Ikiwa nitajibiwa kwa facts nitaridhika na kuona kuwa sasa JF inao washiriki ambao ni great thinkers haswa sio wale wa matusi na posho. JF hii inapaswa kuwa bora kuliko ilivyo sasa, na inaweza kuwa hivyo tu ikiwa watu wake wanafanya na kusema yale ambayo great thinkers wanatakiwa kuyasema na kuyafanya.Siku zote nimekuwa nikijiuliza huyu TandaleOne ni nani kumbe ni wewe! ok!
Hebu ngoja kwanza tukusanye taarifa halafu tutakujibu kwa facts maswali ambayo hujayapatia majibu mpaka sasa.
Tandaleone...........
Swali la msingi na lenye kufikirisha ni kwanini wahaini hao wanawalenga wanaCCM..? je inaweza kuwa watu hao wanamlengwa mwingine wa kisiasa ambao unakinzana na CCM hivyo kuifanyia CCM na Viongozi wake mambo haya..? Sitaki kuamini kuwa vurugu hizi zina unasaba wa aina yeyote na Siasa zetu hapa nchini bali najilazimisha kuamini kuwa vurugu hizi ni hujuma na uhaini unaofanywa na wahuni, wahaini ambao hawaitakii mema nchi yetu. Najilazimisha kuamini hivyo kutokana na maana halisi ya Siasa, ama harakati za siasa kuwa hazihafikiani na kinachofanyika mtwara, bali vitendo hivyo vinashabihiana na maana ya hujuma na uhaini kama ifuatavyo...
Kwani kama hoja ni gesi vipi vurugu zilenge katika mali, ofisi na uhai wa wanaCCM..?
We have a very serious and huge responsibilities to run the country. Maamuzi yetu yanafanywa kwa kuzingatia uhalisia wa mazingira yetu, siasa zetu na rasimali tulizonazo. Hakuna maamuzi kandamizi ama ya upendeleo ambayo CCM ama serikali yake yanaweza kuya-champion. Ni ajabu na ni muendelezo wa siasa chafu kudai serikali ya CCM inalenga kuitenga na kuionea kusini.
Makubaliano ya Pinda na wanamtwara yapo bayana tena yakiwa na viongozi wa kaya, viongozi wa kisiasa na hata wa kidini wa mtwara. Makubaliano hayo yanabainisha faida na mafanikio ambayo mtwara kama mkoa utanufaika nayo kutokana na miradi ya gesi, lakini hmakubaliano hayo hayakuwa yakikataza gesi kutoka mtwara na hata neno lenyewe kutoka linatrumika vibaya kwa maana kiasi cha gesi ambacho kitaendesha shughuli zakiuchumi za mtwara ni kubwa na inayokidhi haja kuliko hata itakayosafirishwa kwa ajili ya kufua umeme kwa ajili ya gridi ya Taifa.Ndugu yangu Tandale One, naungana nawe katika kuhuzunika kwa yale ambayo yametokea Mtwara. Hata hivyo, sioni mwingine yeyote ya kumlaumu au anayepaswa kufikwa na madhila haya zaidi ya CCM na viongozi wake. Hivi madai ya msingi ya wananchi wa Mtwara ni yepi? Na serikali imeyashughulikiaje?
Pinda alipokwenda Mtwara walifikia makubaliano ya kuiacha gesi mtwara. Iweje kipengele hicho kiingizwe kwenye bajeti ya wizara ya Nishati na Madini tena kwa mbwembwe?
Wananchi wa mtwara tumewaandaaje kisaikolojia katika hili? CCM isirudi kulilia huruma ya wananchi, hili wamelitaka kwa muda mrefu hili, sina shaka linatokea sasa. Wananchi wa Mtwara leo sio wale wa miaka ya " Wreath of Father Mayer"., this is a bit new generation.. Korosho imeshindwa kuwasaidia, bandari imeshndwa kuwasaidia, na gesi pia isiwasaidie???
Noo.,
CCM imepanda kiburi, wacha ivune Kaburi..
Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa habari naomba uniambie katika kata ya Madimba Mtwara kuja project kubwa 3 zinahusu nini? na wanachokidai watu wa Mtwara na lindi ni kipi hasa?
Watanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...
Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..
Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .
Ulimwengu mzima, mahali ambapo panavumbulika rasilimali fulani, watu wa pale lazima wafaidike kwanza na zaidi, ndio maeneo mengine ya nchi yapate. Wenyeji wa sehemu zenye mafuta wali resist sana baada ya kuona mafuta yanaenda na wao hawafaidiki. Ni wasukuma tu wa Mwanza ndio samaki zao zilichukuliwa,madini yao yakachukuliwa wanaangalia. Serekali ya CCM isipoliona hilo, hata hiyo gas hawataifaidi, wanaweza wakajenga bomba la mafuta likahujumiwa, nani atakuwa amefaidi? Waweke wazi mikataba ya gas kwanza kama wameshachukua 10% waseme
Akili yako fyatu na walio ku like ni fyatuWatanzania tumeze moto tu hata kama moto ...ukweli kwa hali iliyokuwa inaonekana na kilichotokea jana hapa Mtwara ukweli ulio wazi jambo hili lilipangwa na wako wanaoliongoza ila walikuwa wanangoja sababu ya kuanzia kutekeleza uhaini wao... Cha kushangaza kwa vurugu zinazolipuka wakati huo huo ni nadra kuyapata mabomu ya samaki na magobore, mapanga... Hili jambo tukatae tukubali lilipangwa na wako wanaofanya mipango hiyo.. Na walipanga wafanye hiki na hiki...
