Ugumu wa Maisha: Nchi inanyooshwa au kukosekana kwa ubunifu(creativity)?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Sidhani kama kuna mtu anapenda jinsi raia wake wanavyotaabika, sidhani kama kuna mtu ambaye hazitaki kura 2020, hakuna asiyependa ving'ora.

Wananchi wana hasira na ugumu wa maisha, sio watumishi wa umma, wakulima na wafugaji, wasomi na makundi mengine mengi ni vilio tuu.

Ni lazima tukubaliane kuwa kuna sehemu viongozi wetu wameteleza, kuna vitu vidogovidogo ambavyo hata awamu ya nne haikulazia macho ili kuhakikisha raia wananeemeka na taifa lao pamoja na mapungufu yake wakati huo. Mapungufu ya sasa yaweza kua ni mengi zaidi kuliko zamani.

Hili suala la kusema kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa sifa yake ni kujua kusoma na kuandika pia linachangia kiasi flani. Unafikiri kiongozi aliyefoji cheti ubunifu wa kuwakwamua raia wake na umasikini utatoka wapi? Kiongozi anayejua kusoma na kuandika tu ni muda gani atafikiria viwanda? Tunacheza sisi!

Yaani huwa nasema kuwa tungepata wakuu wa mikoa walao 20 mfano wa Fatma Taleki wa Shinyanga, Chiku Galawa wa Songwe, Antony Mtaka wa Simiyu na Agrey Mwanri waTabora basi taifa hili lingesonga mbele mno.
 
Kwani mawaziri na manaibu, wakuu wa mikoa/wilaya, makatibu na manaibu hawajui kusoma na kuandika?
Tafsiri ya kusoma na kuandika kwako ina maana gani?
 
Ugumu wa maisha ni changa moto. Viongozi wa kitaifa wana jukumu la kuweka misingi imara ya uchumu wa inchi.

Taifa linapokuwa na ziada katika hazina yake linakuwa na wajibu wa kurudisha ziada hiyo kwa wanainchi kwa njia mbali mbali. Tanzania haina ziada ya kutosha kufanya maisha ya kila mtanzania kuwa mazuri.

Tuko nyuma sana hasa kwenye nyanja ya elimu, viwanda, kilimo, miundo mbinu, afya n.k. Haya mambo makuu yanayotakiwa kufanywa na serikali yalitelekezwa kipindi fulani kwa sababu ya tanzania kutokuwa na mfumo wa iana moja ya uchumi.

Wakoloni walioitawala Tanganyika walikuwa na uchumi wa kibepari, tukabadili baada ya uhuru na kuwa na uchumi wa ujamaa. Baada ya mwalimu nyerere kutoka madarakani tukawa na uchumi ambao kimsingi ni wa kibepari.

Kuyumba huku kunaathiri sana maendeleo ya inchi na watu wake.

Inchi kama Kenya, Afrikan kusini na zinginezo hazikubadili mfumo wa uchumi wa inchi zao baada ya uhuru ndiyo maana ziko vizuri katika viwanda, kilimo, elimu, afya n.k.

Hatuna namna tutaendelea kuwa na maisha magumu tu kama hatutakuwa na mfumo moja wa uchumi.
 
Huku kusoma na kuandika kwa hawa watawala wetu sijui kutatufikisha wapi yarabi toba.Wengi hawana ubunifu hata chembe.Ee mwenyezi mungu okoa taifa hili linaloangamia.
 
Tatizo ni dereva wa Bulldozer kupakia binadamu kwenye Lori na kuanza kulikurupusha
 
Nchi inategemea anayeongoza yuko vipi,tizama budget ya maendeleo wizara ya ujenzi imepata asilimia 200 zaidi ya budget,hii inakuonyesha anaetawala ni mjuzi wa kitu gani,kilimo inepata asilimia 3 ya budget halali na wizara nyingi ni hivyo,lakini namwuuliza mheshimiwa kama maendeleo ni flyover,treni ya umeme na ndege,mbona ethiopia wanayo kabla yetu na wananchi wanakimbia nchi yao?
 
Tatizo ni muongoza msafara, amepewa kazi kwa kukurupushwa usingizini; sasa nchi inaenda sengemnege!!!
Eti viongozi wanasema waliamua kumkurupusha jamaa ili adhibiti mafuriko ya mamvi!!!!
Sasa watakosa kila kitu!!! 2020 is coming.
 
Nchi inategemea anayeongoza yuko vipi,tizama budget ya maendeleo wizara ya ujenzi imepata asilimia 200 zaidi ya budget,hii inakuonyesha anaetawala ni mjuzi wa kitu gani,kilimo inepata asilimia 3 ya budget halali na wizara nyingi ni hivyo,lakini namwuuliza mheshimiwa kama maendeleo ni flyover,treni ya umeme na ndege,mbona ethiopia wanayo kabla yetu na wananchi wanakimbia nchi yao?
Unazungumziwa wale wanaokutwa vichakani au kenye Malori huku Tanzania?

Na wana shirika kubwa sana la ndege Africa nzima.
 
mimi kwa mtazamo wangu sidhani kama kuna mfanya biashashara anaepata faida kama atafuata sheria hasa kulipa kodi zote kama zilivyopangwa na nchi hii, inawezekana muuza mahindi ya kuchoma barabarani akawa anapata faida kubwa kwa vile alipi kodi, wenye maujuzi ya maesabu watakubaliana na mimi
 
Back
Top Bottom