Haujasahaulika mkuu. Unaitwa Plague. Unasababishwa na bacteria anaitwa
Yersinia pestis. Unaenezwa na viroboto (fleas) vinavyokaa katika mwili wa panya. Plague ni ugonjwa wa panya. Binadamu anaupata baada ya kuumwa na kiroboto kilicho na bacteria. Kiroboto anapata bacteria kutoka kwa panya mwenye plague. Kwa hiyo plague mara nyingi ni zoonotic. Zoonotic ni ugonjwa wa wanyama ambao unaweza kumpata binaadamu pia.
Panya wahusika wakubwa wanaitwa
Rattus rattus na
Rattus norvegicus. Haya ni majina ya kisayansi. Viroboto vinavyohusika zaidi ni aina ya
Xenopsylla cheopis.
Plague unaweza ukajitokeza kama
- Ugonjwa wa mapafu (pneumonic plague): unaua sana na haraka
- Ugonjwa wa tezi (bubonic plague)
- Ugonjwa wa ngozi (pestis minor)
Ugonjwa huu si mgeni. Uliwahi kuua robo ya wakaazi wa Ulaya kwenye karnne ya 15.
Kwa Tanzania, ugonjwa huu hulipuka mara kwa mara huko Lushoto.
Ni ugonjwa hatari sana kwa sababu huua sana na haraka, ingawa kuna matibabu. Baadhi ya dawa aina ya antibiotics zinaweza kutibu.
Kwa kifupi huu ndiyo ugonjwa wa tauni (plague)
Ukitaka kuujua zaidi, google 'plague'