Ugonjwa wa kuhara damu (Coccidiosis) kwa kuku

Ok. Wana umri gani kwa sasa? Na mama yao ana hali gani anaoensha kuumwa? Je mama yao ana utaratibu wa kuharibu mayai mengi, yani mayai vinza?
Wana siku kama 4/5 ivi,
Mama mzima wa afya haumwi na kaangua watatu kati ya mayai7
 
Wana siku kama 4/5 ivi,
Mama mzima wa afya haumwi na kaangua watatu kati ya mayai7
Ok. Sasa hapo tatizo lipo kwa mama ambae ndie mwenye ugonjwa ila kwakuwa hauna athari kubwa kwa kuku wakubwa ndomana yeye anaonekana mzima, na vifaranga vinapata maambukizi kupitia mayai

Ugonjwa ambao naweza kuhisia ni PULLORUM ndio ambao unafanana na hayo majibu machache uliyotoa, nasema kuhisia kwakuwa sijafanya uchunguzi wa mzoga ili kupata uhakika wa ninachosema

Sasa huo ugonjwa waga tunatibu dalili tu kwa maana kuku alieugua waga anabaki na bacteria na kuwa carrier hivo atakuwa anaambukiza tu kuku wazima na hatimae ugonjwa hautokuja kuisha milele hapo kwako,

Ushauri, chinja kuku wako au wauze na uchome mizoga, vyombo vyao, maranda kama waga unatumia, upumzike kwa muda kufuga ili bacteria wafe, na ukitaka kufuga tena ukanunue kuku ambao wanatoka kwenye chanzo ambacho hakina maradhi

ila kama utaamua kuendelea na huo ugonjwa basi wape dawa hii furazolidone. Kanunue watakupa maelekezo ya kuitumia na vifaranga wako hawatakufa ila wataendelea kuwa na vimelea vya huo ugonjwa na kuambukiza wengine wazima. Asante
 
View attachment 681392 View attachment 681392 View attachment 681391 Mkuu songoros FUSO ivan don habari zenu!!

Msaada, ninae kuku huyo yeye akitotoa vitoto vinakua design hii

• manyoya hayana afya membamba
•sehem za chini kama yamenyonyoka hadi ngozi inaonekana
Kama uonavyo pichani. Shida inaweza kuwa ni nini? Maana ni mara ya pili anatoa ivyo
Baada tu ya kutotolewa uliwaanzishia dawa ipi? Wanaonekana na dalali za ugonjwa huu anaoongelea hapa; ingawa wataalam humu wanasema kifaranga h!kiwezi kurithi ugonjwa toka yai kwa mzazi; wanadai kifaranga kitakuwa kimepata maambukizi hapo hapo bandani kwako.
 
Nimejaribu kuwapa hii ya binadamu mkuu, amoxyln kama sijakosea.. kwajili yamafua sijawapa nyingine. Zaidi mama zao niliwapa chanjo ile inayowekwa kwa friji kwanza
 
Baada tu ya kutotolewa uliwaanzishia dawa ipi? Wanaonekana na dalali za ugonjwa huu anaoongelea hapa; ingawa wataalam humu wanasema kifaranga h!kiwezi kurithi ugonjwa toka yai kwa mzazi; wanadai kifaranga kitakuwa kimepata maambukizi hapo hapo bandani kwako.
Samahani mkuu mbona unaongea kama vile unapingana na tuliosema kuwa kifaranga hakiwezi kuzaliwa na ugonjwa? kama wewe unafahamu kuwa hilo jambo linawezekana tujuze tu mkuu ili tuwe updated maana hii ni science hatuwezi kubishana kama vile siasa endapo ushahidi upo
 
sipingani na sayansi na tafiti ila mfugaji anapata mazingira yanayomfanya akose jibu sahihi; mfugaji kafuata taratibu zote za usafi; katumia kila kitu kinachotakiwa kwa kifaranga cha siku moja yet vinapukutika. Hapa ndipo mfugaji anahitaji kupata jibu sahihi vinginevyo anaweza kukata tamaa.

Ndiyo maana nikauliza kifaranga kinaweza kurithi parasites toka kwa kuku mzazi mwenye infection?

Jibu niliambiwa uwezekano ni mdogo sana na kama upo si kwa magonjwa hatarishi kama huu tunaoongelea hapa:

Sasa basi mfugaji apewe jibu sahihi kwa nini vifaranga 50 to 60% wapukutike ndani ya wiki mbili?
 
Nakupata mkuu, kuhusu kutoa jibu la uhakika jf sio rahisi ndugu yangu, kitu ambacho huyo mkulima anatakiwa kufanya ni kutoa kuku 1 kwa ajili ya wengine na bwana mifugo afanye uchunguzi hapo ndio jibu la uhakika litapatikana kuwa ni ugonjwa gani ambao unashambulia shamba lake

Na pia nimeona hakuna sehemu ambayo mkulima mwenye zile picha ameelezea kuhusu kufanya usafi wa mabanda na vifaa, na kuwapa chanjo zote kuku wake ispokuwa wewe ndio umemuongelea kitu ambacho inawezekana hafanyi

Kuhusu kifaranga kuzaliwa na parasites/bacteria/virus nishasema huko nyuma kuwa inawezekana ila kwa baadhi ya magonjwa na nakumbuka pia nilitaja machache, ila hiyo Coccidiosis haiwezekani ila nashangaa bado unarudia kitu kile kile

Nahisi kuwa wewe kuna kitu unajua au unahisi unajua ila hutaki kufunguka na unabaki na internal conflict hebu jaribu kuongea kile unachokiamini kitasaidia na wengine kuliko kukaa nacho moyoni bila faida yoyote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom