Uhakiki wa wahitimu wa ualimu(sayansi) utakamilika tarehe 18/01/2017 kama mkifuata ushauri huu

ENANTIOMER

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
1,419
804
Poleni kwa uchovu wa kazi ngumu, hongereni kwa kazi nzuri ya kulitumikia taaifa enyi nyinyi watumishi wa wizara ya elimu.

nina wazo ktk zoezi la sasa la uhakiki wa vyeti vya wahitimu wa fani ya ualimu(sayansi). kwakua mmewaambia wahitimu waweke vyeti vyao ktk faili moja la pdf, pia kila mmoja aandike jina lake kwenye file lake, na atume mara moja tena kwa kutumia barua pepe yake mwenyewe; ninaamini kwamba idadi ya barua pepe itakua sawa na idadi ya wahitimu wataohakikiwa, na idadi hiyo itakua ndogo kwani kila muhitimu atatikiwa kutuma file moja tena mara moja.

sasa kazi haitakua ngumu kama ya awali ambayo wengine walituma mara nyingi zaidi na kulata usumbufu ktk kuhakiki. sasa kwakua kazi ya uhakiki itakuaa rahisi, mimi ninashauri kwamba kila siku muwe mnahakiki vyeti vyilivyotumwa siku iliyopita, na sio kusubiri tarehe ya mwisho ya utumaji ndio muanze kuhakiki.

kama mtafanya hivyo inamaana kwamba uhakiki utaisha mapema (haitazidi tarehe 18/01/2017) na majina yatapelekwa wizara ya utumishi napema pia, kisha yapelekwe tamisemi ambao wao kazi yao ni ndogo sana.

kazi ya tamisemi ni kupachika majina kwenye sehemu walizoziandaa zenye uhitaji. hii ni kazi ndogo sana kwani nakumbuka mwaka juzi majina yalikosewa. waliweza kuapngua na kupanga upya kwa siku moja tu, tena majina yenyewe yalikua mengi sana wakiwemo walimu wa sanaa.

Kwa walimu wa sayansi tu ambao ni wachache sana, ninaaamini kazi ya kupachika majina kwenye sehemu zao walizoandaa zenye uhitaji, itachukua siku moja tu. ni matumaini yangu ajira zitangazwe mwishoni mwa mwezi huu, au mwanzoni kabisa mwa mwezi wa pili.

Ila kama lengo lenu ni kuzuia ajira, basi hata haya ninayopendekeza sasa nadhani yatakua hayana nafasi kwani hata zoezi hili la uhakiki litakua ni hewa.

Asanteni.
 
Wanaweza kamilisha mapema uhakiki lakini kutoa hizo ajira inawezekana ikachukua muda kama kauli ya "wakati wowote kuanzia sasa"
 
Wanaweza kamilisha mapema uhakiki lakini kutoa hizo ajira inawezekana ikachukua muda kama kauli ya "wakati wowote kuanzia sasa"
hapo watakua na lengo la kuzia ajira, na zoezi hili litakua kwa ajili tu ya kuzuia ajira.
 
Jinsi ambavyo naifahamu hii govt kwa kuleta siasa ktk kaz, wataanzisha kitu kipya ili waendelee kuzuia hizo ajira
 
Jinsi ambavyo naifahamu hii govt kwa kuleta siasa ktk kaz, wataanzisha kitu kipya ili waendelee kuzuia hizo ajira
ndio maana tunawasiwasi na huu uhakiki umeoanzishwa muda huu. wengine tunahisi umekuja kwa ajili ya kuzuia ajira. maana kama ungekua ni wa nia njema, ungefanyika mapema sana. tusubiri watudhihirishie wao kua, uhakiki waliouanzisha ulikua ni kwa ajili ya kuzuia ajira tu. na watatudhihirishia kukaa kimya mpaka mwezi wa pili ufike huku ajira hazijatoka. mbaya zaidi ukute wataoajiriwa ni elfumbili na kadhaa, means uhakiki huu part two, ulihakiki watu mia kadhaa tu
 
UNA MAWAZO MAZURI BUT SIDHANI KAMA WENZAKO WANAJARI HILO WATASUBIRI WAMALIZE KUTUMA NDIO WAANZE KUKAGUA
ajira zikikawia kutoka, basi tutaconfirm kua uhakiki uliofanyika ulikua hewa, ulikua ni kiinimacho ili dhamira yao isiyo nzuri kwa wanyonge ya kuendelea kuzuia ajira itimie.
 
