Uhamiaji kidogo kuna nafuu sasa

Uhamiaji kidogo kuna nafuu sasa

Gharama ni 150k ikiwa una cheti chakuzaliwa cha chako na mzazi mmoja.
Kama huna cheti cha kuzaliwa wewe na mzazi mmoja andaa 20k@ sawa na 40k plus 150k=190k
Vipi kama wazazi wametangulia mbele ya haki?
 
Hii tabia ya kuomba barua ya mwaliko imepitwa na wakati mno yaani ni ajabu sana...kwani tatizo ni nini?
Shida kubwa ni viza na Nauli kama ninavyo shida iko wapi?hii kitu inajenga hisia za ajabu sana,mbona nikitaka kwenda Iringa,Bukoba ,Nairobi.Bujumbura....huulizwi unafuata nini
Imeshawekwa hisia kuwa maisha ya ndani ni magumu na nje kuna maisha mazuri hivyo huenda wanahisi mtu atatorokea huko...lkn wanashindwa kutambua kuna nchi nyingi zinataka ticket yako tu hakuna haja ya viza mfano Malaysia, MTU unaweza kwenda kama mtalii wa kawaida.

True yatakiwa hichi kipengele wabunge wakisemee kifutwe hizi sio zama za mwalimu kusafiri ilikuwa sawa na kwenda paradiso.Hichi kipengele ni kikwazo wajikite kukusanya mapato kwa kuifanya passport kupatikana kwa kila MTU.Uthibitisho wa safari wa nn sasa.Dunia imebadilika hayo mambo ya uthibitisho wa safari yabakie kwenye maombi ya viza mabalozini.Ni kipengele cha kizamani sana,vijana watoke nje wakalete pesa nchi zingine angalau fursa ukiweka aibu pembeni
 
Juzi nimepata passport yangu electronic sijatoa senti tano...
 
Sawa kiongozi.Wengine hawaoni.Juzi kati kuna mama mmoja toka kaskazini aliilaumu hii idara kuwa wnakataa kumpa mme wake mhindi/chef urai.Aje asome hapa mawazo ya wadau.
Imechukua wiki tatu hadi kupokea taarifa za kwenda kuchukua passport yangu. Ukiwa na taarifa zote naona usumbufu si mwingi sana. Ila kero yangu bado ni kwenye kuomba barua za safari. Kuna watu wanapanga kutumia passport Mwakani halafu nyie mnawaomba uthibitisho leo.


View attachment 1250522
 
Kila kitu online hata kwa smartphone yako au laptop yako unajaza form unaambatanisha vigezo vikitimia na kuthibitishwa ndani ya siku tu unapata
 
2018 nilichukua ile ya kijani na miezi miwili iliopita nimechukua ya blue. Niliwaambia nasafiri naenda Dubai(sihitaji uthibitisho naenda kutembea) na SA(sihitaji uthibitisho naenda kutembea na sihitaji hata Visa).
Dawa yao waambie unaenda kutalii,taja nchi isiohitaji mwaliko wala Visa

Asante kwa huu ushauri, mi nilikuwa na document zote ila ntashirikisha marafiki ili waweze kupata
 
Jamani mbona Mimi nilichemka kwenye barua ya uthibitisho wa safari au kinachonipeleka nje ni nini na uthibitisho wake, nikakwamia hapo, ilikua 2015.

Mambo yamebadilika sasa jaribu tena. Passport ya zamani niliipata baada ya kupata admission ya kwenda shule
 
Jamani mbona Mimi nilichemka kwenye barua ya uthibitisho wa safari au kinachonipeleka nje ni nini na uthibitisho wake, nikakwamia hapo, ilikua 2015.
Mimi niliandika barua kueleza juu ya safari ya kwenda china kibiashara, nikaambatanisha TIN certificate pamoja na nyaraka zote zilizo hitajika.

Sikutoa hata senti moja sema changamoto niliyo kutana nayo ni birth certificate. Nilipo zaliwa nilipewa jina lingine ambalo lipo kwenye birth certificate na nilipo batiwa wazazi walinibadirisha jina. Kwaiyo kulikua na utofauti wa jina, nikaenda kwa mwanasheria akaniandikia DEED POLL nikaambatanisha na copy ya kile cheti chenye kasoro.

Ndani ya siku sita nikawa nimepata na kwamara ya kwanza kimegongwa sirari mpakani mwa tanzania na kenya last month.

Wengi wanakwama kwenye chiti cha kuzaliwa kwamaana jamaa wanasema walio zaliwa below 1980 ndio wanapokea half davit na walio zaliwa above 1980 lazima uwe na cheti cha kuzaliwa hawakubali half davit.
 
Hivi kwa wale tuliokuwa nazo tunataka kubadili tupate mpya tunaanza maombi upya kabisa kama hukuwahi miliki passport au kuna ka unafuu fulani
 
Back
Top Bottom