Uhakiki wa vyeti bado unaendelea?

Uhakiki wa vyeti bado unaendelea?

vidudi

Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
75
Reaction score
37
Wana JF,

Naomba kuuliza vipi zoezi la uhakiki linavyoendelea kufanyika hapa nchini lina matokeo gani? Kuna wafanyakazi hewa vipi hao wanachukuliwa?
Kuna wenye vyeti original lakini si vyao nao vipi wao hujulikana?
Vipi unafanyika uhakiki kwa watumishi wa sekta za ulinzi (JWTZ, polisi, na Magereza) afya (madaktari na manesi) na walimu (wa primary, secondary na vyuo)? Nini tofauti kati ya uhakiki wa idara hizo tatu tofauti ktk uhakiki huo?
Kipi cha kuzingatia wakati wa uhakiki unafanyika kwako?
Nini hatima ya watu ambao hawana vyeti vyao halisi ila wanavyo halisi lakini si vyao?

Naomba kupata maelekezo kwa wale waliowahi kufanyiwa uhakiki na wale wenye ufahamu wa kina juu ya zoezi hili na lini mwisho wake kwa ujumla.

NAWASILISHA.
 
Kama una vyeti feki usijaribu kwenda navyo wiki hii nimeambiwa na majiran zangu hapa wafanyakazi wenzao watatu mpka sasa wapo selo
Hivi kunatofauti gani kati ya vyeti feki na vile vya watu zaidi ya mmoja lakini ni OG?
 
Kama ni Vyeti Vyako na Orijino Usiwe na Hofu!
Uhakiki ni Makini na wa Unaofata Uangalizi Mkubwa!
Kukosa Baadhi ya Vyeti Hakukunyimi Fursa ya Kuhakikiwa!
Mathalani,Kuna Mtumishi Alipoteza Orijino Ya Cheti cha Kidato cha Nne,Ameaagizwa Aende Nyumbani Kwao Kahama Kwa Afisa Mtendaji wa Kata ili Asibitishwe,Kisha Aende Kituo cha Polisi Kupata Loss Report!
Punguza Khofu!
 
Back
Top Bottom