Uhalisia wa vita ya 'makinikia'

20fanaka

Senior Member
Apr 19, 2017
141
113
Anaandika Dr.Kilangi, nguli Wa Sheria za madini na ni Director Wa SAUT Arusha centre na mhadhiri vyuo vingi vinavyofundisha Sheria za madini
............................................
Wandugu,

1. Nitaomba tuvumiliane. Niliombwa kusema kitu. Nitaandika kwa kirefu kidogo. Kwa kuwa ninaandika muda huu, nina advantage ya kuwa nimesoma maoni mengine yaliyotangulia. Nilicheka sana kaka yangu Ngwilimi aliposema halali hadi nimetoa maoni. Sipendi kumkosesha usingizi. Nitaandika kwa paragraphs ili kurahisisha rejea.

2. Nimeangalia maoni mbalimbali yaliyotolewa humu. Yanagusa maeneo yafuatayo:

i)Statement ya Acacia.

ii)Suala la sovereignty over natural resources na tatizo la 'state capture'.

ii) Suala la smelting na mchanga wa makinikia.

iv)Nini tunaweza kufanya kwenye mikataba:
- kuvunja mikataba?
- kushitaki kwa kutuibia?
- ku-review mikataba?
- au kuweka mikataba wazi?

vi) Sheria za kimataifa.

3. Haya ni mambo mengi na mazito. Sio rahisi kuya-summarize kwenye text ya simu. Pia ni vema kukubaliana kuwa kwenye mjadala kama huu itikadi, vyama na mihemuko iwekwe pembeni. Hoja zitawale.

4. Sitaingia kwenye mtego wa kulaumu au kutetea mtu. Nitajikita kwenye masuala ya msingi yanayotengeneza chimbuko la tatizo. Matatizo katika sekta yetu ya Madini, kama ilivyo ktk nchi nyingi zinazoendelea, nyingi zikiwa Africa, na Tanzania ikiwemo, yana chanzo chake ktk maeneo matatu:

i) Falsafa inayotuongoza,
ii) Sheria inayotuongoza.
iii) Mfumo wa utawala.

FALSAFA INAYOTUONGOZA

5. Malalamiko kuwa nchi zinazoendelea na zenye kumiliki resources zinapunjwa hayakuanza leo. Yalianza miaka ya 1950. Haya yalipelea kuibuka kwa falsafa mbili: resource nationalism na resource liberalism. Kila moja ina implications kwenye sheria na kwenye namna nchi itasimamia raslimali zake.

6. Wale wa resource nationalism walitaka nchi iwe na mamlaka kamili kwa resources zao na ziwasaidie na wakatengeneza principle ya permanent sovereignty over natural resources. Walitaka mambo haya yasimamiwe zaidi na sheria za nchi.

7. Wale wa resource liberalism wanataka raslimali ziwe wazi kwa dunia nzima maana mgawanyo wake duniani hauna usawa (japokuwa wao wamelinda teknolojia yao).

8. Katika vision ya nchi, nchi inachagua falsafa ya kufuata. Falsafa inayofuatwa huathiri sera na sheria.

9. Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata falsafa ya resource nationalism hadi 1979. Kuanzia 1979 Tanzania ikaanza kufuata resource liberalism baada ya shinikizo la World Bank na IMF chini ya kitu kinaitwa Washington Consensus. Falsafa hii ilifikia kilele miaka ya 1990 mwishoni. Kwa hiyo ikaathiri sera na sheria.

10. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 2000 nchi imejaribu kurudi kwenye resource nationalism lakini inakwama. Sasa hivi resource nationalism sentiments ziko very high.

SHERIA INAYOTUONGOZA

11. Kama nilivyosema, falsafa huja kuathiri Sera na Sheria. Sheria muhimu hapa ni (nitachanganya lugha kidogo hapa):

i) investment law
ii) mining/petroleum law
iii) tax law.

Investment Law

12. Hiki ni chanzo kikubwa cha ugomvi. Nchi zilizoendelea zimeshinikiza uwepo wa mfumo wa sheria wenye kugandamiza nchi zinazoendelea. Mfumo huu unagawanyika kama ifuatavyo na kila kipande kina matatizo makubwa na mengi.

i) customary international law. Humu kuna principles nyingi ambazo nchi inaweza kuambiwa kuwa imezivunja. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinagombana juu ya principles hizi.

ii) multilateral framework. Hapa kuna mikataba ya mataifa mengi. Tanzania ni mwanachama Wa mikataba miwili yaani unaoanzisha Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na unaoanzisha International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID).

iii) bilateral framework. Hii ni mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties - BITs. Ila inawalinda wawekezaji toka nchi hizo mbili. Nchi inaweza kushindwa kesi sio sababu ya mikataba ila kwa sababu ya BITs.

iv) national framework
(mining and petroleum acts) - hizi zina certain aspect fulani za investment.

v) state-investor agreements (tunayoita mikataba na wawekezaji).

