Ugonjwa pacha wa Ukimwi waibuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa pacha wa Ukimwi waibuka

Discussion in 'JF Doctor' started by nngu007, Sep 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 12 September 2012 19:50[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]Florence Majani
  WAKATI wanasayansi wakiwa wanakaribia kukamilisha utafiti wa kuwezesha kupata tiba ya Ukimwi, ugonjwa mpya ambao unafanana kwa karibu kabisa na huo, umeibuka.

  Adult-Onsets Immunal Deficiency (AOI) umeripotiwa kuibuka katika nchi za Ulaya na kusambaa kwa kasi duniani.

  Kuibuka kwa ugonjwa huo, kumesababisha hofu mpya katika nchi za Ulaya na Bara la Asia ambako wagonjwa wengi zaidi wameonekana kuathiriwa na ugonjwa huo.

  Ugonjwa huu umegunduliwa na Dk Sarah Browne wa Taasisi ya Mzio na Magonjwa ya Kuambukiza ya nchini Marekani (NIAID) ambaye aliongoza timu ya wanasayansi walioendesha utafiti husika.

  Dk Browne alisema tofauti na Ukimwi, ugonjwa huo hauambukizwi kwa ngono wala njia ambazo Ukimwi unaenezwa, ila unadhoofisha kinga za mwili kama ambavyo virusi vya HIV vinafanya.

  Dk Browne katika majibu yake kwa gazeti hili alisema utafiti uliofanywa katika nchi za Taiwan na Thailand, umebaini kuwa watu wazima wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 50 ndio waliogundulika na kuathiriwa zaidi na ugonjwa huu.

  “Watu hao hawakuwa na virusi vya Ukimwi na CD4 zao, (chembe hai nyeupe ambazo huupa mwili kinga ya magonjwa) zilikuwa sawa,” alisema na kuongeza:

  “Bado hatujahakikisha kama ugonjwa huu mpya umewakumba watu wa Bara la Afrika, ingawa upo uwezekano kuwa wapo wengi wenye ugonjwa huu hasa kesi nyingi zinazofananishwa na kifua kikuu au Ukimwi,” alisema Dk Browne.

  Jambo jingine linalochagiza utata katika ugonjwa huo mpya ni kuwa dalili zake ziligundulika kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea.

  Dk Browne alisema mtu hazaliwi na maradhi hayo, bali huyapata ukubwani.

  Vilevile, timu ya wanasayansi hao ilieleza kuwa dalili za ugonjwa huo ambazo zinafanana kwa asilimia kubwa na dalili za Ukimwi hazikuonekana kwa ndugu wengine wa familia ya mgonjwa jambo ambalo linathibitisha kuwa ugonjwa huo si wa kurithi.

  “Mwili kwa kawaida, unazalisha kemikali ambazo zinafanya kazi ya kupigana na vimelea vya magonjwa kila vinapojitokeza, lakini watu wenye maradhi haya, miili yao inazalisha vimelea ambavyo vinabadilisha mfumo wa mwili wa kupigana na maradhi,” alisema Dk Browne
  Watafiti hao mpaka sasa bado hawajajua sababu za ugonjwa huo na wanaendelea kukuna vichwa ili kubaini kiini chake.

  “Bado hatujajua nini kinasababisha ugonjwa huu, lakini tulichokijua ni kuwa watu wanaougua maradhi haya hupata maradhi kama yale yanayoambatana na Ukimwi yaani pneumonia (ugonjwa wa mapafu), TB, au fangasi,” alisema Dk Browne.

  Jarida la Tiba la nchini Uingereza (New England Journal of Medicine) linasema kuwa ugonjwa huo ulibainika kwa mara ya kwanza 2004 Mashariki mwa Bara la Asia.
  Timu hiyo ya wanasayansi ilifanya utafiti kwa watu 204 ambao hawajaathirika na VVU, utafiti ambao ulichukua kipindi cha miezi sita.

  Watafiti hao walitathmini damu za watu hao kwa kutumia kemikali ambazo ziliuwezesha mwili kujikinga na magonjwa, lakini iligundulika kuwa miili ya baadhi yao inazalisha kemikali ambazo zinazuia mwili kujikinga na maradhi.
  “Wakati HIV inashambulia na kuharibu seli za mwili yaani kinga ya mwili dhidi ya maradhi, ugonjwa huo mpya hauathiri seli, lakini mwili unashindwa kutoa ‘amri’ ya kupambana na maradhi,” alisema.

  Alisema mwili wa mgonjwa hushindwa kupigana na maradhi hayo mara baada ya kemikali za kawaida kuzuiwa zisipigane na hapo ndipo mwili huanza kushambuliwa na fangasi, kifua, homa na maradhi mengine nyemelezi.
  “Ni kama kamanda wa polisi ambaye anashindwa kutoa amri kwa askari wake warushe risasi kwa maadui. Katika hali hiyo, polisi (ambao ndiyo seli) wataendelea kusimama wakati maadui wakishambulia,” alisema.

  Shirika la Habari la Marekani (APA) linaelezea kuwapo kwa tukio la hivi karibuni ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 62, raia wa Vietnam, alibainika kuwa na ugonjwa huo.