Binafsi nawapongeza jeshi la polisi kwa jitihada zao walizozitumi kunusuru hali isiendele kuwa mbaya ukweli hata mkiwabeza lakini ukweli uko wazi wamesaidia kwa kiwango kikubwa..Tukumbuke pia si wananchi wote wanapenda kinachoendelea hapa Mtwara. Naomba JWTZ endelee kuangalia hali inavyoendele ili amani iwepo msiingie kazi kutekeleza sheria za kijeshi mana khali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi mana jeshi 99% mafunzo yao ni kuua..
Shime watz turudi nyuma tuache ushabiki wa kisiasa tuliangalie hili jambo kiiundani zaidi na nyuma kuna nini tusiingizwe kichwa kichwa .
Hiyo ni Michadema tuuu, ipo Siku, NASEMA ipo sikuuuuu.
Leo asubuhi ya saa mbili na dakika 56 (08:56:16am) nimepokea ujumbe wa simu kutoka kwa mmoja wa Viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, ambae kwa cheo ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Ujumbe wenyewe ni huu ufuatao:
Ujumbe huu uliniongezea simanzi na majonzi niliyonayo juu ya maafa mbalimbali yaliyojitokeza katika vurugu za Mtwara jana. Simanzi hii ilitokana na kuona hali ya unyonge, woga na wasiwasi mkubwa walionao viongozi wenzangu wa Chama, wasiwasi huo hautokani na woga wa kitoto bali kutokana na hatari wanayoiona mbele yao ya kuwindwa, kushambuliwa na kufanyiwa hujuma na matendo mengine ya kudhuru mwili.
Swali la msingi na lenye kufikirisha ni kwanini wahaini hao wanawalenga wanaCCM..? je inaweza kuwa watu hao wanamlengwa mwingine wa kisiasa ambao unakinzana na CCM hivyo kuifanyia CCM na Viongozi wake mambo haya..? Sitaki kuamini kuwa vurugu hizi zina unasaba wa aina yeyote na Siasa zetu hapa nchini bali najilazimisha kuamini kuwa vurugu hizi ni hujuma na uhaini unaofanywa na wahuni, wahaini ambao hawaitakii mema nchi yetu. Najilazimisha kuamini hivyo kutokana na maana halisi ya Siasa, ama harakati za siasa kuwa hazihafikiani na kinachofanyika mtwara, bali vitendo hivyo vinashabihiana na maana ya hujuma na uhaini kama ifuatavyo.
Maana ya maneno mawili ya mwanzo ya yaani hujuma na uhaini yanafuatana kwa maana hujuma inaweza kutumika kama mkakati wa uhaini. Uhaini ni tendo la kusaliti nchi, serikali au mfadhili; uasi. Hujuma ni shambulio ama vamio: fisidi, kuvuruga ama kuharibu.
Maana ya kipengele cha tatu ambacho kimebeba maneno mawili harakati na siasa, ama siasa ina maana ni mfumo wa mawazo yaongozayo utawala wa serikali ya nchi tafsir nyingine ni utaratibu wa utekelezaji au uendeshaji wa jambo kwa kutumia busara na hekima ili kufikia lengo linalotarajiwa.,na maana ya neno la mwisho yaani harakati ni juhudi zinazoafanywa na watu kwa ajili ya kufikia lengo fulani, bidii, jitihada.
Katika tafsir hizo tatu, kinachoendelea mtwara hivi sasa tunakitoa kabisa katika maana halisi ya harakati za kisiasa, kwa kuwa maana ya harakati za kisiasa ni juhudi za kupanga utaratibu wa mfumo wa mawazo yaongozayo (ama yanayolenga kuongoza) utawala wa serikali ya nchi.
Kwa maana ya Hujuma kuwa ni shambulio, kuvuruga ama kuharibu ni sahihi kwa upande mmoja kuwa hiki ndicho kinachoendelea mtwara lakini kwa tafsir ya uhaini ndiyo hasa inayoelezea kinachoendelea Mtwara.
Ndio ni uhaini uliopangwa na kutekelezwa na watu wenye nia mbaya na nchi hii, wasio wazalendo na waliokosa utaifa. Wanaoendesha mkakati wa nchi kutotawalika, kwa kuibua hujuma mbalimbali dhidi ya serikali na chama kiendeshacho serikali hiyo yaani CCM.
Sio ajenda na hoja ya gesi, bali hoja hii imetumika kimbinu kuendesha mkakati huu wa kihaini ambao unawawinda wanaCCM, ofisi zao, mali zao pamoja na serikali yao. CCM ni chama cha siasa kinafanya siasa ya kuendesha nchi hii, vipo vyama vya upinzani navyo vinalenga kuelekea katika mlengwa huu wa kisiasa, lakini wakati mwingine vinapotoka na kuacha Siasa ama harakati za kisiasa na kujikuta wakifanya hujuma na vitendo vingine vya kihaini. Kwani kama hoja ni gesi vipi vurugu zilenge katika mali, ofisi na uhai wa wanaCCM..?