Salum Sanane
Member
- Apr 14, 2013
- 30
- 4
Wakati Katibu wa mkoa wa Tabora akikagua uhai wa chama wilayani Urambo,tarehe 12 mwezi huu alifika kata ya Kapilula.
Kabla ya kuhutubia wananchi alikutana kwanza na viongozi wa kata na matawi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida katibu huyo alishuhudia mwenyewa matawi yalivyokuwa yamekufa.Mfano tawi la Ulasa A katibu wa tawi alionyesha waziwazi siyo tu kutotekeleza,bali pia kutokujua kabisa wajibu wake.
Katibu Tawi huyo alionyesha wazi takwimu ya ziro katika kila kipengele cha wajibu wake kikatiba:
1. vikao vya kamati ya siasa 0
2. vikao vya halmashauri kuu 0
3. mikutano mikuu 0
4. vikao vya mabalozi 0
5. wanachama wapya 0
6. wanachama waliolipa ada 0
CCM hapo itegemee kushika mamlaka ya kijiji na vitongoji mwakani?
Siyo kazi ya katibu wa mkoa kuchukua hatua,yeye ameionyesha wilaya udhaifu huu, na tutegemee wilaya sasa kuwafukuza uongozi wale wote walioonyesha kukiangusha chama.
Natoa wito kwa wilaya ya Urambo kuanza na na tawi hili ambalo tayari limejidhihirisha.Vinginevyo CCM itegemee kuvuna mbigili.