Uhalifu wa kutisha dhidi ya wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhalifu wa kutisha dhidi ya wanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimbori, Mar 18, 2012.

 1. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,724
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Kuna uhalifu na unyama wa kutisha unaofanywa na; viongozi, waalimu n.k dhidi ya wanafunzi wa kike katika shule Msingi na Sekondari hapa nchini.
  Nimepata kusikia visa kadhaa vya wasichana waliosumbuliwa na kteswa kwa kukataa kufanya mapenzina waalimu n.k hata wakaridhia kuacha shule, huku jamii ikiwalaumu bila ya kujua sababu.
  Hali ni mbaya sana kwenye shule za serikali, na za taasisi zilizo chini ya serikali.
  Wanafunzi walio katika hatari kubwa ni wale wenye mili nikubwa na wanaotoka katika familia masikini.
  Tunapaswa shule mwanafunzi ayokwenda mwanafunzi, pia wazazi waongee na wanafunzi kwa kina ili kujua mahusiano yao na waalimu wao yapoje. Kama unajua shule chafu utusaidie ili kunusuru wadogo zetu. Pamoja Twaweza
   
 2. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Mkuu, nadhani wazo lako ni zuri ila sina uhakika na unaloliita 'ukatili wa kutisha' hapo itabeba nadharia kuwa walimu wakiume wote au wengi wao hufanya hayo! Pia sijajua umetumia vigezo gani mpaka ukafikia tamati ya kusema ukatili wa kutisha. Hata hivyo ukatili upo ila hujatueleza ni kwa kiwango gani, mikoa gani, shule zipi, sekondari au primary au vyuoni, waathirika ni wangapi kwa mwaka nk.
  Naamini hata watoto wa kiume wanapata manyanyaso sana tena kutoka kwa walimu wa kike pia, akikuona unaurafiki na mwanae au ndugu au jirani wa kike ni balaa, utahamishwa darasa na mambo kadha wa kadha zikiwemo adhabu.
  Wandugu, mtoto ni either wa kiume au kike anatakiwa kulindwa na jamii, tusimpe upendeleo mmoja tukasahau mwingine akaja kuharibikiwa.
   
 3. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,724
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Kila mtoto anayo haki ya kulindwa, kila mwanajamii anapaswa kujua hatari zilipo. Nimeshindwa kupata tarakimu kamili kwa kuwa, hii ni uzoefu wangu nikiwa shule ya msingi, sekondari na sasa ni sehemu ndogo ya mfumo wa elimu. Niliyosema ni ya kweli, kwani kuna visa kadhaa nimewahi kusimuliwa na kushuhudia, kwa wanafunzi wa kike wanaodhaminiwa na shule kufukuzwa shule na mkuu kwa kuwa walikataa ngono. Nasema ni ukatili wa kutisha kwa kuwa kuna baadhi ya shule, hususani za..., takribani wanafunzi wote wa kike wanalazimishwa kufanya ngono na baadhi ya waalimu wahalifu. Mwanafunzi akikataa anapewa adhabu kwa makosa ya kusingizia, hata baadhi yao kuogopa kuwauliza walimu maswali au kuomba ufafanuzi. TUJITAHIDI KULEA WADOGO ZETU.
   
Loading...