Uhakiki wa Watumishi hewa serikalini huendane na uhakiki wa vyeti

Munu

Member
Jan 8, 2014
26
6
Swala la uhakiki wa watumishi hewa serikalini ni zuri na faida kwa nchi maana hili tatizo limesababisha hasara ya muda mrefu, kwa maoni yangu ni vizuri uhakiki huu ukaendana na ukaguzi wa vyeti maana kama tutaendelea kubaki na watumishi ambao wapo kazini kweli na wameajiriwa lakini hawana sifa ya nafasi waliyopo bado ufanisi wa kazi utaendelea kuwa chini na serikali itandelea kupoteza hela kwa kuwalipa mshahara watu ambao wahastahili
 
sawa tumekusikia...
ila vipi kama kaingia na cheti sio chake ilhali utendaji kazi wake ni wa ufanisi hapo je tunafanyeje..??

maana mie binafsi siamini vyeti vya makaratasi
 
Mtu anaweza akawa mtendaji lakini sio mwadilifu.
Kitendo cha kuwa na cheti feki kinaonyesha kuwa umeajiri jambazi.

Hii nchi kwa muda mrefu sasa imekua ina watumishi majambazi yaliyoiba vyeti na matokeo yake ni kuporomoka kwa maadili. Mwizi ni mwizi tu.
Ni bora ungemwajiri darasa la saba na akajijua na akajulikana hivyo atasimama kwa uadilifu na unyenyekevu mkubwa kuliko kuajiri msomi aliyeiba cheti.
Huyu atakua mbabaishaji.
Enzi za Mwalimu Nyerere palikua na walimu wa UPE lakini walikua wanafundisha kwa moyo wote. Na wanafunzi wengi walifundishwa na walimu hao.
Palikua na madaktari na Manesi wa M.A na RMO wenye Elimu ya kawaida tu lakini walikua hawatukani wagonjwa na kuficha dawa. Walikua waadilifu pamoja na Elimu zao ndogo. Leo hii kuna baadhi ya madaktari wenye kutia mashaka ambao kila wagonjwa kumi wanaofanyiwa oparation 7 wanakufa kwa uzembe. Hao ni wale walioiba vyeti vya ndugu wenye division one na kwenda kusomea udaktari.

Suala la kujuana limesababisha kuajiriwa kwa wafanyakazi wengi wenye vyeti vya bandia kutokana na ukweli kuwa walioko juu ndio waliowatafutia ndugu zao vyeti feki na mara nyingine kuwanunulia mitihani ili tu wapate ajira ,na wanakua hawana wasiwasi mana anayekagua hivyo vyeti ndiye aliyempa ajira kwa cheti feki na anajua hilo.

Hawa ni majipu makubwa sana.
 
NA TUKIZUNGUNZIA WATUMISHI HEWA, ISIISHIE HAPO TU,KUNA WANAFUNZI WENGI SANA KWA SASA WANASOMESHWA NA SERKALI YA MAGUFULI NJE YA NCHI ...NA NIPESA NYINGI SANA..
MBAYA ZAIDI KUNA WANAFUNZI HEWA WENGI SANA. .YAANI ULAYA HAWAPO, EIDHA WAMEKUFA, WAMEFUKUZWA, WAMESHINDWA MASHALT YA VYUO NA.
LAKINI PESA INAONEKANA INATUMWA KILA MWEZI NA KILA MWAKA.

HIKI NACHO NI KIJIPU, WATUMISHI HUSIKA WANAJINUFAISHA NA HIZO PESA.
 
Swala la uhakiki wa watumishi hewa serikalini ni zuri na faida kwa nchi maana hili tatizo limesababisha hasara ya muda mrefu, kwa maoni yangu ni vizuri uhakiki huu ukaendana na ukaguzi wa vyeti maana kama tutaendelea kubaki na watumishi ambao wapo kazini kweli na wameajiriwa lakini hawana sifa ya nafasi waliyopo bado ufanisi wa kazi utaendelea kuwa chini na serikali itandelea kupoteza hela kwa kuwalipa mshahara watu ambao wahastahili
Mkuu hapo unaongelea ualimu,polisi,magereza,jwtz na taasisi kibao za serikali sio rahisi,tujipange hapa tulipo kwenda mbele,tukubali nimakosa tulifanya
 
Vyeti feki ni tambazi, lakini hamna hata MTU anayethubutu hata kulitomasa, watumishi hewa ni jipu Sawa litumbuliwe lakini vipi kuhusu hili tambazi?
 
Ha ha ha Tambazi tena lippo kwapani!..lkn haina jinsi litumbuliwe tu....pambavu inatia hasira Sana.
 
