Uhai wa Chama Cha Mapinduzi

Uhai wa Chama Cha Mapinduzi

Salum Sanane

Member
Joined
Apr 14, 2013
Posts
30
Reaction score
4
Wakati Katibu wa mkoa wa Tabora akikagua uhai wa chama wilayani Urambo,tarehe 12 mwezi huu alifika kata ya Kapilula.
Kabla ya kuhutubia wananchi alikutana kwanza na viongozi wa kata na matawi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida katibu huyo alishuhudia mwenyewa matawi yalivyokuwa yamekufa.Mfano tawi la Ulasa A katibu wa tawi alionyesha waziwazi siyo tu kutotekeleza,bali pia kutokujua kabisa wajibu wake.
Katibu Tawi huyo alionyesha wazi takwimu ya ziro katika kila kipengele cha wajibu wake kikatiba:
1. vikao vya kamati ya siasa 0
2. vikao vya halmashauri kuu 0
3. mikutano mikuu 0
4. vikao vya mabalozi 0
5. wanachama wapya 0
6. wanachama waliolipa ada 0
CCM hapo itegemee kushika mamlaka ya kijiji na vitongoji mwakani?
Siyo kazi ya katibu wa mkoa kuchukua hatua,yeye ameionyesha wilaya udhaifu huu, na tutegemee wilaya sasa kuwafukuza uongozi wale wote walioonyesha kukiangusha chama.
Natoa wito kwa wilaya ya Urambo kuanza na na tawi hili ambalo tayari limejidhihirisha.Vinginevyo CCM itegemee kuvuna mbigili.
 
CCM?.. Au unaota, mnapojifariji kwa vipropaganda vyenu kumbe huwa mnajiaminisha kwamba bado mpo...heri anayejijua kuwa amekufa maana huwa hajishughulishi tena
 
1380603_445857332202360_872830734_n.jpg
 
Pombe za usiku mbaya sana unadhani viongozi wa ccm wanaakili kama ya slaa akiona watu wanamtazama tofauti tu yeye anafukuza kazi pole na lile ulilonalo litakupa shida sana.
 
Wakati Katibu wa mkoa wa Tabora akikagua uhai wa chama wilayani Urambo,tarehe 12 mwezi huu alifika kata ya Kapilula.
Kabla ya kuhutubia wananchi alikutana kwanza na viongozi wa kata na matawi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida katibu huyo alishuhudia mwenyewa matawi yalivyokuwa yamekufa.Mfano tawi la Ulasa A katibu wa tawi alionyesha waziwazi siyo tu kutotekeleza,bali pia kutokujua kabisa wajibu wake.
Katibu Tawi huyo alionyesha wazi takwimu ya ziro katika kila kipengele cha wajibu wake kikatiba:
1. vikao vya kamati ya siasa 0
2. vikao vya halmashauri kuu 0
3. mikutano mikuu 0
4. vikao vya mabalozi 0
5. wanachama wapya 0
6. wanachama waliolipa ada 0
CCM hapo itegemee kushika mamlaka ya kijiji na vitongoji mwakani?
Siyo kazi ya katibu wa mkoa kuchukua hatua,yeye ameionyesha wilaya udhaifu huu, na tutegemee wilaya sasa kuwafukuza uongozi wale wote walioonyesha kukiangusha chama.
Natoa wito kwa wilaya ya Urambo kuanza na na tawi hili ambalo tayari limejidhihirisha.Vinginevyo CCM itegemee kuvuna mbigili.
Mkuu wewe ni mdogo wake na ben saanane?
tujuze ili tukae mbali na wewe.
 
tunakushuru kwa uzi wako wa kiuchunguzi , bali kichwa cha habari kiitwe KIFO CHA CCM .
 
Hivi jina Saanane huwa linamaanisha saa nane ya usiku au ya mchana?
 
Kila mtu hupimwa kwa kauli zake,na hapo utamjua pimbi ni nani.
Hoja si jina bali utekelezaji wa majukumu ya mtu.Labda nikiri tu kuwa umenisaidia kuelewa kuwa kuna watu ambao sio wana CCM wamejipachika ili kukiharibia chama muelekeo.
Viongozi wa CCM sasa chukueni hoja hii kama ushahidi na hivyo kuwaondoa madarakani wavurugaji wote waliojivisha jezi za CCM hali wao ni CHADEMA.
 
tunakushuru kwa uzi wako wa kiuchunguzi , bali kichwa cha habari kiitwe KIFO CHA CCM .

Hota yako naikubali kwa asilmia 100,wana CHADEMA sasa wamegundua mtindo wa kuingia CCM na kushika nyadhifa mbalimbali kwa lengo la kugeuza "UHAI WA CCM" kuwa "KIFO CHA CCM".
 
Wewe Salum Sanane una udugu na Ben Saanane?

Au ni majuha wawili tofauti ambae mmoja ni Sanane (what ever it means) na mwingine ni Saanane? (Two O'clock).
 
Last edited by a moderator:
ccm ilishakufa zamani.hata huku kijijini kwetu hakuna cha tawi wa shina lililo active,hakuna wanachama wapya,hakuna anayelipia ada,wote wanasubiri uchaguzi ufike kadi zao zilipiwe na wagombea au wanunuliwe kadi mpya na wagombea ili kuwapitisha katika kura za maoni.kiufupi nyakati za chaguzi ndio muda wa kuchuma TUNAKULA CCM TUNALALA CDM.mkakati wetu 2015 wakitugawia kadi za magamba tunachukua,pesa tunakula maana ni kodi zetu walizotuibia na tunatumia kadi hizo kupitisha mgombea dhaifu wa magamba ili tumfumue kirahisi kwenye uchaguzi.
 
Wewe mchache wa mawazo,angalia mvumo wa vyama.Wamekuwa wanapokezana kwa muhula wa kuitwa CHAMA KIKUU CHA UPINZANI.Awali walianza UMD,baada ya muda fulani wakaishiwa ikaingia NCCR.Baada ya mhula wao kupita CUF nao wakawa chama kikuu cha upinzan.Hatuwezi kushangaa kwa zamu hii ya wabovu CHADEMA,na mbinu zenu sasa zimeanza kubainika.Mtaendelea kupokezana hivyohivyo.
 
Back
Top Bottom