Ugonjwa usiojulikana wawaua watu zaidi Liberia

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Watu wawili zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa usiojulikana ambao uliwaambukiza watu waliohudhuria mazishi mapema wiki hii katika kaunti ya Sinoe nchini Liberia kusini mashariki mwa mji mkuu Monrovia.

Vifo hivyo vinafikisha idadi ya watu waliofariki kuwa 11.

Watu watano kwa sasa wametengwa na wengine wanne wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu.

Mamlaka hata hivyo zinasema kuwa si mlipuko mwingine wa Ebola.

Uchunguzi bado haujaonyesha chanzo cha ugonjwa huo usiojulikana lakini wizara ya afya ina mpango wa kupeleka sampuli za damu katika mahabara za ngambo ikiwemo Marekani.

Maafisa wamewashauri watu kuchukua tahadhari zilizochukuliwa wakati wa mlipuko wa Ebola ikiwemo kuosha mikono.

Chanzo: BBC Swahili
 
Watu wanatengeneza biological weapons wanakuja kuzijaribia Africa.

Nchi zetu zinatakiwa kuimarisha usalama zaidi hasa mipakani na wanapokuja wazungu wakaguliwe haswa.
 
Haya magonjwa ni man made!!! Mungu awalaani hao wanaosababisha majanga haya!
 
Back
Top Bottom