Ugumu wa maisha umezidi kijijini kuliko mijini

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,015
2,000
#Habari:Ugumu wa maisha wafanya wakulima kwenda kinyume na ushauri wa JPM,mkoani Ruvuma
___________________________
Wakulima mkoani Ruvuma wameanza kuuza mahindi yao kwa bei ya chini kwa walanguzi kabla ya soko la serikali kupitia hifadhi ya taifa ya chakula (NFRA) kutokana na hali ngumu ya maisha.

----

Wakulima mkoani Ruvuma wameanza kuuza mahindi yao kwa bei ya chini kwa walanguzi kabla soko la serikali kupitia hifadhi ya taifa ya chakula (NFRA) kutokana na hali ngumu ya maisha.

Wakizungumza kwa niaba ya wananchi wao madiwani wamesema mazao ya wakulima ndio dhamana ya mkulima hivyo anapokuwa katika hali ngumu ya kimaisha anayauza kwa bei yoyote kwa walanguzi ambao wananufaika kwa mgongo wa mkulima.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameendelea kuwataka viongozi kuanzia ngazi ya vijiji kuwaelimisha wakulima kuuza mazao yao kwa bei nzuri na kujiwekea akiba ya chakula huku akisema kuwa mkoa wa Ruvuma una chakula cha kutosha.

Hivi karibuni akizungumza mjini Dodoma rais Dkt. John Magufuli amewataka wakulima nchini kutouza mazao yao kwa bei ya chini kwa walanguzi na kujiwekea akiba ya chakula.

Chanzo: ITV
 
Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,026
2,000
Sio tu wanauza kwa ajili ugumu wa maisha lakini Ruvuma wanalima mahindi kama zao la biashara kwa hiyo wanauza vile kulingana na mahitaji yako ya pesa yalivyo wanalima kwa wingi wakisubili serikali watahudumiaje familia zao
 
haha

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
749
1,000
Jamani vijijini watu wamechakaa acheni masihara daaaaah? Yaani watu uliowazidi umri wameisha kanisa
 
Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
53,464
2,000
Ndio maana mimi niliuliza ule ushauri anawapa wakulima wa nchi gani? Ni wakulima wachache sana wenye jeuri ya kukataa kumuuzia mlanguzi
 
Kitanga

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
311
250
Mara nyingine viongozi wa kisiasa wanaongea kama vile ni wageni katika nchi hii. Mkulima ambaye analima kilimo cha kawaida akishapata mavuno tu lazima auze ili kurejesha gharama kama vile pembejeo alizokopa au kuiwezesha familia yake kujikimu. Kwa hiyo, ni vigumu kumzuia kuuza mazo yake. Itakuwa rahisi kwa mkulima mabaye ni mfanyakazi pia maana anapata msahahara kila mwezi.
 
wolfpack

JF-Expert Member
Aug 6, 2013
662
500
Huku ukiona vitz unapata matumaini sasa mzee baba huko unaona tu baiskeli tena imechoka what do you expect mkali
 
Murashani GALACTICO

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
468
1,000
Upatikamaji was hiyo buku sasa
Kijijini ukifika zisome changamoto zifanye kuwa fursa na fursa ukiiona ichangamkie. Utapiga hela tuu. Ninekuja kijijini kufanya kazi ya umma. Nilihisi ninepewa adhabu kuja huku. Ila sasa ukitaka kunihamisha ni ngumu sana kunitoa kijijini. Ndugu wakija kutafuta maisha wengi wanakataa kutoka wanaanzisha biashara huku huku. Yawezekana kuna vijiji vinepigika ila sio hiki nachoishi.
 
Gustavo Gaviria

JF-Expert Member
Nov 19, 2018
582

Kijiji gani unaishi mkuu.

Nina idea ya kuchomoka niingie vijijini
 
Kashaija72

Senior Member
May 18, 2020
155
250
Kijijini ukifika zisome changamoto zifanye kuwa fursa na fursa ukiiona ichangamkie. Utapiga hela tuu. Ninekuja kijijini kufanya kazi ya umma. Nilihisi ninepewa adhabu kuja huku. Ila sasa ukitaka kunihamisha ni ngumu sana kunitoa kijijini. Ndugu wakija kutafuta maisha wengi wanakataa kutoka wanaanzisha biashara huku huku. Yawezekana kuna vijiji vinepigika ila sio hiki nachoishi.
Kuna Kijiji kimoja nilifika wanalima Sana mpunga. Hapo kila mfanyakazi akipelekwa hataki kuhamishwa.
 
Luhomano

Member
May 1, 2020
51
125
Hivi kwanini serikali wasiwatafutie wakulima masoko ya uhakika maana haiwezekana bei za pembejeo ziwe zinabadilika kwa kiwango kidogo kati ya mwaka na mwaka, kwa mfano mbolea 58000 hadi 60000 lakini gunia la mahindi debe sita utakuta ni 21000 Mara nyingine 60000. Kwahiyo angalau kungekuwa na uafadhali kwenye pembejeo then uzalishaji mkubwa kuliko gharama za uzalishaji kuwa mkubwa halafu bei mbovu huu utakuwa wizi kama wizi mwingine
 
dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
1,518
2,000
Kijijini ukifika zisome changamoto zifanye kuwa fursa na fursa ukiiona ichangamkie. Utapiga hela tuu. Ninekuja kijijini kufanya kazi ya umma. Nilihisi ninepewa adhabu kuja huku. Ila sasa ukitaka kunihamisha ni ngumu sana kunitoa kijijini. Ndugu wakija kutafuta maisha wengi wanakataa kutoka wanaanzisha biashara huku huku. Yawezekana kuna vijiji vinepigika ila sio hiki nachoishi.
Kwako we mgeni itakuwa ni rahisi isitoshe ni mtumishi uwezo wa kuwa na mtaji upo, Shida inakuja kwa wenyeji kuweza kutoboa ni mgumu sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom