Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili.
Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'.
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'.

stomach_ulcers
Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'

SABABU ZA VIDONDA VYA TUMBO
Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu.
Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers'
Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo.
Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.
Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.
Chembe za urithi 'Genetics': Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.
Uvutaji sigara/tumbaku: Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta.
Matumizi ya pombe/vilevi: Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe.
Msongo wa mawazo 'Mental stress': Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda.
...Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain'
...Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.
Kushindwa kumeza vizuri chakula.
Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni.
Kujisikia vibaya baada ya kula.
Kupungua uzito.
Kukosa hamu ya kula.

DALILI HATARI
Kutapika damu.
Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito.
Kichefuchefu & kutapika.

JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:-

Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteja wake ni vidonda vya tumbo.

Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika :-

Kupima damu 'Blood test'

Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative'

Kupima pumzi 'Breath test'

Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'

Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi. Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'

Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray.

Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'.

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs'

Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni.

Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol.

Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka.

Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine.

Matibabu kwa njia za asili, zipo dawa mbali mbali unazoweza tumia zikiwa kwenye mfumo wa unga au kimiminika

Kwa ushauri na tiba kwa maradhi mbali mbali wasiliana nasi.
what's app /call
+255 655 821 550
Sulayman Sangida
ahsante sana
 
*SIRAAJUL MUNIYR HERBS MEDICINE*
*MSAGISAGI*
NI DAWA INAYOTIBU::-
VIDONDA VYA TUMBO
MAJERAHA/VIDONDA VYA KWENYE NGOZI.
*MATUMIZI*
KOROGA KIJIKO KIDOGO (CHA CHAI) KWA MAJI MOTO/MAZIWA/UJI KIKOMBE 1X3 SIKU 14.
KWA UPANDE WA MAJERAHA YA NJE NYUNYIZIA KUTWA MARA MBILI.

KWA USHAURI NA TIBA ZA MARADHI MBALIMBALI WASILIANA NASI.
+255 655 821 550
ABUU NU'UMAN - MAKUMBUSHO DAR
Axante
 
UHUSIANO KATI YA VIDONDA VYA TUMBO NA NGUVU ZA KIUME

Wanaume wengi wanaougua vidonda vya tumbo kwa muda mrefu hutokewa pia kuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwahiyo ikiwa mwanaume una tatizo la kushindwa kuhimili tendo la ndoa na unaumwa vidonda vya tumbo, basi cha kwanza utatakiwa ujitibu vidonda vya tumbo.

Hili linakuwa kweli hasa tukiziangalia baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo kama zifuatazo;

Baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo zinazopelekea pia upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na zifuatazo:

1. Kuchoka choka sana bila sababu maalum
2. Kuumwa mgongo au kiuno
3. Kizunguzungu
4. Kukosa usingizi
5. Kiungulia
6. Tumbo kujaa gesi
7. Tumbo kuwaka moto
8. Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
9. Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
10. Kusahahu sahau na
11. Hasira bila sababu.

Dalili au matatizo yote hayo hapo juu yanayompata mgonjwa wa vidonda vya tumbo ndizo ambazo kwa namna nyingine kama matokeo yake zinapelekea tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wengi.

Kwa ushaur na tiba za magonjwa mbalimbali wasiliana nami

+255 655 821 550
Sulayman Sangida
Naxhukuru xana kuuj
 
Habari dr. Polee na majukumu ya kazi yako! Mi n kijana mwenye umri below 30, ni miez miwili nasumbuliwa na vidonda vya tumbo na nimeenda kama hosptl kama mbili iv lakini nkitumia doz nakuwa afazar kama wk iv tena unakuta najickia maumivu ka moto unawaka tumboni apa maeneo ya chini ya chembe ya moyo so naitaji ushaur wako ni dawa gani ntumie ili niwe salama,ingawa masharti yote ya vyakula walivonambia nisile nimetii lakini bdo tatzo lipopalepale?
Njoo PM
 
PAPAI BICHI NI DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO (ulcers)

CHUKUA PAPAI BICHI KABISA NA ULIOSHE VIZURI.
USILIMENYE WALA KUONDOA MBEGU ZAKE.
BAADA YA KULIOSHA KIKAMILIFU, BILA KULIMENYA LIKATE KATE VIPANDE VDOGO VIDOGO.

WEKA VIPANDE HIVYO KWENYE CHOMBO SAFI, KWA MFANO JAGI.

WEKA MAJI SAFI HADI USAWA WA VIPANDE HIVYO ULIVYOKWISHA WEKA KWENYE CHOMBO CHAKO.

TUNZA MCHANGANYIKO HUO (VIPANDE VYA PAPAI VIKIWA VIMELOWEKWA KWENYE MAJI) KWA SIKU NNE. HESABU SIKU, KWA MFANO KAMA UMELOWEKA MCHANGANYIKO HUU JUMATATU, ANZA KUHESABU JUMANNE, JUMATANO, ALHAMISI NA IJUMAA ITAKUWA SIKU YA NNE.

SIKU HIYO YA NNE, MAJI YATAKUWA YAMEBADILIKA RANGI NA KUWA MEUPE, CHUJA VIZURI KUTENGANISHA MAJI NA VIPANDE VYA PAPAI NA KIMSINGI MAJI HAYA NDIO TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO.
DOZI

KUNYWA NUSU GLASI YA MAJI HAYA KILA SIKU ASUBUHI, MCHANA NA JIONI. HAUTASIKIA TENA MAUMIVU KWASABABU MAJI HAYA YANATIBU KABISA VIDONDA VYA TUMBO AMBAVYO VINAKUSABABISHIA MAUMIVU UNAYOYASIKIA.
UTAENDELEA KUNYWA KWA UTARATIBU HUO KWA WIKI KADHAA, HII INATEGEMEA UMEISHAATHIRIKA KWA KIASI GANI NA VIDONDA HIVI, HIVYO TUMIA DAWA HII HADI UTAKAPOPONA KABISA. HATA HIVYO NI MUHIMU KUPIMA ILI KUJUA KIASI CHA MAENDELEO UTACHOKUWA UMEFIKIA (RECOVERY)
 
Habarini za jioni ya pasaka ndugu wana jamvi.

Si mwandishi sana humu jamvini japo ni msomaji wa muda kidogo. Leo nimependa ku share jambo lilionipa msaada baada ya kuona watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na shida ya vidonda vya tumbo.

Binafsi niliumwa na vidonda vya tumbo kwa miaka mitatu Lakini nilielekezwa na jamaa niliyekutana naye. NILIEKEZWA BURE NAMI NATOA UFAHAMU HUO BURE.

Tafuta majani flani ntaatach hapa ya aina mbili nayo ambayo utayachuma na kuyatwanga yakiwa mabichi na kisha kuandaa maji ya uvuguvugu na kisha kuyachanganya na hiyo rojo na kisha chuja. Kikombe kimoja cha robo lita kwa siku 3. Nawe utapona kama nilivyopona.

Nina mwaka wa 4sasa toka nipone. So nina hakika na nisemalo. Majina ya hayo majani siyajui kwa majina yake ila picha zake ndio hizo hapo.

Wataalamu wa classification wanaweza saidia kutupa majina ya hayo majaniView attachment 1078498View attachment 1078499
Ninaweza kuunga mkono hili,kuna mtoto wa ndugu yangu alishikwa na vidonda vya tumbo vikali sana mpaka ikawa hawezi kuingiza kitu tumboni,tulihangaika sana mahospitalini Dar bila dawa kupatikana,ila alienda Moshi akapewa dawa ya majani unachanganya na maji,alipona wiki hiyo hiyo na mzima mpaka leo,kibaya zaidi mama wa huyo kijana ambaye ndio alikuwa naye bega kwa bega kumuuguza alifariki miaka kama 3 iliopita,Sasa sijui yule babu kama bado yuko hai,maana ni karibu miaka 10 imepita...
 
sawa sawa inaonekana kwako maumivu si makubwa
Mkuu mimi maumivu yamepungua sana tu ndiomaana sijatumia huo mkojo, nilirudi hospital wakanipa dawa inaitwa pantonix, ni nzuri sana nahisi napona
 

Attachments

  • IMG_20190515_054401.jpg
    IMG_20190515_054401.jpg
    73 KB · Views: 118
Mkuu mimi maumivu yamepungua sana tu ndiomaana sijatumia huo mkojo, nilirudi hospital wakanipa dawa inaitwa pantonix, ni nzuri sana nahisi napona
walikupima wakakuandikia ama na vyako Vina mda gani mkuu? hiyo dawa bei gani?
 
Ninaweza kuunga mkono hili,kuna mtoto wa ndugu yangu alishikwa na vidonda vya tumbo vikali sana mpaka ikawa hawezi kuingiza kitu tumboni,tulihangaika sana mahospitalini Dar bila dawa kupatikana,ila alienda Moshi akapewa dawa ya majani unachanganya na maji,alipona wiki hiyo hiyo na mzima mpaka leo,kibaya zaidi mama wa huyo kijana ambaye ndio alikuwa naye bega kwa bega kumuuguza alifariki miaka kama 3 iliopita,Sasa sijui yule babu kama bado yuko hai,maana ni karibu miaka 10 imepita...
Mimi mchagga hayo majani yanaitwaje mkuu
 
walikupima wakakuandikia ama na vyako Vina mda gani mkuu? hiyo dawa bei gani?
Walinipima ndio walisema kuna michubuko tumboni, nilitumia bima kwahiyo sijui bei take.lla kuna siku nilitaka kununua dukani nilikuta vidonge 30 ni elfu 30. Vidonda vyangu vimenitesa kwa miaka 4 sasa
 
Back
Top Bottom