Ugonjwa huu umenimalizia tikiti nifanye nini kuepuka nao

IMG_20171214_141940.jpg

Hivyo ndivyo tikiti inavyokuwa
 
aiseee mkuu hapo tikiti lilikosa maji pindi ulipoanza napengine angalia mahali hapo je kuna wadudu wanashambulia kwa chini
 
Unalimia kwa sehem gan nikupe ushauri

mkuu hata mimi hilo tatizo limenikumba, kwanza nililima wakati wa masika yakawa yanaoza upande mmoja, nikadhani yamezidiwa maji. Ila nikalima baada ya masika lakini tatizo likawa hilohilo. Ila nilichogundua hayo matikiti ya hybrid ndio yenye shida, lakini yale meusi sikuona yakipta tatizo hilo. Naomba ushauri huo pia unikute na mimi.
 
Pole sana mkuu, huo ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu aitwaye kwa jina la kienyeji "dondoa".

Mdudu huyo hutoboa matunda yakiwa machanga na ana sumu ambapo akishatoboa hukojolea hiyo sumu na kusababisha tunda lioze kwenye sehemu iliyotobolewa au kuozesha tunda zima.

Kama halikuoza lote, litaoza sehemu iliyotobolewa na hiyo sehemu husinyaa na sehemu zingine huendelea kukua hivyo tunda huwa na mkunjo flani.

Wadudu hawa huishi kwenye miti hususani mikuyu, miembe nk.

Wadudu hawa ni waharibifu sana kwenye matunda hivyo dawa za sumu kali na zenye harufu huwakimbiza shambani mfano Selecrone ni dawa mojawapo unapaka kwenye pamba au vipande vya godoro na kusimika shambani kila mahali.

Pia kuna mitego ya kuwanasa ambayo hutundikwa at least mitego 6 kwa ekari moja na kila mtego ni shs 5000.

Hiyo mitego ipo kama chocolate inawa attract hao wadudu wanapoingia tu hukutana na sumu na kufa hapo hapo.

Wauzaji wa hiyo mitego nawafahamu waliopo Arusha.

Pole sana mkuu
 
Mkuu asante kwa ushauri
 
mkuu hata mimi hilo tatizo limenikumba, kwanza nililima wakati wa masika yakawa yanaoza upande mmoja, nikadhani yamezidiwa maji. Ila nikalima baada ya masika lakini tatizo likawa hilohilo. Ila nilichogundua hayo matikiti ya hybrid ndio yenye shida, lakini yale meusi sikuona yakipta tatizo hilo. Naomba ushauri huo pia unikute na mimi.
Pole mkuu yaani ni hasara sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom