Uhalisia wa watanzania

Uhalisia wa watanzania

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
53,000
Reaction score
104,440
Tumekuwa tunajidanganya na kuwadanganya watu wa ulimwengu kuwa watanzania ni wakarimu, wapenda amani, wacheshi, kupendana na mengine mengi ya sifa nzuri. Si kweli, watanzania wana roho mabaya, makatili, wanafiki, wauaji etc. Ni muda na nafasi vilikuwa havijajitokeza.

Sasa muda na nafasi vimejitokeza, angalia:

1. Wasio na ajira za serikali walishangilia na bado wanashangilia na kufurahia watu kufukuzwa kazi vyeti, darasa la saba, etc. Kuwa wacha tukose wote ajira.

2. Walio mitaani wanashangilia wafanyakazi wa serikali wanavyonyanyaswa na kudhihakiwa, kutishwa etc, wacha waipata.

3. Wasiokuwa nacho wanafurahia watu kufungwa kushitakiwa, kufirisiwa, kubomolewa, kunyanganywa mashamba.

4. Wenye vyama vyao vilivyo madarakani wanafurahia mateso ya vyama pinzani.

5. Walio na madaraka wanafurahia kukandamiza wasio na madaraka.

6. Watu wanafurahia wenzao kupigwa risasi.

7. Watu wanafurahia magonjwa ya wenzao.

Upendo, amani vilivyokuwa vinanadiwa na kunatangazwa ndani ya watanzania haya yanayoendelea yasingelikuwepo sasa.
 
HAWA NDIO WATANZANIA MKUU.SIKU ZOTE HUPENDI ALIE NACHO AISHIWE AWE KAMA WAO
 
Back
Top Bottom