Ugoni: Yalishawahi kukuta?....Soma hiki kisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugoni: Yalishawahi kukuta?....Soma hiki kisa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by platozoom, Feb 3, 2012.

 1. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Ni mwaka 2011 kuna rafiki yangu niliefahamiana wakati nilipoenda Kigoma. Baada ya kusita kwingi akanihadithia kisa chake kinachomsononesha mpaka leo.
  Aliishi na mke wake kwa muda wa miaka 3 na kupata mtoto mmoja, jamaa ni mfanyabiashara wa kawaida na mara nyingi huwa anasafiri kwenda Mwanza,kahama na Dar kununua bidhaa na kuzipeleka Kigoma kama kawaida.

  Siku asiyoisahau maishani alirudi nyumbani majira ya saa 6 usiku nyumbani kwake baada ya kukatisha safari kwa sababu gari ya mizigo aliyokuwa anaitumia iliharibika njiani.Bila hofu yeyote akagonga hodi mara kama tano hivi,ya sita akaja shemeji yake ambaye ni mdogo wa mkewe kumfungulia - Akastuka! Hii haikuwa kawaida,akauliza "dada yako yuko wapi?" mdogo mtu hana jibu(umri km miaka 7 hivi). Kuingia ndani hajamkuta mkewe bali mwanae amelala kitandani.

  Alipandwa na hasira huku akitetemeka,akachukua kisu na kutoka nje......swali likawa anaenda kumtafuta wapi? akili ikamtuma aende guest iliyokuwa umbali wa mita kama 500 toka pale anapoishi,akajivuta mpaka pembeni mwa guest ile, tena swali likamjia amuulize mlinzi? hapana.Akaka pembeni huku anatazama mlango wa guest.

  Saa 7......8..9 mpaka saa kumi hajaona mtu anatoka nje na ghafla mvua ya manyunyu ikawa inapuliza huku akivumilia.Akili yote imemtuma ni pale ndipo alipo mke wake, na mawazo lukuki kichwani.

  Ilipotimu saa 12 mlinzi akafungua mlango na geti.Jamaa akapata fursa ya kuingia...........akavuka mlango wa kwanza..wa pili akasikia unafunguliwa.Lahaula alietoka wa kwanza ni mkewe,kijasho kikamtoka.Akamshika mkono na kumrudisha chumbani.
  Lengo lilikuwa ni kuua....huku akitoa machozi akamuuliza mgoni wake "wewe ***********umetumia kondomu" akajibu ndio.
  Mgoni karibia kuzirai............jamaa akamvuta mke wake "nikuue wewe ***?" .Mkewe akaomba sana msamaha.

  Kifupi jamaa alitoka ndani na kuishia kwake na kumfungashia virago mkewe.Mpaka leo hajasahau kilichompata na imemuwia vigumu kuponya majeraha ya moyo na hajui ni vipi alishindwa kutimiza lengo alipofika Guest,kila anapokumbuka hana hamu ya kuoa tena.Nasaha za wazee wa pande zote mbili hazikusaidia kuokoa ndoa hiyo.
   
 2. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 581
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Dah! Inasikitisha sana!
   
 3. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  hiyo inaitwa ajali kazini kwa dunia ya kileo hicho ni kitu cha kawaida. Aoe mwanamke mwingine ila asimwamini mwanamke maana hawaaminiki hawa viumbe
   
