miaka mingi iliyopita.
"Uhamiaji hatuna nia ya kuwafukuza watu hawa hapa nchini bali kuwabaini na kutoa mapendekezo ya kisheria kwa watunga Sera kuamua vinginevyo juu ya uwepo wao"
Alitaja madhara ya kupokea wahamiani haramu kuwa ni pamoja na kuwa na watu ambao wataingia katika mgao wa rasilimali za Taifa na kunufaika zaidi kuliko watanzania wenyewe.
Mara nyingi kundi hili wengi wao huwa wahalifu tena wakutumia silaha kali kama vile ujambazi na kusababisha madhara kwa wananchi.
Taarifa za uhakika zinaeleza utekaji uliofanyika Mara nyingi Kiteto wanaohusika na matukio hayo ni wageni kutoka nje.