Wengi tunaangalia hii tu. Hatuangalii hizo frameworks zingine ambazo baadaye zinatukandamiza.

Pia, framework No. i, ii, na iii ziko chini ya himaya ya sheria za kimataifa.

Mining/petroleum law

12. Mining and petroleum law hutengenezwa na nchi yenye resources. Lakini nchi zilizoendelea huwa zina-influence mno zoezi la utngenezaji sheria hizi, maana hizo ndio hutoa mineral or petroleum rights. Wako tayari hata kuidanganya nchi kwa misaada wanayojua tunahitaji sana. Wanaweza kutudanganya kuwa wanatupatia technical support. Kumbe wanatutengenezea sheria itakayowezesha kutuibia.

Tax Law

13. Tax law ni Eneo jingine ambalo linatumika sana kutuibia. Mnapokuwa mnatengeneza sheria zenu za kodi hawa jamaa hawaachi kuwazungukieni na kuwa-influence.
MFUMO WA UTAWALA

14. Kuna tatizo kubwa sana linalozikumba hasa nchi za Africa na baadhi ya zinazoendelea zilizo nje ya Africa. Hili ni tatizo la 'state capture'. Kama ilivyo concept ya 'river capture' kwenye geography, basi state capture means influence by the elite or business people or investors such that the state (led by its government) fails to think on its own and it follows the thinking of the group that has captured it.

15. Wakati wa kufuata falsafa ya resource liberalism, Tanzania iliingia kwenye total 'state capture'. Ndio kusema tuliondoa kichwa chetu tukaweka kichwa kingine. Tukawa tunafikiri kwa mfumo wa hicho kichwa kingine. Sasa tumeanza kurudisha kichwa chetu.
SUALA LA MCHANGA WA MADINI

Utangulizi

16. Suala hili wote tunajua background yake. Kamati ya Pili natumaini itafanya kazi ya na uchambuzi Wa kutosha.

Mchanga kwenye Madini ni Mali ya nani?

17. Principle ya 'permanent sovereignty over natural resources inasema huu ni Mali ya nchi. Article 27 of the Constitution of the URT inachukua mwelekeo huo huo. Hata Section 5 of the Mining Act says the same. And the same position was in Mining Acts za 1998 na 1979. Zile za kabla ya Hapo ziikuwa zinazungumzia mwingereza.

18. Hata hivyo kuna ubishi kuwa pale nchi inaposaini state-investor agreement (Mineral Development Agreement) na kutoa mineral rights je nchi inakabidhi sovereignty yote kwa companies. Makampuni yatasema 'ndiyo'. Nchi zinatakiwa ziseme 'hapana'.

19. Mineral rights means rights to extract minerals and sell them. Does it include transporting them outside the country in order to extract minerals? I don't think if contracts say so. And if they do, that defeats the principle of permanent sovereignty over natural resources!

Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

20. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya 'fair and equitable treatment', na 'state responsibility' na ya 'respect for acquired rights'. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.

21. Kuwashtaki makampuni kwa kutudanganya? Tunaweza, na tutatumia argument kuwa wamevunja customary law principle ya 'good faith and prohibition of abuse of rights'. Lakini wakisema uchunguzi wa mchanga tumeufanya kwa upande mmoja wanaweza kushinda.

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.

23. Kuiweka wazi mikataba ili watu wote waione? Investors wataegemea kwenye principle of confidentiality of investment agreements. Hii principle IPO katika international law. Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji - Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.

24. Kwa hiyo kumbe tunaweza kufanya nini sasa? KAMA ALIVYOSEMA MHESHIMIWA RAIS, HII VITA, NA HII NILIYOTOA HAPA NDIO PICHA HALISI YA VITA HII.

Basi wandugu siku nyingine msinitafute ili nitoe Maoni yangu. Vinginevyo mjiandae kusoma kitabu.

