Magu
Senior Member
- Jun 13, 2011
- 156
- 56
Mwenzenu nafuga mbwa wawili nyumbani kwangu ambao nawapenda sana na ninawahudumia kwa chakula na mahitaji mengine kama malazi na matibabu. Leo nimekuwa na kazi ya kuwaogesha kwa dawa mimi mwenyewe, ila bahati mbaya mmoja wao mdogo wakati namuogesha alinikang'ata jino ktk mkono wangu, je naweza kuwa ameniambukiza ugonjwa wa kichaa cha mbwa au ugojwa mwengine wowote unaoambukizwa na mbwa? Katika kusoma niliwahi ona wataalamu wakidai kuwa si kila kuumwa na mbwa unaweza ambukizwa (Not every dog bites can infect rabies), naombeni ushauri wenu wanaJF