Ugumu anaoupitia Harmonize ni kielelezo tosha kwanini sanaa yetu haikui. WCB inaua wasanii nje ya lable yao

ze jj

JF-Expert Member
Aug 20, 2012
485
571
Nimefatilia kwa undani mikiki anayopitia Konde Boy toka ajiengue WCB. Kiukweli hajashuka Kama tunavyolazimishwa tuamini. Kwanza official songs katoa UNO na KUSHOTO KULIA na zote zimefanya vyema you tube. Hainshtui na Hujanikomoa ni bonus track wakati anajiandaa kuachia album yake.


Inashangaza sana kuwa Nchi yenye watu million 50 tunataka msanii awe Diamond Platnumz tu. Wenzetu Nigeria, International Artist ni wengi kwa sababu wanaachiana nafasi. Huku Tz tunapambana kushushana yaani mpaka media za YouTube hazipost show za Harmonize ili tu akose mvuto. Wenzetu wamefanikiwa kwa kuachiana nafasi.

Sasa hivi wamemwachia nafasi BURNABO. Hata hapa watu watakavyojibu ni kwa kumkatisha tamaa Konde Boy.
 
Hii business dogo mambo ya kuachiana na kusibiliana ni ujamaa wa vijijini kila mtu apate faida yake kwa juhudi zake.

Kwani msanii ni huyo harmo tu!! Akisema aanze kuwasubiria wenzake atasubiri wangapi?
Acheni mawazo ya kijamaa ktk ubepari
 
Ujamaa umetulemaza sana aisee.

Hiyo nibiashara sio kusaidiana kila mtu apambane hili ni soko huria. Ni wapi kabaniwa kondeboy? Kati ya WCB na konde gang nani anabaniwa? Nani nyimbo zake vituo vingi hazichezwi?

Labda jicho lako halioni Mbali kuna management ya WCB na kuna management ya Konde gang kila management ifanye Kazi yake ya biashara sawasawa.

WCB na Konde gang sio vituo vya misaada ni biashara tena zenye ushindani. Sikwamba Nigeria wanaachiana hapana kila mtu anapambana mpaka atoboe na ushindani upo palepale Sema wenzetu wameshazoea ubepari Hakuna kulia kwenye business.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikua hujui?
Diamond kawahi kutoka nje halafu kafunga mlango..
siku akiacha mziki ndio mziki utakua mziki.
Ndo mana napend singeli haina ubinafsi, wimbo mzuri utakuweka kileleni sio jina
Mbona diamond kawasaidia wasanii wengi amempa connection shetta kufanya collabo na kcee, chege na run town, amemlipia video ya dully Sykes inde, kamsaidia dj ommy kumpa connection mpaka kumwezesha kufanya vizuri medani za kimataifa.Pia angekuwa ni mbinafsi Kama unavyosema harmo asingekuwa msanii wa kimataifa, Asingemtoa Rayvanny, Lavalava na mbosso
 
Back
Top Bottom