kwa kuliona hili la uhaba wa walimu unavyoathiri hata ufaulu wa wanafunzi, nadhani imepelekea wakae kwa muda mrefu bila kutoa matokeo ya kidato cha pili, huku wakiwa wanajadili matokeo ya kidato cha pili 'either' wayaweke ktk mfumo wa zamani wa wastani ambao waziri wetu mpendwa anaupenda sana au wayaweke kwa divisheni ili kuficha watani wa alama F uliokithiri (lakini mfumo wa divisheni kwa 'form two' waziri wetu haupendi, kwani kutumika kwake hakujashirikisha wadau mbalimbali wa elimu na haujazoeleka kutumika 'form two'). kwa ktumia mfumo wa division kwa 'form two' wamepandisha ufaulu kwa kiwango cha juu, kwani aliyepata alama D mbili kafaulu vizuri. Tuwape hongera sana kwa kuondoa GPA iliyokua inawabeba wanafunzi, na kuweka DIVISION inayowabeba wanafunzi pia. ila tuwakumbu kuhusu kuhusu ajira za walimu, japo wao wanaona sio muhimu sana, kwani ufaulu utaongezwa na mfumo DIVISION ili kuficha athari za kutotoa ajiri za walimu.
 
matokeo kidato cha pili yametoka na masomo yalioongoza kwa kufeli ni sayansi yani inaanza physics inafata chemistry,pia na somo la b.maths....na shule haizna waalimu,pia serikali inataka wanafunz wote wasome sayansi wakati huohuo mwaka wa pili huu toka graguates wa mwaka 2015 na 2016 hawajaajiriwa na hao wanafunz ambao saiv wapo kidato cha 3 wanategemea kufanya mtihani kidato cha nne mwakani then serikali inategemea matokeo mazuri au inalaumu walimu na wanfunzi kufeli masomo yao,wanategemea nini na huku waalimu hao wanaohitajika mpaka leo hawajaajiriwa? tunaendelea kuua elimu,mana masom hayo wanafunzi hawafundishwi na wataendlea kufeli na hakutakuwa completion au kurejea ule muda ambapo wanafunzi hawakusoma au hawakuwa na waalimu katika baadhi ya masomo hayo.
 
Kwa mliotuma vyeti andaeni nauli za kuelekea katika vijiji mtakavyopangiwa mapema FEBRUARY mwaka huu, japo serikali ilishakanusha kutoa ajira mwezi FEBRUARY kanusho hilo litayeyuka kama lilivyoyeyuka kanusho la kutoajiri walimu wa Sanaa.
 
ndio maana nasema kua, kama wakiacha kutoa ajira mwishoni mwa mwezi huu, basi zoezi hili wanaloendesha litakua hewa. na wizara ya elimu itakua imejiingiza kwenye chuki hii kwa kuhusika kwake ktk jitihada ovu za kuzuia ajira za alimu wa kuhudumia wanyonge
 
ikiwa mwezi februari mwanzoni, basi tutaamini wizara ya elimu haikua na nia mbaya ya kuzuia ajira. vinginevyo wizara hiyo itaubeba malaba wa lawama, maana uhakiki huu wa mwezi huu ambao ajira zilipaswwa kutangazwa, hauleti picha nzuri. huu utakua ni uhakiki hewa wenye lengo baya kwa wanyonge
 
Aliesema Ajira ni Feb wakakanusha naona kabsa kuwa hii inaelekea kuwa ni ukweli, ila kama itapita Feb basi serikali imejpanga kuzuia ajira mpaka mwaka wa fedha 2017/2018!

Nakama lengo nikuvuta muda na kuzuia ajira hakika watalaaniwa!
 
ndio maana nasema kua, kama wakiacha kutoa ajira mwishoni mwa mwezi huu, basi zoezi hili wanaloendesha litakua hewa. na wizara ya elimu itakua imejiingiza kwenye chuki hii kwa kuhusika kwake ktk jitihada ovu za kuzuia ajira za alimu wa kuhudumia wanyonge
dah ase....waendlee tu kusubiri mkuu.
 
Matamko ya kinafiki, uhakiki walisema haitazd miez 2 je sahv miez mingap? Bado tunaamin maneno tu na matamko? Mi siamn kitu au mtu yeyote sahv maana siasa imekuwa chafu kuwahi ktokea!
 
Back
Top Bottom