Uhalisia wa taifa la Israeli

Umejitahid kuelezea lakin yote ni sifur ngoja nikipata muda nitakujibu kila kitu. Japo kwa kifupi biblia inasema kumkataa Yesu kwao ilikuwa ni lazima ili litimie lile neno yaan ni sawa na kusema yuda iskarioti alimsaliti Yesu ili unabii utimie
 
Hongera mkuu. Umeyupa elinu ya kutosha. Mara nyingi sisi waafrika tuba tabia ya kujidharau hivyo wengi watakupinga kwa hulka zetu bila kuleta maandishi. Ni ukweli usopingika kuwa siye waafrika ndio wacha Mungu kuliko jamii zingine. Kwa hiyo ndio taufa teule sio hao wazungu.
 
Kuweka reference za kwenye bible kumenifanya nijitoe kwenye huu uzi
 
Ndugu ukimzungumzia myahudi unazungumzia -Tora. Na asilimia kubwa ya wayahudi hawatumii biblia .
 
Umejitahidi kueleza kwa kirefu lakini umeacha maswali mengi kuliko majibu uliyojaribu kujibu kwenye Akili za walio wengi.
Nijibu maswali yangu machache nikijibiwa nitarudi tena,

(1) wayahudi wa kweli mpaka sasa wako wapi?na nchi gani?

(2) Ni ushahidi gani unauotoa kudhihirisha kwamba wale wajakazi wa wake wa yakobo ambao Yakobo alizaa nao ni weusi kutoka kushi?

(3)biblia inaonyesha baada ya Yesu kupaa wanafunzi wake walikimbia uyahudi kuogopa kuuwawa na kukimbilia maeneo mbalimbali kama korintho,efeso, filipi,na maeneo mengi.
Na siku ya sabato walikuwa wakiingia kwenye masinagogi ya wayahudi kuhubiri habari za Yesu.
Je huko waliokuwa wayahudi ktk maeneo niliyotaja ndiyo huko ethiopia?

Yaani Filipi,korintho efeso ,Rumi na kwingineko ndio huko Ethiopia na misiri kwa waafirica wenzao?
 
Kuna point unazo lakini naona umeandika kishabiki saana hasa wa udini pia, nijuavyo mm jukwaa hili halipo hivo watu wanakuja na facts. Huu uzi ungefaa jukwaa la dini sio hapa.
 
Umejitahid kuelezea lakin yote ni sifur ngoja nikipata muda nitakujibu kila kitu. Japo kwa kifupi biblia inasema kumkataa Yesu kwao ilikuwa ni lazima ili litimie lile neno yaan ni sawa na kusema yuda iskarioti alimsaliti Yesu ili unabii utimie
Sawa,kwahiyo Yuda hakutenda Dhambi kumsaliti Yesu kwakuwa tu alikuwa anatimiza unabii?,Na wana wa israeli hawakutenda dhambi kumkataa,kumtesa na hatimaye kumsulubisha Yesu kwakuwa tu walikuwa wanatimiza unabii? Sio kweli, Biblia imesema wazi Luka 17:1 "Majaribu hayana budi kuja ila ole wake anaye yaleta"! unabii ukiandikwa lazima utimie lakini ole wake huyo anayeutimaza kwa dhambi hukumu yake ipo pale pale kama asipo tubu!,Biblia imetabiri siku za mwisho zitakuwa ni siku ambazo maasi yataongezeka Je watakao kuwa wanayafanya hayo maasi watakuwa wanatimiza unabii so hawatendi Dhambi?,Yesu aliwaambi wanafunzi wake kuwa watateswa,watadhihakiwa na watauawa kwaajili ya jina lake Luka 21:12 kwahiyo unataka kusema waliowaua mitume hawakutenda dhambi kwakuwa walikuwa wanatimiza unabii wa Yesu?
Yesu alimwambia(alimtabiria) Petro kuwa utanikana mara tatu (MATHAYO 26:34) na kweli Petro akamkana mara tatu kabla jogoo hajawika exactly na neno alilosema Yesu ,alitenda dhambi ndiomaana akaenda kutubu na kulia kwa uchungu!
"DHAMBI NI DHAMBI TU ukiitenda ukiwa unatimiza unabii au la!, mbele za Mungu inabaki kuwa Dhambi"!
 
Na katka watu wte walotolewa utumwan misri waliofika nchi ya ahad hawakuzid 5
 
Na katka watu wte walotolewa utumwan misri waliofika nchi ya ahad hawakuzid 5
Upo sahihi ila bado walikuwa waisrael,au tuwaiteje?haijaandikwa kuwa wapo waliojiunga nao njiani. Ukiweza kuibariki Israel ibariki.ukitaka kuilaani Fanya hivyo umepewa huo uhuru wa kuchagua.hata ukimchagua mfilisti ni haki yako haya ni masuala ya kiimani zaidi.

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Hii habari imekaa kiitikadi zaidi. Leo ningeulizwa upande wenye nafuu ningesema Israel kuliko Palestine, kwa sababu gani? Kwa mtazamo wangu wote wanao tetea Israel they are not aggressive, na wauaji, ila ukiona au kusikia wanaopenda itikadi zinazofanana na wapelestina na hasa kiini, they are too dangarous, very demanding for nothing even in our country some are like that! Hata leo ukifuatilia duniani hutashangaa kuwa wameua! Sasa kama wao ndiyo wayahudi kweli na ni matajiri wa ROHO hii ROHO ya kuua wanadamu ni ya kimungu? Kuonewa au uwepo wa wayahudi fake ni kibali cha kuua watu pote walipo duniani? Kiukweli hata mwandishi wa habari hii....???
 
Mleta mada, binafsi nataka kujifunza. Nasubiri kwa hamu ujibu kwa uwazi swali uliloulizwa mara kadhaa kuwa wayahudi halisi wako wapi kwa sasa? Au ndio hao kabila la Igbo la Nigeria ulilotaja hapo?! Kama ni hilo, ni watumwa wa nani?
 
Haionyeshi kama walichukua watu wengine njian au lah,,,Na tukumbuke jina Israel alipewa Jacob baada ya kumshinda malaika so kama sio uzao huo sidhan km kuna Israel nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…