Ugonjwa wa kuhara damu (Coccidiosis) kwa kuku

farmersdesk

Senior Member
May 26, 2012
164
120
UGONJWA WA KUHARA DAM
(Coccidiosis) KWA KUKU:
Na Dr Khalfan 0752367114
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea aina ya Protozoa na hushambulia kuku wote wakubwa na
wadogo ila huathiri zaidi kuku wadogo. _
*Jinsi unavyoambukiza* :
Kula chakula chenye kinyesi au maji yenye vimelea vya ugonjwa huu.

*Dalili* :
Kuharisha kinyesi kilichochanganyika na
damu au kinyesi chenye rangi ya ugoro,
Kuku kudhoofu na kupungua uzito.
Kuku kuzubaa na kushusha mabawa kama
kavaa koti.
Kuku kujitenga na wengine.
Kupoteza hamu ya kula.

*Tiba* :
Dawa aina ya Amprolium na ni vizuri ikichanganywa na doxycol au oxyfam20% dawa hizi huchanganywa kwenye maji na
kupewa kuku kwa siku 5 hadi 7.
*Kinga* :
Vifaranga wakifikia umri wa siku saba (7) wapewe Amprolium kwa siku tatu (3) mfululizo, hata
kama dalili za ugonjwa hazijajitokeza.
Tenganisha vifaranga na kuku wakubwa
Kuku wagonjwa watengwe na kupewa tiba mara moja
Wapo chakula kuku wako chenye mchanganyiko wa Ridocox au vigostart.
Zingatia usafi wa banda na vyombo vya chakula.
 
Je kifaranga anaweza kuzaliwa na vimelea vya ugonjwa huu? kama hivyo ndivyo mfugaji atumie njia gani kutibu?
 
Hapana kifaranga hakiwezi kuzaliwa na maambukizi
Let say, kama kuku alikuwa na ugonjwa huu je vimelea haviwezi kuwa ndani ya yai linaloanguliwa na kisha kuathiri kifaranga kitakachozaliwa?
 
Let say, kama kuku alikuwa na ugonjwa huu je vimelea haviwezi kuwa ndani ya yai linaloanguliwa na kisha kuathiri kifaranga kitakachozaliwa?
Hapana hakiwezi mkuu, kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kusambaa kwa mtindo huo ila sio coccidiosis
 
Kwani huu ugonjwa unatibika na amprolium pekee au nitangazo la biashara hili?
 
Kwani huu ugonjwa unatibika na amprolium pekee au nitangazo la biashara hili?
nilisoma pahala, wanasema pia unaweza tumia Agracox, dawa yenye Surpher ama Limoxin sasa wataalam waje hapa watudadavulie
 
Hapana hakiwezi mkuu, kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kusambaa kwa mtindo huo ila sio coccidiosis
noted; kwa hiyo unataka kuniaminisha kwamba kifaranga hakiwezi kurithi ugonjwa wowote aliokuwa nao mama yake wakati anataga lile yai?
 
noted; kwa hiyo unataka kuniaminisha kwamba kifaranga hakiwezi kurithi ugonjwa wowote aliokuwa nao mama yake wakati anataga lile yai?
Sina maana ugonjwa wowote, nasemea coccidiosis...! Japokuwa kuna magonjwa mengine ambayo kumpata kifaranga kupitia mayai mfano, Newcastle, pullorum, aspergillosis, lymphoid leukosis, marek's

Kwa hiyo jibu hapo ni hapana, kifaranga hakiwezi kupata ugonjwa wa coccidiosis kupitia yai
 
nilisoma pahala, wanasema pia unaweza tumia Agracox, dawa yenye Surpher ama Limoxin sasa wataalam waje hapa watudadavulie
Vifaranga vyanngu vinakufa kila siku, kuku hawaongezeki na madawa natumia lkn huwa wanavaa koti tu
 
Vifaranga vyanngu vinakufa kila siku, kuku hawaongezeki na madawa natumia lkn huwa wanavaa koti tu
Kuvaa koti ni dalili ya ugonjwa huu; ila hata mimi sijui uhusiano wa cocidiosis na salmonella; ngoja watufafanulie zaidi
 
Kwani huu ugonjwa unatibika na amprolium pekee au nitangazo la biashara hili?
Hapana sio biashara ispokuwa ndio dawa iliyozoeleka na wengi na pia ina matokeo chanya sana kwenye kutibu huo ugonjwa

ila kuna dawa kadhaa ambazo zinaweza pia kutibu na best kabisa ni ambazo zina contain Sulphur kama vile sulphonamides, sulfamethazine, sulfaquinoxaline, sodium sulfachloropyrazine monohydrate
 
Uko sahihi mkuu
 
Kuvaa koti ni dalili ya ugonjwa huu; ila hata mimi sijui uhusiano wa cocidiosis na salmonella; ngoja watufafanulie zaidi
Coccidiosis husababiswa na protozoa ,na salmonellosis (typhoid) husababiswa na bacteria aina ya salmonella.maranyingi magonjwa haya unaweza kuya tofautisha kwa dalili zake japo kua yote huambatana na kuahara.lakini muonekano wa miharo ni tofauti .coccidiosis kinyesi chake hua kimechanganyika na dam au ugoro.lakin salmonella kuku huharisha kiyesi kama chokaa.
 
wana umri gani? umetumia dawa zipi?
Wanakufa tu wakianza kuingia wiki ya 3-4 hivi, baada ya hapo hakuna kinachobakia.. Wanataga upya ni mwendo huo huo
Hadi unakata tamaa nipo nakula mayai tu sasa

Dawa ni hizi ninazoshauriwa sioni manufaa
76ea49fa70159c015fb86a9577ac238b.jpg
 
ha ha ha, so Mzee umeamua kula mayai siyo...

Mkuu hizi naona ni antibiotics plus vitamin's - hebu jaribu kutumia Limoxin kwa muda wa siku tano - packet wanauza Tshs 8500 approx.
 
ha ha ha, so Mzee umeamua kula mayai siyo...

Mkuu hizi naona ni antibiotics plus vitamin's - hebu jaribu kutumia Limoxin kwa muda wa siku tano - packet wanauza Tshs 8500 approx.
Wacha nijaribu, nimepoteza vifaranga vingi sana.. Ngekua tajiri sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom