Ugumu au wepesi wa kutawala nchi hufuata haya

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Ni kawaida watu kuwa na mawazo yao juu ya serikali zao na kulinganisha mataifa yao kimaendeleo, kiutawala na kimahitaji na wengine uenda mbali kaona wao wanaweza kuifkisha mbali nchi zaidi kuliko waliyopo. Haya ni mawazo na mtu hazuiwi kuwa na fikra hizo, ila unapaswa kujua maeneo muhimu unayoweza kujifunza kuyazingatika katika kuwaza kwako na kama ni kiongozi au una ndoto za kuwa kiongozi basi ukayajua na kujifunza ukajua ugumu na wepesi wa kuongoza kijiji, wilaya, mkoa au nchi husika.

Ni maeneo haya:

Mfumo wa utawala na ukomo wake. Taifa lolote duniani, ugumu au wepesi wa kutawala eneo/nchi husika huweza kuonekana katika mfumo wa utawala, kama ni mfumo wa vyama vingi, ushindani unahitajika, ni lazima kwa namna yoyote ile kiongozi aliye madarakani lazima afanye vitu vyenye kuonekana kugusa maslahi ya watu. Tafakari, Serikali haina fedha ya kutosha kukidhi anayotaka kuyatenda kiongozi wa nchi, miaka ni michache ya utawala na vyanzo vya mapato vinasuasua na miradi ni ya gharama na ya muda mrefu. Miaka mi 4 au mi 5 kiutawala watu uiona ni mingi sana lakini kiutawala ni michache ukilinganisha na ukuaji wa uchumi wa nchi husika na mipango ya maendeleo itayokonga roho za watu na kuendeleza maendeleo ya nchi husika. Ikiwa ni utawala wa kijeshi jipange upinzani wa mtutu wakati wowote au kutumia dora muda wote ili kubaki madarakani.

Ukubwa wa nchi. Mtu analinganisha kiutendaji na kihuduma kama kujenga miundombinu ya barabara, maji, nishati na makazi nchi ya Uingereza na ya Congo ama Tanzania, ni vitu viwili tofauti, ukilinganisha ukuaji wake wa pato (kihistoria) la nchi na ukubwa wa nchi kuwafikia watu wote. Ukubwa wa nchi ni ukubwa wa majukumu, ukubwa wa nchi uhitaji fedha za kutosha kuunganisha usafirishaji, nishati, masoko, bidhaa, huduma za elimu na afya, uwekezaji, uvunaji wa rasilimali, rasilimali watu na malipo. Ikiwa nchi uchumi wake bado mdogo maendeleo ni mchakato sio chafya.

Idadi wa watu na utegemezi. Nchi inapokuwa na watu wengi, mahitaji ya kihuduma huwa ni mengi na gharama kuwafikia wote. Wepesi, huwa ni wingi wa watu lakini utegemezi wao kwa serikali uwe ni mchache katika ajira, kieneo( watumishi), elimu na afya (kiwango angalau hata 50%). Tafakari, mifumo ya ukusanyaji kodi na kutoa huduma fulani bila malipo, ikiwa mifumo hiyo ingeweza pia kuongezea nchi pato kwa kiwango kizuri tu, hapa utajifunza serikali nyingi za Afrika zinajitahidi sana kupunguza mzigo wa majukumu wa watu wake na kujitwisha kama katika elimu na afya, bado utoaji rudhuku katika bidhaa, malighafi, ongezeko la kodi, uhitaji wa ajira, wingi wa wafanya biashara wadogo na ustawi wa sekta binafsi.

Ukuaji wa teknolojia. Nchi kasi yake ya ukuaji kiuchumi, kihuduma na kijamii, teknolojia nayo ina sehemu yake, katika uvunaji wa rasilimali na uwepo wa wataalam. Ukopaji wa teknolojia na utegemezi wa uvunaji wa rasilimali kwa kiwango kikubwa, katika Taifa lolote inaonyesha bado kasi yake ya uchumi ni ndogo, sera za nchi kwenda kinyume na watu wawazavyo ni lazima. Serikali bora uwaza kwenda mbele kiteknolojia. Ujenzi wa miradi mikubwa ugharimu mno lakini ni kukimbizana na teknolojia na kujiimarisha kiuchumi pamoja na kuwawezesha wanachi kujenga teknolojia na uchumi wao. Wananchi uamini serikali ndiyo yenye kukuza teknolojia lakini ukweli watu ndio wenye kukuza teknolojia na ndio maana seriakli duniani zinafurahi kumpata mtu anayeanzisha kitu chenye tija. Kazi ya serikali ni kuweka sera na mazingira wezeshi.

