Habari za majukumu wadau wa JF.
Uhakiki wa vyeti uliofanywa na serikali kwa watumishi wa umma miezi michache iliyopita umejaa sana dosari.
Licha ya uhakiki kutohusisha watunga sera/sheria wetu uhakiki huo haujawagusa kabisa waajiriwa katika sekta binafsi na wale waliojiajiri wenyewe. Hali hii inaleta maswali mengi yasiyo na majibu.
Hata hivyo kwa watumishi wa umma tuliohakikiwa wapo wengi walioingizwa katika makosa ambayo hawakustahili. Mathalani wapo walioorodheshwa kuwa wameghushi vyeti wakati wana vyeti halali. Wapo walioorodheshwa kuwa hawakukamilisha kupeleka vyeti (incomplete) wakati walikabidhi vyeti vyao vyote kwenye zoezi la uhakiki.
Cha kushangaza zaidi katika zoezi hilo kuna watumishi ambao wamehesabiwa zaidi ya mara moja kwasababu katika vyeti vyao kimoja kilianza na majina yao ya kwanza (first name) na vyeti vingine vilianza na majina ya pili(surname). Mathalani, sekondari alitumia PETER JOHN na cheti kinasomeka hivyo na alipokwenda chuo majina yake yakasomeka JOHN PETER na cheti kinasomeka hivyo,huyu amehesabiwa Kama ni watumishi wawili tofauti na Kila mahali ameandikiwa incomplete ila vyeti vyote ni halali na ni vyake.
Katika mazingira haya yamesabisha watumishi hao kupata taharuki na kupoteza muda mwingi kufuatilia namna ya kutatua matatizo hayo badala ya kufanya kazi. Tunaomba serikali ilione hili na kutatua changamoto hii bila kuwaathiri watumishi hao.