mulwanaka
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 5,262
- 12,835
#Habari:Ugumu wa maisha wafanya wakulima kwenda kinyume na ushauri wa JPM,mkoani Ruvuma
___________________________
Wakulima mkoani Ruvuma wameanza kuuza mahindi yao kwa bei ya chini kwa walanguzi kabla ya soko la serikali kupitia hifadhi ya taifa ya chakula (NFRA) kutokana na hali ngumu ya maisha.
----
Wakulima mkoani Ruvuma wameanza kuuza mahindi yao kwa bei ya chini kwa walanguzi kabla soko la serikali kupitia hifadhi ya taifa ya chakula (NFRA) kutokana na hali ngumu ya maisha.
Wakizungumza kwa niaba ya wananchi wao madiwani wamesema mazao ya wakulima ndio dhamana ya mkulima hivyo anapokuwa katika hali ngumu ya kimaisha anayauza kwa bei yoyote kwa walanguzi ambao wananufaika kwa mgongo wa mkulima.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameendelea kuwataka viongozi kuanzia ngazi ya vijiji kuwaelimisha wakulima kuuza mazao yao kwa bei nzuri na kujiwekea akiba ya chakula huku akisema kuwa mkoa wa Ruvuma una chakula cha kutosha.
Hivi karibuni akizungumza mjini Dodoma rais Dkt. John Magufuli amewataka wakulima nchini kutouza mazao yao kwa bei ya chini kwa walanguzi na kujiwekea akiba ya chakula.
Chanzo: ITV