Ugumu zoezi la urejeshaji wa nauli za SGR

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2018
Posts
274
Reaction score
646
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaendelea na zoezi la urejeshaji wa nauli kwa abiria aliyeshindwa kusafiri Desemba 31, 2025 jioni na Januari 1- 2, 2025 kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu.

Hata hivyo zoezi hili limekumbwa na ugumu kufuatia baadhi ya abiria kukatiwa tiketi na watu wengine hivyo mawasiliano yao (simu ama email) kutokuwamo katika mfumo wetu wa tiketi hivyo kusababisha kikwazo cha mawasiliano baina ya pande zote hususani abiria aliyelipa na kusafiri. Ndugu abiria na mteja, Shirika linaomba radhi kwa changamoto iliyojitokeza.

Kwa mawasiliano zaidi juu ya suala hili, tafadhali wasiliana nasi kupitia nambari ya huduma kwa wateja 0800 110 042, WhatsApp 0738 594962 ama tutumie namba yako ya simu inbox (DM) kupitia Account yetu ya Instagram “tzrailways”

Huduma bora kwa wateja wetu ndiyo kipaumbele cha Shirika.

Ahsanteni.

Pia soma:
~
KERO - TRC mli-cancel safari yetu ya SGR ila kurudisha nauli imekuwa ngumu na hampokei simu!
~ TRC wafafanua kinachokwamisha urejeshaji nauli kwa abiria walioshindwa kusafiri Desemba 31, 2025 hadi Januari 2, 2026
 
Kuna watu wanakatiwa ticket itasumbuwa bado.
Kukatiwa ticket kvp labda
Je wanazungumzia kukatiwa ticket na agent wa shirika la Reli?
Au
Kukatiwa ticket na mtu wa karibu na msafiri kupitia simu ya mtu ambaye sio msafiri?
Kwasababu ninachoamini kama mtu atakatiwa ticket na mmojawapo wa niliowataja hapo juu lazima taarifa zinapokelewa Moja kwa Moja kwenye mifumo ya shirika sasa ugumu wa kurejesha nauri unatoka wapi?
 
1) Wamejuaje kama wamekatiwa ?

2) Warudishe hela kwa kutumia taarifa za hao hao maajenti waliotumwa kuwakatia tiketi abiria wengine, kwa sababu abiria waliwaamini wakawabidhi mpaka pesa wawakatie tiketi.. hivyo na wao wafanye kuwa amini hivyo hivyo kuwa watazirudisha hizo pesa kwa waliowatuma kuwakatia tiketi.

MBONA HAKUNA UGUMU WOWOTE.
 
Kivyovyote vile itakavyokuwa wao watudishe pesa kupitia taarifa za yule aliyekata tiketi..suala la kujua kuwa aliyekata anamkatia mtu mwingine na siyo kwa ajili yake waachane nalo.
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaendelea na zoezi la urejeshaji wa nauli kwa abiria aliyeshindwa kusafiri Desemba 31, 2025 jioni na Januari 1- 2, 2025 kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu.

Hata hivyo zoezi hili limekumbwa na ugumu kufuatia baadhi ya abiria kukatiwa tiketi na watu wengine hivyo mawasiliano yao (simu ama email) kutokuwamo katika mfumo wetu wa tiketi hivyo kusababisha kikwazo cha mawasiliano baina ya pande zote hususani abiria aliyelipa na kusafiri. Ndugu abiria na mteja, Shirika linaomba radhi kwa changamoto iliyojitokeza.

Kwa mawasiliano zaidi juu ya suala hili, tafadhali wasiliana nasi kupitia nambari ya huduma kwa wateja 0800 110 042, WhatsApp 0738 594962 ama tutumie namba yako ya simu inbox (DM) kupitia Account yetu ya Instagram “tzrailways”

Huduma bora kwa wateja wetu ndiyo kipaumbele cha Shirika.

Ahsanteni.
Mlinikoseshe deal nono sanaaa wakuu. Sema nini nime samaheee tu 🥹
 
1) Wamejuaje kama wamekatiwa ?

2) Warudishe hela kwa kutumia taarifa za hao hao maajenti waliotumwa kuwakatia tiketi abiria wengine, kwa sababu abiria waliwaamini wakawabidhi mpaka pesa wawakatie tiketi.. hivyo na wao wafanye kuwa amini hivyo hivyo kuwa watazirudisha hizo pesa kwa waliowatuma kuwakatia tiketi.

MBONA HAKUNA UGUMU WOWOTE.
Wanatafuta sababu za kukwepa kurudisha hizo nauli.
Ukiwasiliana nao wanataka uandike barua ya kuomba kurudishiwa. Hiyo nayo ni namna ya kudelay na mwishowe kutolipa kabisa.
Kukata ticket unakata bila barua, ila refund mpaka barua, si utopolo huo?
 
Back
Top Bottom