Wakati wa sasa kiutawala. Nyakati zimebadilika, sasa watu wanatafsiri tofauti kwenye neno uzalendo, ulipaji kodi, watawala, uchumi, uwajibikaji, kujitoa na namna wanavyopokea maagizo na kutekeleza masuala mbali mbali ya kitaifa, vijiji nk. Kwa nchi za Afrika, wananchi wanatamani kupata starehe ya maisha kulipa uchungu wa mateso ya mkoloni, lakini wakati huo uchumi hauwaruhusu, serikali na watawala wa Afrika wanatupiana vijembe vya mikopo ni sumu lakini hawana fedha za kutosha na wananchi wanahitaji huduma na kwa wakati huo huo utawala uliopo sio wa kifalme ni wa uchaguzi, kwa kudunduliza ni ngumu. Unapozitizama nchi zilizopiga hatua kiuchumi kidunia kwa wakati ule (1500-1945) ni haki yao kwani dunia ulifunikwa na damu, uwizi, unyonyaji, utumwa, kujitoa kwa wengi,uvumilivu wa matumbo na mifuko ila kwa wakati huu mtu uona tija kwanza tumbo lake na mfuko wake.

Itikadi katika huduma za jamii. Serikali za afrika zina mizigo mikubwa ya Bima za Afya, huduma za Afya, huduma za elimu, soko la bidhaa na malighafi, Usululishaji wa migogoro ya ardhi, kijinsia na upokeaji wa wakimbizi, kupambana na umaskini na miikopo ya elimu. Serikali zinawekeza kwa nguvu sana kwa wananchi. Zipo huduma serikali ingeweza kufumbia macho lakini kwa uzalendo na utawala bora wanakomaa kuzibeba, Amerika kipindi cha Obama care na kipindi cha Trump juu ya huduma za Afya, hali haikuwa shwari. Ni wazi serikali za Afrika zina pata ugumu kuhakikisha fedha inapatikana kusimamia huduma za jamii na bado inakutana na ukubwa wa eneo, rushwa na wahujumu.

Mabadiliko ya hali nchi/ mazingira. Nchi zenye jangwa, wakati wa ukame, vimbunga, wadudu walao mazao nk. Hivi ufanya ugumu utokee katika kutawala, yako mambo lazima yanapotokea yagharimu serikali fedha na umakini kama njaa, mfumuko wa bei, vifo, nishati hafifu, maradhi ya mlipuko na kushuka kwa pato la nchi. Ikiwa wananchi hawana tafakuri juu ya haya ugumu lazima uwepo kwa utawala taifa lolote.

Pato la nchi na hitaji la nchi wakati huo. Mahitaji ya nchi uongezeka kwa kasi ila pato la nchi huweza kusimama au kukua kwa kusua sua, ugumu upo mahitaji hayasubiri. Lazima utawala husika upambane ili kufikia hitaji la nchi husika. Ndio maana mikopo haiepukiki bali la msingi ni mikopo hii ifanye yaliokusudia. Kuna msemo " raha nazitaka ila marejesho yananikondesha" yatakondesha Taifa lolote ikiwa pesa husika haijafanyiwa jambo lenye tija. Kubuni vyanzo vya ndani inawezekana na ufanywa lakini mafanikio yake sio ya haraka kuzidi mahitaji ya nchi na mengine huleta minong'ono kwa wananchi, ni kosa watu kulinganisha nchi zilizoendelea kiuchumi miaka ya 1750 na za 1960.

Ushindani kisiasa na utekelezaji wa ahadi. Hakuna jambo gumu la utawala kama ushindani. Uchaguzi unapoishi vyama vingine uendelea kupinga kila kitu kwa chama tawala na ikiwa lengo lao ni kushika dola tu na sio kuibeba umma iliyopo, kwani siasa ya mauaji, vitisho na machafuko hufanywa na wasio jali utu wa mtu. Matokea ya ushindani ndio ushindi wa uchaguzi awamu ijayo popote, bila fedha za kutekeleza ni sawa na kuchemsha maji na jiwe kuwapa tumai wenye jamaa.
Majanga( mazingira na afya ya mtu). Maradhi yanayosumbua, uchafuzi wa mazingira, ajali, mvua kutonyesha kwa muda mrefu. Hata ikiwa nchi imejipanga kukabiliana na majanga bado wao sio waonaji yanayokuja yakoje. Jifunze kupitia Covid, Black death, Tsunami, Matukio ya kigaidi na mfumo wa bei toka soko la dunia na migogoro ya kisiasa ya kimataifa. Hivi vimeathiri pakubwa nchi nyingi na vinaathiri pakubwa tawala na wananchi wanapopata changamoto hizi mzigo huu ni wa serikali. Serikali ndio mungu wa dunia, lawama zote ni yeye.

