Ebola yaua zaidi ya watu mia tano nchini DRC

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,366
2,000
Wizara ya Afya: Waliokufa kwa Ebola DRC wamepindukia 500

Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kwa maradhi ya Ebola tangu yaibuke tena hivi karibuni nchini humo imepindukia 500.

Taarifa ya Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kwa maradhi ya Ebola imefikia 502 huku mpango wa chanjo dhidi ya maradhi hayo ukiokoa maisha ya maelfu ya watu katika nchi hiyo.
Oly Ilunga Kalenga, Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema kuwa, kwa mara ya kwanza mpango wa chanjo ya Ebola umezuia vifo vya watu 76,425.
Mlipuko mpya wa maradhi ya Ebola ulitokea Agosti mwaka jana katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambao unapakana na Uganda na Rwanda.

Chanjo ya Ebola imekuwa na mafanikio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Kutokana na kwamba wimbi la hivi sasa la ugonjwa wa Ebola limetokea katika maeneo ya mpakani, nchi zinazopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nazo zimeamua kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.

Hadi kufikia tarehe 27 Novemba 2018, kulikuwa kumeripotiwa kesi 422 za Ebola, 375 kati ya hizo zikiwa zimethibitishwa na 47 ni za kudhaniwa. Hadi tarehe hiyo, watu 242 walisharipotiwa kufariki dunia huko Kivu Kaskazini na Ituri. Mripuko mkubwa zaidi wa ugonjwa wa Ebola ulitokea baina ya Disemba 2013 na Aprili 2016 na kuua zaidi ya watu 11,000 katika nchi za magharibi mwa Afrika za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Wizara ya Afya: Waliokufa kwa Ebola DRC wamepindukia 500
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom