****Ugonjwa hatari wa Nguruwe ****

emgoa

Member
Jun 23, 2012
11
1
Guys huu ugonjwa wa Nguruwe unaua banda zima kwa siku moja nini kinga? Ukishatokea inabidi ufanyeje kurudi kwenye game? Wale Vitoto vinavyobaki vinafaa kuendelea kufugwa au vinakuwa tayari navyo vinamaambukizi? ?
 
Guys huu ugonjwa wa Nguruwe unaua banda zima kwa siku moja nini kinga? Ukishatokea inabidi ufanyeje kurudi kwenye game? Wale Vitoto vinavyobaki vinafaa kuendelea kufugwa au vinakuwa tayari navyo vinamaambukizi? ?
Hapo ni kuzika tu wote na kusafisha banda kwa dawa,ugonjwa hauna kinga wala tiba.
 
Watoto kama hawajaambukizwa wahamishie sehemu nyingine uliyoiandaa kwa kuifanyia usafi wa madawa. Harakisha okoa kizazi hicho, pesa hiyo ujue! hii hali ikipita utauza bei juu
 
Japokuwa hujaeleza dalili za ugonjwa lakini nahisi ni African Swine Fever.
Ugojwa huu hauna tiba wala chanjo,unaua nguruwe wengi kwa wakati mmoja.
Ili kuokoa nguruwe wengine fanya yafuatayo:
Tafuta dawa iitwayo V-RID kwenye maduka ya dawa.
Ukipata changanya mls 4 au 5 za dawa kwa maji ya lita moja.
Wanyweshe nguruwe mls 2 za mchanganyiko huo kwa kila nguruwe (tumia syringe kuwanywesha)
Dawa iliyobaki wanyunyizie kwa pampu mwilini kisha nyunyizia kwenye banda wanalokaa.
Ukifanya hivyo unaweza kuwaokoa.
 
Hello..... Karibuni Sana Katika group linalohusu ufugaji wa nguruwe

Karibu Sana wewe mtaalamu wa mifugo, mfugaji, mnunuzi, pamoja na Wale wenye kiu ya kujifunza zaidi kuhusu ufugaji huu wenye tija na kipato cha uhakika.....

Click link ifuatayo kujiunga......

Zingatia kujitambulisha pindi tu uingiapo katika group hili
ZINGATIA KUJITAMBULISHA PINDI TU UINGIAPO KATIKA GROUP HILI... JINA, MKOA, SHUGHULI

TSA- PIG FARMING
 
Back
Top Bottom