Uwajibikaji wa watumishi, wananchi na wateule. Ustawi wa starehe na nguvu ya nchi pia ni hii, iwapo pakiwa hafifu lazima serikali yoyote itapwaya. Uzalendo inatija kubwa katika kufanya nchi yoyote iwe nyepesi kutawalika. Utiifu, kufanya kazi kwa malengo ya umma na kukwepa uvunjifu wa sheria ni eneo tija.

Uhitaji wa fedha na matumizi sahihi ya fedha. Mkopo sio sumu katika nchi bali huwa ni sehemu ya kufanya ufike haraka unapotaka kufika, unapotumika vyema uleta tija kubwa kwa mataifa mbali mbali na ukweli uliopo mkopo unaweza kugeuza kuwa tajiri ama kukufirisi, kukithi mahitaji kwa wakati, kupata mtaji, kupunguza utegemezi, kutatua tatizo husika kwa muda sahihi. Wengi wanaamini vyanzo vya ndani vinakidhi lakini hawajui nchi zao husika zinaingiza kiasi gani, uhitaji ukoje na mfumo wa utawala unasukumaje kufanya hivyo. Ikiwa unatawala kwa miaka minne ama mitano na nchi haina fedha ila kiongozi anao mpango wa kupata fedha kidogo za awamu kwa vyanzo vya ndani ni sawa akikopa, uoga nao ni sumu ya kuthubutu. Ni ngumu kwa mzazi kukubali mtoto afe ikiwa tiba yake ipo japo fedha hana bali anapaswa kuikopa na arejeshe kwa sharti la kheri, atakopa tu.

Mitazamo juu ya uhuru wa nchi husika. Fikra juu ya neno uhuru uleta ugumu katika kutawala, wapo wanao amini uhuru ni kuishi kwa kuitegemea serikali, watu wanasahau kuwa uhuru una majukumu. Nchi nyingi zinakumbana na migogoro kwa watu kuona maisha wanayoishi viongozi ni ya anasa, mtu anahoji kwanini Mkuu wa nchi atumie gari aina ya V8 wakati anaweza kutumia Vitz akasafiri tu vizuri, kwanini wanalipwa mishahara mikubwa ikiwa huku kada zingine hakuna mishahara mikubwa. Na vyama vingine ubeba hizi fikra kuaminisha watu kuwa wataweza kuajiri watu wote wasio na ajira, kuhakikisha watu wanakula vizuri, kuwa na fedha na kupata mahitaji yote huku wakizidi kuhaidi kutoa na hudumu zingine bure. Wanasiasa wanapolisha umma fikra potovu juu ya uhuru na rasilimali zilizozopo na maisha ya starehe katika taifa husika nayo ni changamoto.

Kwenda na wakati. Ni ngumu wakati unabadilika alafu nchi haijapiga hatua kuelekea pale utawala unapotaka au jamii inapotaka. Muda unapoipanga serikali ya nchi yoyote wananchi hawaelewi, nayo ni moja ya jambo gumu ambalo kiongozi anapaswa kulikabiri. La sivyo ugumu wa kutawala Taifa hilo lazima uwepo. Iwe ni mfumo wa elimu, wa afya, usafirishaji, teknolojia, masoko, mifumo ya fedha, biashara, ustawi wa jamii, sheria, silaha, nishati, uwekezaji, mifumo ya kodi, muingiliano wa jamii nk.

Badiliko la dunia. Nchi yoyote haipo pekeake katika uso wa dunia, yapo mataifa yamezuia baadhi ya biashara, teknolojia na sheria. Lakini kumekuwepo na magendo na ukiukwaji wa kile walichokizuia. Serikali zimekumbwa na mfumo wa bei za bidhaa na huduma, angako la mapato ya nje na ndani, matumizi yasiotarajiwa kutokana na ugaidi kushamili katika mipaka au nchi jirani. Teknolojia imehama na hivyo na nchi husika kulazimika kuhama teknolojia husika kuboresha mawasiliano na utendaji. Kwahiyo utajifunza ugumu uliopo pale unapo tafakari taifa lako.

