Uhaba wa mafuta ya petroli -Arusha

Thomas Odera

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
670
149
Wakuu nimezunguka karibia vituo vingi vya mafuta hapa Arusha muda mchana na kila nilipofika sikupata huduma ya mafuta aina ya petroli, lakini nikaja kupata hapa Manji's karibu na Metropole. Je, inawezekana ni mgomo au kuna uhaba wa mafuta hayo?.

Hofu yangu ni kuwa inawezekanaje mafuta yaishe kwenye vituo kwa wakati moja kama vile umeme wa Ngeleja unapokatika nchi nzima, naombeni ufafanuzi wenu maana si mara ya kwanza hali hii kutokea.

Iliwahi kunikuta Tanga mjini, ghafla mafuta ya petroli yaliisha vituo vyote na kituo kimoja tu cha BGP kule Sahare ndiyo walikuwa nayo.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom