.
Mkuu, Jaji haandai nyaraka, kazi ya jaji ni kuandaa hukumu. Nyaraka yeyote ya mahakama utakayoiona imeandaliwa na maofisa wa mahakama na sio jaji, kama nyaraka inahitaji saini ya jaji basi nyaraka huandaliwa na jaji hupelekewa kwa ajili ya kuweka sahihi.
Nyaraka nyingi tu za mahakama huwa zina makosa. Majaji wengine hawajui kuandaa baadhi ya nyaraka (mfano decree) (samahani kwa waheshimiwa majaji kwa hili, inabidi niseme ukweli tu), na wanaofahamu kuziaandaa wengi wamepitia uwakili au ukarani. Nyaraka hizi, japo zinahitaji ujuzi wa sheria kuziandaa vizuri, zinaweza kuandaliwa na mtu asiye na ujuzi wa sheria ili mradi awe na uzoefu wa kuziandaa tu.
Majaji wa mahakama ya tanzania ni wajuzi wa sheria, na wanafanya kazi yao ya kusikiliza kesi, kuandaa hukumu na kutafsiri sheria kwa mujibu wa ujuzi wao wa kisheria. Hiyo amri unayosema ilitolewa dhidi ya TANROADS bila shaka nimetolea ufafanuzi hapo juu.
Incidence nyingi zimetokea kwa majaji kupakaziwa nyaraka za kusaini wakati haziko sahihi na hazikustahili kuwa nyaraka za mahakama. Mara nyingine hii husababishwa na rushwa iliyotawala ndani ya mahakama.
Ahsante