Fikra za kiongozi. Wewe kama kiongozi unamawazo gani, unamahusiano gani na wengine na nchi zingine. Mawazo yako ni binafsi au ya kijamii, unapokeaje maoni ya wengine, adui yako unapambana nae vipi, unataka ufike wapi baada ya ukomo wako, nini uwe umekikamilisha kwa wakati wako, unatumiaje nafasi yako kwa maslahi yako, kwa maslahi ya nchi na watu wanaofanya nawe kazi, ubunifu wako na utiifu wako na ukali wako. Msimamo wako ndio itikadi yako na fikra zako, siyo kila mtu atakubaliana na ulitakalo ama ulifanyalo.
Usalama wa kiongozi. Ikiwa mkuu wa nchi hayupo salama, anaweza kushambiliwa na wapinzani kwa nguvu ama silaha. Hili ni tatizo. Nchi yoyote kiongozi mkuu wa nchi ndio alama ya kwanza ya amani na utiifu katika vyomba vya dola.

Kwa mambo hayo machache utajifunza kuongoza nchi sio suala dogo kama wengi wanavyofikiri bali ni jambo kubwa linalohitaji kujitoa kweli na kukubali lawama, ukweli uliopo hata siku moja huwezi kumfurahisha kila mtu ni lazima kama kweli una ndoto ya kuwa kiongozi usimame katika yale yatayogusa maslahi ya wote. Maarifa ya uongozi yanapaswa kubaki kuwa ni maarifa ya watu wote na sio maarifa ya mtu mmoja.

Unapoanza kulaumu au kukosoa mfumo wa serikali yoyote duniani unapaswa kutambua vyema Historia ya taifa husika, mfumo wake wa utawala, idadi ya watu na ukubwa wa mipaka yake, mifumo ya kodi, rasilimali na uwezo wa uvunaji wa rasilimali hizo, rasilimali watu waliyopo katika nchi husika, makusanyo ya kodi na bajeti ya Taifa husika, mipango ya serikali husika, utegemezi na mgawanyo wa rasilimali, kuathiriwa kwake kiitikadi na mataifa ya nje, uzalishaji kwa wengine, ustawi wa watu wake na teknolojia iliyopo katika nchi husika.
#mmmuhumba#
#Siasa kwa maisha ya watu na uchumi endelevu
#Kiongozi mkuu anapotenda yalio bora hakika anastahili pongezi na kuombewa dua njema.
#imarika#
20221113_005152.jpg
 
Maandishi mengi yote utopolo.

Kwa maana yako tuigawanye nchi ziwe nchi nyigi ndogondogo ili tuendelee?

Wingi wa watu maana yake wingi wa nguvukazi na wingi wa kodi. Unataka watu wachache utapata wapi kodi na nguvu kazi?

Bila eneo kubwa utapata wapi ardhi ya kilimo, madini mbalimbali , hifadhi na mbuga za wanyama?
 
Maandishi mengi yote utopolo.

Kwa maana yako tuigawanye nchi ziwe nchi nyigi ndogondogo ili tuendelee?

Wingi wa watu maana yake wingi wa nguvukazi na wingi wa kodi. Unataka watu wachache utapata wapi kodi na nguvu kazi?

Bila eneo kubwa utapata wapi ardhi ya kilimo, madini mbalimbali , hifadhi na mbuga za wanyama?
Asante kwa mawazo. Maana yangu ni kuwa wingi wa watu ni faida ila taifa lolote likiwa na idadi kubwa ya watu ambao ni tegemezi hawajakuwa na uwezo wa kujitegemea ni ngumu nchi yoyote kutawalika ni lazima serikali ihakikishe inaweka mikakati kuwakwamua na ndio maana uhitaj kuhakikisha. (Tizama China na India kama watu wangekuwa tegemezi pasingetawalika na hapa nchini kwetu)

*utoaji wa elimu ya msingi kwa watu wake ili kupata rasilimali watu.
*kuziona fursa na kujitegemea kiuchumi mfano nchi nying zilizopata uhuru na kutokea mapinduzi moja wapo ukosefu wa ajira uliokidhiri, maslah mabovu ya watumish na hali ngumu ya maisha ya watu.
*miundombinu kuwezeshs kuvuna ardhi, mbuga, madini, samaki nk
KUHUSU ukubwa, taifa kubwa linahitaji rasilimali fedha za kutosha kutoa huduma, uwezi niambia leo una mtoto mmoja utamwekea bajeti sawa na mwenye watoto kumi.

