Ugunduzi wa vifungashio badala ya plastic ni fursa yenye pesa nyingi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,273
Umeshawaza maisha bila vifungashio vya plastic kwa 100%. Kuachana na plastic ni wazo zuri lakini tachukua muda mrefu kutekelezeka.

Fikiria mfuko wa chips unaununua kutoka kwenye barafu, vifungashio visivyo vya plastic vinavyohimili barafu ni changamoto kwa watunza mazingira.

Wachina wamebuni mabakuli ya bamboo yanayohimili baridi lakini mifuniko yake ni plastic. Inawezekena pia mifuniko hiyo ni mkakati wa kumfahamisha mteja bidhaa iliyoko ndani. Faida ya matumizi ya mabakuli haya ni kuwa kiwango cha plastic kinachotumika ni kidogo.

Miti milaini kama minazi inaweza kutumika katika kutengeneza vifungashio. Wabunifu wadogo hasa vijana, wazi la kubuni vifungashio mbadala ni nafasi inayoweza kukutoa kimaisha.

Unaweza kutumia mitandao kuuza wazo lako.
 
Nadhani Tetra Pack ni mbadala kwa vifungashio hasa vimiminika vyenye kuhitaji baridi. Brown Paper iliyowekwa soft coated layer inahimili hali kwa uzuri kabisa.
 
Out of the topic unajua kuna pesa mtaani hatuioni, umeshawaza kuwa na duka la chakula barafu, uza maharage yaliyochemshwa 1/4, 1/2, kilo. Pia mihogo uliyomenywa pakiti she, 3,000.
Nimeona kariakoo wakaanga chips wananunua viazi vimemenywa na kupasuliwa tayari kwa ndoo. Na sehemu za masokoni unanunua nazi wana kukunia. Au kuku wanakuchinjia na kunyonyoa. Au nanasi wanalimenya kabisa.

Unapunguza kupeleka uchafu nyumbani. Tena hapa kwenye matunda wangeweza kuweka na namna ubebe jwisi kabisa. Vyote hivi ni fursa
 
Out of the topic unajua kuna pesa mtaani hatuioni, umeshawaza kuwa na duka la chakula barafu, uza maharage yaliyochemshwa 1/4, 1/2, kilo. Pia mihogo uliyomenywa pakiti sh, 3,000.
Always!

Tatizo uhakika wa soko na uhifadhi kuzuia kuharibika. Wengi hawana majokofu na uhakika wa kusambaza kwa muda mfupi.
 
Nimeona kariakoo wakaanga chips wananunua viazi vimemenywa na kupasuliwa tayari kwa ndoo. Na sehemu za masokoni unanunua nazi wana kukunia. Au kuku wanakuchinjia na kunyonyoa. Au nanasi wanalimenya kabisa. Unapunguza kupeleka uchafu nyumbani.
Tena hapa kwenye matunda wangeweza kuweka na namna ubebe jwisi kabisa. Vyote hivi ni fursa
Wachina matunda yote wanapack kwenye makopo, kuna makopo ya mafenesi, machenza, matunda damu, pears wewe unalofikiria. Nazi unanunua tui kwenye koop. Ukipika dakika 10 msosi uko tayari.

siyo kupika usubiri mkaa ushike uanze kukuna Nazi. Maharage na mihogo ni vyakula vinavyolika sana mwezi wa Ramadhani.
 
Always!

Tatizo uhakika wa soko na uhifadhi kuzuia kuharibika. Wengi hawana majokofu na uhakika wa kusambaza kwa muda mfupi.
Umeme pia si wa kuamini kan, fikiria tani ya maharage ikuozee kwenye freezer Tanesco wamekata siku tatu.
 
Wachina matunda yote wanapack kwenye makopo, kuna makopo ya mafenesi, machenza, matunda damu, pears wewe unalofikiria. Nazi unanunua tui kwenye koop. Ukipika dakika 10 msosi uko tayari.

siyo kupika usubiri mkaa ushike uanze kukuna Nazi. Maharage na mihogo ni vyakula vinavyolika sana mwezi wa Ramadhani.
Tatizo ni moja tuu. Vichwa vya wabongo ni ngumu sana kupokea wazo jipya. Wanataka wathibitishe kila hatua. Naelewa ulichosema maana kule wanauza mpaka kuku waliokaushwa.

Hata machungwa ya kukausha na mananasi utapata. Wanauza mpaka mboga ambazo wewe ukifika unapasha tuu mpaka nyanya na vitunguu na viungo washakuwekea ndani.
 
Out of the topic unajua kuna pesa mtaani hatuioni, umeshawaza kuwa na duka la chakula barafu, uza maharage yaliyochemshwa 1/4, 1/2, kilo. Pia mihogo uliyomenywa pakiti sh, 3,000.
😊
Comment nzuri hi😍
 
Umeme pia si wa kuamini kan, fikiria tani ya maharage ikuozee kwenye freezer Tanesco wamekata siku tatu.
Yes! Hili wazo lipo, watekelezaji wachache maana miundombinu sio wezeshi.

Labda tujuilize Mini Markets na Super Markets wenye uwezo kwa nini wasiingie na bidhaa zao zilizofungashwa au kuongezwa thamani?

Hii inafanyika vizuri na H&M (Clothing Store), Wendy's (Food) and co.
 
Back
Top Bottom