 4. client3

  client3 JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 6, 2007
  Messages: 742
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  ni kweli viumbe hivi haviaminiki hasa baada ya kuushtukia mchezo uchezwao na wanaume.
  mimi nafikiri wakati wa kuambizana ukweli umefika,kama mtu ana uhitaji wa kitu cha nje funguka kwa kutoa sababu zako,kama zina mashiko mnaweza kuruhusiana,mfano namtamani mwanamme mwingine anayenisifia na kuonesha ananijali mm na hisia zangu,nina shida ya pesa ambazo nadhani naweza kupata nikiwa na mwingine,nahisi namtamani mwanamke yule wewe hunivutii kama awali, nk maana hivi ndo vyanzo......la sivyo unafiki utatumaliza.
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ndoa baada ya fumanizi pale mfumaniwa anapokuwa ni mwanamke kunakuwa na nafasi ndogo sana kama tundu la sindano ndoa hiyo kuendelelea. Hiyo inatokana na aina ya malezi tuliyopewa sisi wanaume, inahitaji msuli wa moyo kwa mwanaume kukubali kuendelea na ndoa baada ya kumfumania mkewe. mara nyingi hata ndoa inapoendelea mapenzi yanakuwa ni kama hayapo labda tu huyo mwanaume awe na utambuzi wa hali ya juu na mwenye kumudu kudhibiti kisirani.
  Kwa wanwake ni tofauti sana, wao wanaweza kuendelea na ndoa na mapenzi yakawa motomoto baada ya fumanizi kwani wao ni wasemehevu sana na ni wenye subira. Nimeshuhudia rafiki yangu amewahi kufumaniwa na mkewe zaidi ya mara tano lakini ndoa yake imeendelea kuwa imara hadi leo, jamaa mwenyewe imebidi aache ubazazi wake. Siku moja huyo mke wa rafiki yangu alinieleza kwamba ilibidi abadilike yeye kwa sababu tatizo lilikuwa ni lake, hakufafanua alikuwa na tatizo gani, lakini nilimuelewa. mara nyingi sisi ndio tunaotakiwa kubadilika ili wale tunaowapenda wapate kubadilika. kuna mambo matatu ambayo tunaweza kuyatumie ili kukabiiliana na changamoto za ndoa. Nayo ni haya:
  1. Kubadilika
  2. Kujiondoa
  3. Kukubaliana na hali halisi ili tuishi
   
 6. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Nahisi ni sahihi lakini mbona sijaona uvumilivu na kusameheana? au umefanya makusudi ili mama mdogo ajihadhari? hata mimi aliponihadithia niliduwaa na kuwa mdogo kama piriton na suala la kuoa kwangu limekuwa kitendawili kidogo.
   
 7. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmmh! Mpe pole.
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Bwana weye kwakuwakandia wanawake duh! Ebu mwambie arudishe Moyo amrudie mkewe mungu hapendi Talaka.
   
 9. M

  Muggssy Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tusiskilize upande mmoja may be huyuu jama alikua part of the problem. Watu wengi wanakua bizzy na mambo ya biashara hadi wanasahau majukum ya kifamilia. Ikumbukwe kwamba wanawake wengi kwasababu ya idleness nyumbani wanahitaji phycological compesation ambayo ni kushugulikiwa ipasavyo ili kiziba hiyo gap ambaye inakua ina miss kwahiyo mwanaume anapokua bizzy na kazi na kusahau jukum lake la msingi (Haki ya msingi ya kumpa mwanamke ndani ya ndoa) anavo enda nje hua anatafuta compesation ambaya anaikosa ndani ya nyumba
   
 10. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hilo la kurudiana ndio hataki kusikia.Lakini baya zaidi alikuja kugundua kwamba dada yake mkubwa na huyo mke wake (shemeji) alikuwa anajua mchezo! alipoipata na hiyo ndio ikamaliza kabisa mchezo.
   
 11. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Mmmh hapo sitii neno maana sikuwahi kushuhudia game lao!
   
 12. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  mpe pole na mwambie amsamehe mkewe na warudiane
   
 13. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda signature yako
   
 14. c

  chief2662 Member

  #14
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  da 2tafute pesa 2 wanawake wapo 2 tena washenzi kama hao
   
 15. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Pole yake aisee kwa kuwa jambo hilo ni noma sana
   
 16. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Aachane na viumbe hawa dhaifu; usipofanikiwa kupata mwanamke bora ukaokota tamtam ya mtaa imekula kwako - bora kuacha kuoa kabisa. Akitaka watoto achukue li-mwanamke jingine alipe ukweli - lizae naye then kila mmoja achukue hamsini zake - INAUMA SANA.
   
 17. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Shida sio kusamehe; ni je aliyesamehewa ana thamini msamaha aliopewa? na hili halijalishi iwe ni kwa manaume ama mwanamke; so tusimlaumu sana rafiki yako; huenda ana vigezo kuwa msamaha wake hautokuwa na thamani kwa msamehewa.......namsifu kwa maamuzi magumu na namtakia kila la kheri atasahau siku moja!
   
 18. M

  MAGISAC Member

  #18
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa wanawake Mungu katuumba tofauti sana tunajua kusamehe sana. Ni kosa kubwa kwa mwanamke kutoka nje ya ndoa lakini sio kwa mwanamme.
   
 19. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  jamaa ana moyo kweli...mi ningeua nadhani
   
 20. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #20
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hayajawahi kunikuta na Mungu anisaidie yasinikute
   
Loading...