Uhalali wa Mauaji: Je, Tunaongozwa na Waliokosa Amani ya Nafsi?

Uhalali wa Mauaji: Je, Tunaongozwa na Waliokosa Amani ya Nafsi?

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
519
Reaction score
1,463
Katika nyakati za giza la kiutawala, ambapo siasa imegeuka kuwa uwanja wa majeraha ya nafsi na miili ya raia, tunalazimika kuuliza kwa sauti ya juu: Ni kwa kiasi gani utu wetu unadhalilishwa kwa kisingizio cha uongozi?

Utekaji wa watu wasio na hatia, kuuawa kwa siri, na kutoweka kwa sauti za haki si matukio ya ajali ya kisiasa — ni dalili ya mfumo uliokosa moral legitimacy. Haiwezekani tukakubali kuwa "leadership" ni kwa wale wenye uwezo wa kutisha, kuumiza na kuondoa wengine kwa hila na nguvu. Huo si uongozi, huo ni utawala wa kishetani uliojifunika koti la demokrasia.

Tunajiuliza: Nani anatoa uhalali kwa mtekaji kuwa mgombea? Nani anabariki muuaji kuwa kiongozi wa watu?

Katika tafsiri ya kina ya psychopolitics, watu wanaotenda maovu haya si viongozi bali ni watu waliokosa amani ya ndani (inner peace), wanaoishi kwa woga wa siku zao wenyewe, wakiamini kuwa silence ya waliodhulumiwa ni ushindi. Ni makosa ya kihistoria kufikiri kuwa damu ya asiye na hatia inaweza kuficha uovu kwa muda mrefu. Historia huwa haifutiki, na nafsi za watu haziwezi kupumbazwa milele.

Power acquired through blood is inherently fragile. Hakuna utawala uliojengwa juu ya mifupa ya raia ukadumu kwa heshima wala uhalali wa kweli. Maumivu haya tunayoyapitia — kutekwa kwa wapendwa wetu, kuondolewa kwa sauti huru, kutishwa kwa familia zetu — hayawezi kuwa “acceptable cost of politics” katika jamii ya watu waliostaarabika.

Hii nchi si ya familia zenu. Hii nchi si taasisi binafsi ya kuendeleza vizazi vya kihuni kisiasa. This is not a dynastic enterprise. Ni ardhi ya raia wenye akili timamu, wenye haki ya kusema, kukosoa na kudai heshima ya utu wao.

Tutazidi kusema. Hatutazimwa. Sauti ya haki huwa na mwangwi wa milele. Na kama hamuwezi kusikia kwa sasa, basi jiandaeni — justice haikimbiwi, inachelewa tu. Mtazungukwa na majeneza yenu wenyewe, siyo ya miili ya watu mliyoiondoa kwa hofu yenu.

Haki haifi. Na dhambi za damu hazifutwi na propaganda.
Na kwa hakika, roho za waliotekwa na kuuawa kwa ajili ya kusema kweli, zitabaki kuwa mashahidi wa milele wa uovu wenu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom