Ugonjwa wa dengue wazidi kuwa tishio, idadi yaongezeka kwa kasi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa na Naibu wake

Wizara ya Afya imesema idadi ya wagonjwa waliothibitika kuwa na homa ya dengue imefikia 3,495 hadi kufikia Juni Mosi 2019.

Takwimu hizo zimetajwa ikiwa ni siku nne tangu idadi ya waliothibitika kufikia watu 2,971 kutoka Januari 1 hadi kufikia Mei 29, 2019.

Akitoa takwimu hizo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kati ya wagonjwa hao 3,495 waliogundulika baada ya kupimwa 3,333 na vifo vitatu ni kutoka katika jiji la Dar es Salaam.

“Kati ya watu waliopimwa waliogundulika kuwa na virusi au walikwishapata homa ya dengue 3,333 ni kutoka Dar es Salaam, 135 jijini Tanga, 19 kutoka Pwani, 6 Morogoro, Singida mmoja na Kilimanjaro pia mmoja.”

“Takwimu za ugonjwa huu kutoka Januari hadi Juni 2019 ni kama ifuatavyo, Januari kulikuwa na wagonjwa 56, Februari 82, Machi 159, Aprili 678 na vifo viwili, Mei 2,485 na kifo kimoja,” amesema Ummy Mwalimu.

Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy ameagiza kila nyumba na mtaa kuhakikisha maofisa afya wa wanafuatilia upuliziaji dawa hizo, huku akitoa angalizo la kuwepo kwa dawa feki ambazo hazisaidii kuangamiza mazalia hayo, hivyo akaelekeza wapuliziaji wahakikiwe ili mwananchi ajue wanaotambulika na manispaa husika.

“Lazima tuweke mazingira yetu safi na salama, niseme tu ugonjwa wa homa ya dengue si mpya na unaathiri nchi nyingi, jumla ya watu milioni 390 huugua ugonjwa huu nchini na vifo ni 40,000 pekee, lakini Malaria watu milioni 216 wanaugua kila mwaka ila vifo ni 450,000 hivyo bado malaria ni tishio,” amesema.
 
Isiwe siasa wafanye kweli,huu ungonjwa ni hatari sana
 
Back
Top Bottom