Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Sidhani kama Rais wa TanZania hapendi kutumia Kiswahili pindi anapokuwa na mgeni hapaTanzania, nafikiri tatizo kubwa liko kwenye matayarisho na sera za nchi!
Kwa mfano leo hii Raisi wa Vietnam kama Rais wa Tanzania angetumia Kiswahili ina maana ingebidi kwanza kuwe na mfumo ambao tayari ungetengenezwa kabla hata ya Rais kuja jinsi ya kutafsiri Kiswahili kwenda Kivietnam na hii siyo kazi rahisi sana, ilipaswa Wizara husika wajue kwamba Rais wa TZ atatumia Kiswahili kwenye maongezi yake na hivyo wawasiliane na Wavietnam khs hilo ili Wavietnam wajitayarishe jinsi ya kumtafsiria Rais wao ktk kiswahili kwenda Kivietnam lkn kwa kuwa hatuna huwo utaratibu nina uhakika Wavietnam waliuliza kabla hata Rais wao hajaja Rais wetu atatumia Lugha gani sisi tukawaambia Kiingereza hivyo wao wakajitayarisha kwa Kivietna na Kiingereza na kinyume chake!
Sasa basi kwa kuwa ni swala la kimfumo ni lazima mfumo wetu mzima ukubali na uamue kwamba rais wetu atatumia Kiswahili popote pale alipo na pia baada ya hapo tufanye maandalizi ya kufanikisha hilo!
Inawezekani ni uamuzi tu lkn huwezi tu kutegema kesho akija Rais wa labda Latvia ambaye ataongea Kilatvia basi na Magufuli naye aongee Kiswahili siyo raisi kihivyo ni lazima kwanza sisi tukubali na tubadilishe mfumo na inawezekana, sema tatizo letu ni UVIVU kwa maana itachukuwa kazi kidogo sasa Kiingereza ni ready made na ni rahisi kukitumia hasa kwenye tafsiri maana upatikana wa watafsiri ni kazi rahisi!
Ikumbukwe kwamba si ajabu hata Shahada ya Utafsiri nchini mwetu haipo, na hii ni kozi maalum watu wanasomea wanaitwa kiingereza mainterpreter sasa nchi nyingi zina mainterprter wa karibia lugha zote na hili watu husomea Chuo Kikuu kwa upande wa Wazungu na nchi nyingine ni rahisi kwa mfano kumpata mtafsiri wa ktk Kiswahili kwenda kwenye lugha yao lkn kwetu ndiyo ishu ni ngumu kuwapata Watafsiri kwa kifupi tuna mapungufu makubwa sana karibia kila eneo!