Michael Dudicoff
JF-Expert Member
- Aug 20, 2024
- 203
- 270
Habari za muda huu.
Niende kwenye mada Moja kwa moja.
Chama Cha Mapinduzi hakijakosa hela kiasi cha kuandaa harambee ya watu kukichangia pesa za kuendesha shughuli za uchaguzi.
Miaka yote chama kimekuwa kikishiriki uchaguzi pasi na kuhitaji watu kukichangia.
Lengo kuu la harambee ile ilikuwa ni kupeleka ujumbe kwa wapinzani wa mama Samia wanaodai kwamba mama Samia hakubaliki na watu wamemchoka, na kwamba ndani ya CCM kuna mpasuko , kuwaonyesha kwamba bado CCM ina umoja na iko pamoja na mama Samia na kwamba watanzania wa kada tafautitafauti bado wapo pamoja na mama Samia na wapo tayari kumuunga mkono kwa kila hatua ya kisiasa anayoichukua kwa ajili ya maendeleo ya chama na serikali.
Kitendo cha kupata zaidi ya bilioni 80 ndani ya siku moja kati ya bilioni 100 zinazotakiwa ikiwa ni mchango kutoka makundi tafautitafauti wakiwemo wanasiasa, wafanya biashara wakubwa , wachimbaji wa madini, klabu za mipira na makundi mengine ni ujumbe kwa wale wanaompiga vita mama Samia na pia wanaosambaza propaganda za kwamba kuna mpasuko ndani ya CCM kwamba wanapoteza muda wao bure kwakuwa mama Samia bado anakubalika sana na kuungwa mkono na watanzania wengi wa makundi tafautitafauti.
Wapinzani wa mama Samia wanatakiwa kutafuta kazi nyingine ya kufanya kwakuwa kadiri wanavyompiga vita ndivyo ambavyo watanzania wanazidi kuwapuuza na kuongeza nguvu za kumsapoti rais Samia.
Moja ya maneno yaliyowavunja moyo wapinzani wa mama Samia ni maneno aliyoyasema dk Emmanuel Nchimbi baada ya mama Samia kuchukua fomu ya kugombea urais ya kwamba DK NCHIMBI AMEJIANDAA KUWA MSAIDIZI WA RAIS SAMIA NA HAKUJIANDAA KUWA MSHINDANI WAKE!.
Naomba kuwasilisha.