  Mwanamke huyo alianza kuugua homa mfululizo na kifua kikuu ambapo daktari wake alimtibu bila mafanikio, hadi alipopewa rufaa ya kwenda Taasisi ya Taifa ya Afya (NIH), Marekani na kugundulika na ugonjwa huo.

  Maradhi hayo yamesababisha mwanamke huyo kupungua uzito kutoka kilo 41 hadi 30 na bado anatibiwa kwa zaidi ya mwaka katika kituo hicho cha afya.

  Jarida la Promed la nchini Marekani linasema kuwa madaktari katika kituo cha NIH ambapo mwanamke huyo amelazwa wanaendelea kumpa tiba mbalimbali ikiwamo dawa za saratani ambazo zinadaiwa kuzuia vimelea vinavyosababisha maradhi mwilini.

  Hata hivyo, Dk Browne alisema changamoto kubwa ni kujua nini kinasababisha maradhi hayo.

  Kauli za madaktari nchini

  Akizungumzia kuhusu ugonjwa huo mpya, daktari wa patholojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Innocent Mosha, alisema hana taarifa yoyote kuhusu ugonjwa huo mpya, lakini alisema mwili kukosa kinga ni jambo linaloweza kutokea wakati wowote hasa kwa watu wanaotumia baadhi ya dawa.

  “Kwa mfano mtu anayetumia dawa zenye kitu kiitwacho steroid, zinashusha kinga, hata mionzi kwa wagonjwa wa saratani, lakini kinachosababisha zaidi ni HIV,” alisema Dk Mosha.

  Alisema kwa vyovyote hakuna tishio kubwa juu ya ugonjwa huo kwa sababu hauambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama ilivyo kwa VVU.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wananchi; msijirushe rushe ndugu yw VVU amezaliwa; Jipendeni kwanza kabla hamjapenda hao wa Mitaani
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Tofauti na VVU, hii haiambukizwi kwa ngono. Nadhani ni auto-immune disease imekuwa in a reverse form. Badala ya ku-trigger immunity system kuushambulia mwili bila sababu, hii inazima trigger ya kushambulia maradhi.

  Hadi kiama kije, tutashika adabu manake ukimwi wenyewe unatutoa jasho hadi leo! Duh!
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Interesting ... ! Some kind of shadow playing with scientist eh?
   
 5. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Hii inafaa zaidi kule JF Doctors, huku imepotea njia
   
 6. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  sijaelewa hapa tu!!
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  LOVE YOUR LIFE FIRST before you go out and LOVE the ONE NIGHT STAND TRASHES...
   
 8. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Sayansi hizi ngoja tusubiri tu hadi kiama tunaona magonjwa kibao
   
 9. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,506
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  yeeeesu na maria kwa hiyo timu imeongezeka na mpira bado uleule
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  King'asti,

  Loh! Kuna kazi hapa, .. "ni auto-immune disease imekuwa in a reverse form" ... kwa hiyo what is the basic different in molecular level with AIDS? ... Maana personally kuna kitu kingine nakiona hapa! Yaani chukulia mtu immunity yake ikawa ime kuwa compromised kama ulivyosema alafu akashambuliwa na HIV ... how would one differentiate between the two syndromes?
   
 11. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  okey...so inahusianaje na huu ugonjwa mpya?
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Wazee wa molecular biology ndo mna kazi hapo! Mtoa mada kahusisha na hiv prevention ila hatujamuelewa maana yake. Hii ni worst case scenario!
  Kama una hii problem manake ni kuwa hata dalili za magonjwa hupati (manake hata homa kwako hamna wala sores, as a result ya mapambano kati ya immunity system na ugonjwa). Sasa hata dalili za hiv hatutaziona! Kuhusu kutofautisha, clinical diagnosis tu ndo itahusika. So mgonjwa atahitaji kupimwa say mapafu kujua kama ana pneumonia ama TB manake hatakuwa na dalili yoyote. Sie wenye vipimo vya kubip ndo kwisha habari yake. Manake unakuwa kama nyumba isiyo na mlango, wakiingia au kutoka hata hujui!
  Ni kifo moja kwa moja bila mswalie mtume aisee! Kazi imeanza upya!
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Bagah, msome Azimio Jipya na mimi hapo juu.
  Ukiwa na huu ugonjwa, kila kitu kitakuua manake mwili unakuwa unazima alert system. So hutajua una malaria, amoeba, wala nini. Ukiwa na tatizo tumboni, mwili unastuliwa na kuhara ni kama njia ya kusafisha. Same as ukiwa na TB unakohoa kama njia ya kujaribu ku-clear mapafu na wewe unastuka. Halikadhalika ukiwa na infection kwenye kizazi, extra discharge unapata kama alert ya mapema mwili ukijaribu kuondoa tatizo. Sasa hii kitu inaondoa huu uwezo kabisa. Pata picha ukiwa na hiv, ambayo ujanja wake ni kuiwahi na mapemaa kabla haijakutenda. Inakuwa kwishnei bab G, juma juma dedeeh!
   
 14. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,303
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  hizi dizaini tofauti tofauti,huko tunaelekea nahisi kutatokea ugonjwa ambao ukiupata unashambulia magonjwa mengine,au itatokea mtu inabidi uugue ugonjwa flani ili uwe mzima, tehe tehe,,,,
   
Loading...