Dr. Adelatus Kilangi

©copy and pasteu
 
Namba 21 hapo ina mantik, ispokuwa km bado kuna nafas ya kujustfy report ya Profeser Mruma kwa kufanya sampling nyingine kwa kutumia kamati hii hii lakini safari hii ikihusisha pia wadau wengine watakaokubalika na pande zote mbili wakitumia sample ambazo hazijaguswa. (kuondoa utata iwapo zimechakachuliwa/ kuongezewa concetration ya hayo madini)
 
Hii ndio shida ya wasomi wetu, wanapenda kuwa nice guys kwa kutokutaka kuchukua upande. Pamoja na maelezo mazuri ingenoga zaidi kwa kusema mkuu na tume na kampuni nani anamakosa,na kakosea wapi nini kifanyike.

Lkn mimi nimeona amegusia kila jaribio kile tunachoweza kufanya na challenge yake kisha akaacha wahusika wajue cha kufanya.
Ukiread mind na matamanio ya wazalendo wa nchi hii utagundua wangependa ACACIA ishtakiwe na ilipe fidia ya udanganyifu wa nyuma na ianze kulipa malipo halisi ya kile wanachosafirisha.

Jambo hili amelieza Doctor ktk aya no21 na changamoto yake. Uwezekano wa jambo hili kufanikiwa nimejaribu kueleza ktk comment yangu iliyopo no 3 hapo juu.
 
20fanaka,
Shukrani kwa kuweka maoni ya msomi Dr. Adelatus Kilangi. Ushauri wake unafanana pia na wa nguli msomi mwenzie wa sheria Mh. Tundu A. Lissu.

Maamuzi ya "mchanga wa dhahabu" yataitikisa nchi na kupelekea hasara nyingi ikiwemo kulipa fidia kubwa na nia ya kuvutia uwekezaji mkubwa nchini toka wawekezaji wa ndani na kimataifa kuigia dosari kutokana na hofu ya kutoijua kesho itakuwa vipi maana "sera" ya serikali ni ya "Maamuzi ya kukurupuka".
 
Songambele Hakuchukua upande ndio imekusaidia a lay person kama wewe na Mimi kuwa na balance kwenye kufikiri!
Yeye hatetei kesi yeyote hapa,yeye Ana inform public na hakuna best approach zaidi ya kuwa neutral
 
Dr aksante sana nimekuelewa !
Ngoja nitoe copy nipitie tena baadae.

VITA YA 1978 CHA MTOTO SANA!!!!!!!!!
 
BADO NAAMINI TANZANIA TUTASHINDA HII VITA.
NCHI YETU NA MADINI YETU

MUNGU SAIDIA
 
Mawazo yasiyo na mihemko na kwa lugha rahisi. Hili andiko linatakiwa kuwafikia watu wengi iwezekanavyo, hasa wale wanaofikiri kila anayepinga aproach ya president ni adui.
 
Kwakweli nimesoma kwa kurudia ili nione kama kuna upenyo lakini sioni, naona tumebanwa kila kona. Na Magu akijifanya mbabe kwenye hili suala ndio tutaumia zaidi. Labda tufuate ushauri wa Lissu unaweza kutusaidia.
 
Rais nae anafikiri na anajopo la washauri na wanasheria na ndio maana alitengeneza kamati nyingine ya kisheria zaidi,sasa basi tuisubiri hiyo ijayo sio sasa kila mmoja uzalendo umemuisha anataka nchi ishindwe kesi ili watafute matarumbeta,mungu atawalaani kila ajae kwa siri tuijue yake shari!
 
Pamoja na haya yote uliyoyaeleza vizuri na kwa ufasaha bado natakuelewa sheria ina sema nini juu viongozi wetu kutembelea/kukagua migodi ya hawa wanaoitwa wawekezaji imekaa kimya au inakatazo?
 
Hii ndio shida ya wasomi wetu, wanapenda kuwa nice guys kwa kutokutaka kuchukua upande. Pamoja na maelezo mazuri ingenoga zaidi kwa kusema mkuu na tume na kampuni nani anamakosa,na kakosea wapi nini kifanyike.
Mkuu mbona Dr kaonyesha kila kitu. Jiongeze tu utaona tayari kitanzi kishavalishwa shingoni bado tu kuondoa stuli mtuhumiwa apoteze uhai.
Ishakula kwetu tayari. Chezea wazungu na makuwadi wazalendo wa uchumi
 
Back
Top Bottom