Swala la uhakiki wa watumishi hewa serikalini ni zuri na faida kwa nchi maana hili tatizo limesababisha hasara ya muda mrefu, kwa maoni yangu ni vizuri uhakiki huu ukaendana na ukaguzi wa vyeti maana kama tutaendelea kubaki na watumishi ambao wapo kazini kweli na wameajiriwa lakini hawana sifa ya nafasi waliyopo bado ufanisi wa kazi utaendelea kuwa chini na serikali itandelea kupoteza hela kwa kuwalipa mshahara watu ambao wahastahili

Unatafuta kulogwa ndg yangu achana na hizo habari
 
Mkuu hapo unaongelea ualimu,polisi,magereza,jwtz na taasisi kibao za serikali sio rahisi,tujipange hapa tulipo kwenda mbele,tukubali nimakosa tulifanya

Ni rahisi na ni lazima watumbuliwe.
Hawa ndio wezi wakubwa kwenye sekta za umma na sekta binafsi.
Wengi pia wapo sekta binafsi kuliko hata serikalini. Hawa watu kama wako majeshini ni wachache na hawazidi elfu mbili lakini athari yake ni kubwa kuliko kuwaacha.
Hawa ni mawakala wa wahalifu.
Sio wazalendo kabisa. Kwao kila kitu ni dili. Na kila jambo wanalofanya linalenga maslahi tu. Na wanapokosa kule wanachokilenga wanakitafuta kwa njia zisizo halali.
Hawa ndio wanaopaka matope taasisi hizo.
Ukimwona mwalimu aliyepata ajira yake kwa cheti chake halali hata kama ana division 4 lakini anajituma na anawapenda wanafunzi wake na anafanya kila mbinu kuinua elimu ya mtanzania. Kwake ajira haipatikani kwa dili

Hawa wenye vyeti feki ndio wanaonunua madaraka na vyeo kwa fedha na ngono. Na pia kama ni mabosi wanatoa haki kwa rushwa ya fedha na ngono. Hawa ndio wanaoendekeza vitendo vya ushirikina na uchawi na mara nyingine kuwaua wale wenye vyeti halali kwa woga wa kushindwa kiutendaji na ubunifu.

Bila kuwasaka walipo watu wenye vyeti feki bila kujali taasisi walizozidanganya zoezi la kutumbua majipu litakua halijafika kwa haki.
Haikubaliki na sio haki hata kidogo kuwanyima ajira watu waliosomea vyeti vyao kihalali kwa juhudi kubwa na kwa gharama kubwa halafu wapewe nafasi watu wenye vyeti feki na wanaotumia cheti kimoja kwenye ajira zaidi ya moja.

Huu sio uzalendo ni ujasiri wa kuliibia taifa.
Wanajiamini nini hadi wafoji vyeti na kuajiriwa bila hofu?
Nani anawalinda na vyeti vyao feki? Kila mtu atavuna alichopanda.
 
Hahahah umenikumbusha mbali kweli,"nifundishe nisifundishe mshahara wangu unaingia"
 
Nakubaliana na hoja kweli wale walioingia serikalin kwa vyeti vya kugushi ndo hawa wengi wao wanaenda ndivyo sivyo na maadili ya kazi...hili swala linatakiwa liwekewe mkazo ili watu hawa wawajibishwe na pengine watoe fain kwani wameingiza serkali hasara kubwa.
 
vyeti feki ni tatizo kubwa kwenye nchi hii natamani watangaze motisha fulani ili waumbuliwe kwani wapo kila sekta mpaka bungeni na ndio wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi kwani wanafikiria maslahi yao kwanza
 
wakiweza kuwaondoa hao vyeti feki Nchi itaanza kuwa na maendeleo maana maamuzi mengi yatafanywa na wasomi kweli sio hao wa makaratasi tu.
 
Swala la uhakiki wa watumishi hewa serikalini ni zuri na faida kwa nchi maana hili tatizo limesababisha hasara ya muda mrefu, kwa maoni yangu ni vizuri uhakiki huu ukaendana na ukaguzi wa vyeti maana kama tutaendelea kubaki na watumishi ambao wapo kazini kweli na wameajiriwa lakini hawana sifa ya nafasi waliyopo bado ufanisi wa kazi utaendelea kuwa chini na serikali itandelea kupoteza hela kwa kuwalipa mshahara watu ambao wahastahili

Mr Munu, tunaanza na pesa za serikali kwanza na mambo mengine yanafuata kuwa na subira ni suala la mda tuu.
 
vyeti feki utavigunduaje?mfano utagunduaje kama cheti changu cha udsm ai udom ni feki?
 
sawa tumekusikia...
ila vipi kama kaingia na cheti sio chake ilhali utendaji kazi wake ni wa ufanisi hapo je tunafanyeje..??

maana mie binafsi siamini vyeti vya makaratasi
Cheti sio chako umekiiba au umekipata kwa udanganyifu....maana yake wewe ni jizi kama majizi mengine ,huna uadilifu unapaswa uondoke .Achia nafasi yupo mwadilifu na mchapakazi aliyestahili hiyo nafasi lakini kutokana na kujuana ukawezeshwa kuipora hiyo nafasi.
 
Back
Top Bottom