Zipo nchi zilikuwa na ukubwa kama Ujerumani iliunganisha nchi zaidi ya mia tatu, Italia pia. Imebak historia.
Unadhani kwanini Tanzania inapambana kutafuta miradi, uwekezaji, utoaji wa elimu, huduma za afya, mikopo kwa wajasiriamali, punguzo la kodi, TASAF, MKUKUTA, nk ni kuwezesha jamii iweze kujijenga kiuchumi.
Kwahiyo ugumu au wepesi wa kutawala utegemea haya.
 
Sijasoma.

Andiko ni refu sana.

INAONYESHA umetoa maelezo meeeengiiiiiii sana.
ILA HOJA NI CHACHE..
Ungejaribu ku summarize Andiko lako limpe wepesi msomaji.

Weekend tunasoma vitabu. sio makala ndefu kiasi hiki.
 
Asante kwa mawazo. Maana yangu ni kuwa wingi wa watu ni faida ila taifa lolote likiwa na idadi kubwa ya watu ambao ni tegemezi hawajakuwa na uwezo wa kujitegemea ni ngumu nchi yoyote kutawalika ni lazima serikali ihakikishe inaweka mikakati kuwakwamua na ndio maana uhitaj kuhakikisha. (Tizama China na India kama watu wangekuwa tegemezi pasingetawalika na hapa nchini kwetu)
*utoaji wa elimu ya msingi kwa watu wake ili kupata rasilimali watu.
*kuziona fursa na kujitegemea kiuchumi mfano nchi nying zilizopata uhuru na kutokea mapinduzi moja wapo ukosefu wa ajira uliokidhiri, maslah mabovu ya watumish na hali ngumu ya maisha ya watu.
*miundombinu kuwezeshs kuvuna ardhi, mbuga, madini, samaki nk
KUHUSU ukubwa, taifa kubwa linahitaji rasilimali fedha za kutosha kutoa huduma, uwezi niambia leo una mtoto mmoja utamwekea bajeti sawa na mwenye watoto kumi.
Zipo nchi zilikuwa na ukubwa kama Ujerumani iliunganisha nchi zaidi ya mia tatu, Italia pia. Imebak historia.
Unadhani kwanini Tanzania inapambana kutafuta miradi, uwekezaji, utoaji wa elimu, huduma za afya, mikopo kwa wajasiriamali, punguzo la kodi, TASAF, MKUKUTA, nk ni kuwezesha jamii iweze kujijenga kiuchumi.
Kwahiyo ugumu au wepesi wa kutawala utegemea haya.
Kwa hili umesema sasa. Utegemezi ni mzigo si kwa taifa tu hata kaya pia.

Serikali imetengeneza watu wake wae tegemezi . Ni hatari.

Serikali itoe elimu isiyotegemea kuajiriwa serikalini.

Watu waandaliwe kujitegemea kwa kujiajiri.

Leo mtaani, mwalimu wa digrii anazidiwa maisha na kijana wa darsa la nne anayechomelea grili.

Tupambane tupate katiba mpya. Mawazo mazuri kama haya tutayasema hadharani siyo nyuma ya keyboard
 
Kwa hili umesema sasa. Utegemezi ni mzigo si kwa taifa tu hata kaya pia.

Serikali imetengeneza watu wake wae tegemezi . Ni hatari.

Serikali itoe elimu isiyotegemea kuajiriwa serikalini.

Watu waandaliwe kujitegemea kwa kujiajiri.

Leo mtaani, mwalimu wa digrii anazidiwa maisha na kijana wa darsa la nne anayechomelea grili.

Tupambane tupate katiba mpya. Mawazo mazuri kama haya tutayasema hadharani siyo nyuma ya keyboard
Kuna jitihada kubwa sana zinafanyika na zinaendelea kufanywa kuleta wepesi na maendeleo hapa nchini, upo utofauti mkubwa ulio wazi unaonekana na unastahili pongezi na penye kukosoa tukosoe izidi kuimarika.
Tatizo ni kuwa vyama vya kisiasa bado vina mifumo ya kizamani ya kujitafutia imani kwa umma na bado wanahitaj kujijenga , ikiwa kama ni timu ya mpira ukasema hebu kila chama kipange wachezaji kuanzia raisi mpaka na chini ni kizungumkuti.
Swali dogo la kutafakari:
*Kama vyama vina miongozo yao na wanaikiuka na kuvurugana wataweza kufuata hiyo katiba?

Kuna makala niliiona hapa JF imeuliza ni chama gani kinaweza kushika dola mbali ya chama tawala.

Soma na hii makala niliwahi kushauri pia vyama vya siasa nchini vifanye ili viwe shindani kiukweli.

 
Back
Top Bottom